Korea kaskazini ndani ya Africa

Korea kaskazini ndani ya Africa

Smartkahn

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2020
Posts
889
Reaction score
1,490
Misukule wanauliza pengine mlio timamu muwasaidie kufikisha maswali yao kwa watawala wake

1).Lengo nia au dhamira ya mtawala/watawala ni ipi?

2).Wanasema mnataka wao wawaeleweje?
1766472176937.Screenshot_20251223-094205.png

Think wisely and take action.
 
Sijaona maamuzi au kitendo cha kiungwana chochote kilichochukuliwa kuendana na uzito wa jambo lilitokea kwa makusudi...

Hii maana yake nini!?
 
Misukule wanauliza pengine mlio timamu muwasaidie kufikisha maswali yao kwa watawala wake

1).Lengo nia au dhamira ya mtawala/watawala ni ipi?

2).Wanasema mnataka wao wawaeleweje?
View attachment 3519368
Think wisely and take action.
Waandamanaji hao AKA Misukule wanadai wanahoja na zinamashiko, hivyo wasikilizwe,! pasipo na excuses yoyote ile.

Hapa issue siyo kuzuia au kudhibiti maandamano, hapa issue ni kutafuta mzizi wa tatizo, kwanini watu wanaandamana! Baaasi...!!!

Hawachoki kuendelea kutoa maoni yao, Wadau licha yakua walishashauri kabla wakapata kusema haya...
Ulishawahi kukosea kujibu maswali, ukapewa nafasi ya kufanya masahihisho (correction), unakusanya baadae matokeo yanatoka, umekosa maswali yote tena.😎

Taarifa(picha) za watu Maalumu zitakuwa(wekwa) hadharani.

Hali hiyo itakua ishara ya maboresho/masahihisho yasiyo sahihi katika nyaraka, yatakayofanyika kwa siri kubwa na amateur baada ya kuamriwa gizani katika hari ya hewa yenye manyunyu ya mvua.

Baada ya kukosea na kujua wapi tumekosea hututarajii kukosea tena, hasa ukizingatia maboresho/masahihisho yanafanywa na kundi la watu(jopo, tume, Taasisi) tofauti na hapo ni makusudi yenye dhamira mbaya si kwa taifa bali kwa atakayebeba mzigo wa lawama(who (wahusika wawe makini(weledi)))

1. Naam... Sababu kubwa ni Siasa kwa maana ya siasa kuelekea uchaguzi, huku ikikolezwa na mafahari wawili wakimataifa wasioweza kukaa katika zizi moja.

Hao mafahari wananguvu na wanaingilia hadi mambo nyeti ni wakongwe katika gemu ya siasa mithili ya kungwi/somo ambaye ana mingle katika ndoa ya watu na kutoa manual script/ratiba ya nini, nani, wapi sangapi, na kivipi faragha yenu kifanyike.

Sasa tuachane na hao mafahali tujadili sisi mifigo wafuasi.

2.Sababu ndogo ndogo

Kimsingi hali hii tunayopitia kipindi hiki kuelekea uchaguzi chanzo kikuu/mzizi wa tatizo ni serikali yenyewe inazalisha tatizo badala ya kutatua tatizo yenyewe inalikuza tatizo.

Kwanini nasema inalikuza tatizo ni kwasababu baadhi ya raia wenye kujali wanapoona shida mahali wanasubiri mrejesho/ufumbuzi wa tatizo wanapoona hakuna kinachofanyika, kisaikolokjia hilo gape likisipo zibwa kwa hatua stahiki automatically binadamu ataliziba yeye kwa mawazo/idea au matendo anayoyajua yeye.

Pindi ananyanyuka na hoja mawazo au vitendo vyake binafsi moja kwa moja serikali inamjia juu na kumuona mkosoaji anayeikashifu serikali(viongozi) anaonekana amevunja sheria na anachukuliwa hatua kama kukamatwa na polisi kufikishwa mahakamani... Ilhali chanzo cha tatizo na mwenye makosa ni uongozi kuto kuwajibika kukosa weledi katika majukumu yao matokeo yake wanaacha mambo mengi wazi wananchi wakiyaona na kupigia kelele inakuwa nongwa.

Hii sio sawa nashauri serikali tekelezeni wajibu wenu ipasavyo.

Kwa mwenendo huu na ulimwengu ulivyofunguka hivi sitarajii hali iendelee kuwa hivi hivi kwa kwa afya ya nchi, hivyo basi mabadiliko na maboresho ni muhimu sana... Na kama hakuna nia yoyote ya mabadiliko ya kanuni sheria basi watawala wahakikishe nchi inajifungia piga propaganda raia wenu kama wanavyofanya North Korea bila hivyo "patachimbika, dawa inachemka, tutakua kujenga ukuta tusipo ziba ufa"

Hitimisho
Tunatarajia nini kama viongozi tutakua hututimizi majukumu yetu ipasavyo na kwa weledi tunataka tugundue nini? Hali hii inayoendelea sio nzuri na ni uthibitisho kwamba kunamahali tunafeli.

Asante.

Sitaki kuamini kwamba siasa za ndani ndio zimetufikisha hatua hii...

Ila inawezekana Taifa linapokea vitisho vya kiusalama vinayopelekea kua na hari hii tuliyonayo na watawala hawana namna bali ni kutii

Kama sio tatizo ni nini!? Mbona mambo mengi yanaepukika, tuache upumqavu/upu-uzi huo mara moja.

Hizi ni assumption/dhana ya kwamba kuna;

=>Deep State.
Kuna kila dalili maamuzi ya nchi yanatolewa na watu ambao hawapo katika utawala na pengine sio asili na raia wa nchi licha ya kuwa anaewasilisha maamuzi hayo ni kiongozi wa nchi ila sio hiari yake na hayana baraka zake.(Mateka wa deep state).


=>Uhandisi Jamii.
Kuna kila dalili wananchi kimkakati wameandaliwa kisaikolokjia(deep) kupitia madhaifu migogoro, na tofauti tulizokuanazo tokea uhuru.

Kwa wewe raia iyo fikra na hizo hasira ulizonazo juu ya utawala si bahati mbaya kuna wataalamu wametaka uwe na hali hiyo(wana jambo lao).

=>Survival Mode:
Wananchi wako katika hatari na hari ya taharuki, wasijue waegemee wapi na wamuamini nani na hakuna anaejali, hali kama hii hupelekea liwalo na liwe.

Assumption hizi zinaweza kuwa kweli ama sio kweli.

JE KAMA NI KWELI TUTARAJIE NINI!?

1.Hatari ya vitishio vya usalama kuikumba nchi kama vile;







2.Kuwa watumwa ndani ya nchi yetu, uchumi na fursa za kiuchumi ikiwemo rasilimali hatutakua na maamuzi nazo hata kunufaika nazo...uchumi utakua sawa lakini majority tutakuwa walala hoi na wafanyakazi katika makampuni kutoka nje.

3.Nchi kuendeshwa kijeshi na kiimla kama tunavyosikia huko Korea.



NA KAMA ASSUMPTION HIZI SI ZA KWELI.
Basi zoezi la uchaguzi lisimamishwe kamati ziundwe tujitathmini tuweke
tofauti zetu pembeni tukishakuwa sawa ndio tuendelee na zoezi maana mambo yamekuwa mabaya zaidi.

Ni decisive minute... Inawezekana. Tofauti na hapo nchi inakua ipo rehani maadui wanaweza kutumia nafasi hiyo kutuvuruga kama wanavyovuruga sehemu nyingine huko.

Kimsingi mzizi wa fitna (root cause) ni au umeanzia serikalini.

Haiwezekani watu wote hao wakawa wamekosea harafu viongozi ndio mkawa sahihi.

Hadi hayo yote yanatokea serikali ilikua wapi? maana ndie viongozi! wanaotegemewa na wananchi.
Kutokua muwazi kunaweza kusababisha suluhu isipatikane na pia kwa namna moja ama nyingine kuongeza tatizo zaidi.


Tunafahamu Binadamu sio malaika hivyo tukikosea tukubali makosa, kukosolewa na kuelekezwa...

Mambo mengi yaliotokea kwa asilimia kubwa yalikua yanazungumzika na watu walishauli. (tatizo ni maslahi ing'i ya vene)

Binadamu tunategemeana na ndio maana ya serikali, kuna wizara mbalimbali kwa pamoja zinaunda mfumo unaoendesha nchi.

Ni kufilisika kwa hekima, endapo yatakuwa yanatokea matatizo katika taifa arafu analaumiwa mwananchi... Ilhali nchi hiyo inauongozi. Hata tukisema uongozi haupaswi kulaumiwa bali wawajibishwe wananchi bado itakua haingii akilini, kwasababu tatizo linaenda hadi linaleta madhara hao viongozi wenye dhamana walikua wapi na wajibu wao ni upi!? na nani awajibishwe kiongozi au mwananchi!? (Finu figwe fitagarye)

Hadi apo unaweza ukaona incopitence iko wapi... Kuna kauli zinatolewa na viongozi katika namna ambayo inakuacha unastaajabu pale... Unaanza kujiuliza maswali ivi maadili yalienda wapi, kuna wazee/washauri wenye busara kweli huko juu!?

No(kipindi cha kina Mh. Mkapa ukisikiliza speech za viongozi kama ulikua na njaa unajikuta umeshiba na una-li-feel taifa lako).

Hitimisho;
Ninapendekeza Raisi apate likizo ya siku 14 huku akitizamwa afya hasa (CNS)

Wakati huo washauri wake wawe wanapiga warm-up ya ku-deliver nondo zilizotukuka... Kwamaana ye ndio public figure isitoshe anaongoza watu million 70 na sio wadudu.
 
Back
Top Bottom