The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesisitiza kuwa ataendelea kuiunga mkono Urusi katika vita dhidi ya Ukraine. Ameitoa kauli hiyo katika mkutano wake na Waziri wa Mambo ya nje ya Urusi Sergei Lavrov mjini Wonsan.Kim Jong Un amesema nchi hizo mbili zina mitazamo inayofanana kuhusu masuala yote ya kimkakati na Pyongyang iko tayari kuunga mkono hatua zote za utawala wa Moscow katika kukabiliana na kiini cha mzozo wa Ukraine.
Wakati huohuo Waziri wa Mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amezionya Marekani, Korea Kusini na Japan dhidi ya kuunda ushirika wa kiusalama unaoilenga Korea Kaskazini.
Pyongyang imekuwa ikiiunga mkono Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine kwa kuipa silaha na wanajeshi. Nazo Marekani, Korea Kusini na Japan zimetanua luteka za pamoja za kijeshi kutokana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini unaozidi kukua.