Kongole kwako Profesa Jay kuwa mtangazaji wa redio Clouds

Ni mbunge wa zamani au aliyewahi kuwa mbunge sio mstaafu,huyo aligombea tena akashindwa kwa mujibu wa matokeo ya tume ya uchaguzi hakuwahi kustaafu naona hili neno kustaafu siku hizi linatumika vibaya.
Binafsi nawajua wabunge kadhaa waliowahi kustaafu mfano Marehemu Mzindakaya, Marehemu Sitta,Mzee Edger Majogo,Mzee Pinda hawa waliamua kuacha kugombea wenyewe baada ya kutumikia ubunge kwa muda fulani na wakafikia uamuzi wa kuachia wengine wabebe jukumu lakini sio hawa wanaogombea na kushindwa waitwe wastaafu.
Tena mbunge wa binadamu na wanyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza siamini kama ni kweli

Na kama ni kweli basi mzee baba atakua kaishiwa mbinu kiasi cha kwenda kuajiriwa clouds kwa level ya mtangazaji

Kwa jinsi Prof alivyojijenga sio tena mtu wa kuajiriwa kwenye viposition vidogo dogo kama baba levo

Kwa level alizofikia anatakiwa kuwa boss wa issue zake na kama ni kuajiriwa basi iwe kwenye position za maana haswa

Lakini kama kaishiwa mbinu basi hakuna namna ajibanze tu hapo mjengoni clouds
 
Kutoka Ubunge hadi utangazaji ni failure.

Hivi kweli Professor J. ameshindwa hata kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kule Morogoro, anaishia kuwa mtangazaji?

Kiinua mgongo alichopata kwenye Ubunge ni mtaji tosha wa kuanzisha kilimo cha kisasa kuliko kuwa mpiga kelele redioni.
Vp keshafukuzwa hapo clouds?maana simsikii tena
 
Kwa upande mmoja nimpe pongezi kwa maamuzi binafsi ya kwenda kuwa mtangazaji clouds.

Ila kwa upande mwingine wa kwangu binafsi simpi pongezi kwa uamuzi aliofanya. Kwa level yake na hassle ya mda mrefu aliyofanya, mpaka kufikia kuwa mbunge, ametengeneza brand kubwa sana.

Nilitegemea atengeze ajira kwa vijana na angalau afungue redio yake binafsi! Kwa brand yake nina uhakika ingefanya vizuri sana.

Angekuwa amefanya la maana sana kuliko kwenda kuishi kwa masharti ya mwisho wa mwezi na kufanyia kazi mawazo ya mtu.

Profesa Jay,wee ni brand kubwa hebu jiongeze zaidi, acha hizo, wee ni role model wa vijana wengi, usiwaangushe!!
kwnn humshangai millard ayo kung'ang'ania clouds pia badala ya kufungua tv au redio yake.
 
kwnn humshangai millard ayo kung'ang'ania clouds pia badala ya kufungua tv au redio yake.
Nadhani sio sahihi sana kulinganisha hawa watu, kuna utofauti

Hata hivyo Ayo amejikita zaidi kwenye Online media ambayo pia CMG wana ubia
Ayo ni zaidi ya muajiriwa pale CMG, ameajiriwa na ni mmbia na CMG kwenye online media zake

Prof kama angekua kaajiriwa pale ingekuwa kama akina Jose Mara, Baba Lovo, Fidah Amani nk ambao wao ni watangazaji tu

Ila huu ni uzushi tu Prof haja ajiriwa pale
 
Wale ndugu zangu walio kunywa maji ya bendera ya vyama vyao vya siasa "......clouds CCM........ mimi si sikilizi Clouds sababu ni CCM......",haya sasa Prof J huyo mjengoni,sijui mtampokonya uwanachama.
Vipi bado anaendelea kusikika hapo ccm radio!?
 
Pongezi kwako kwa maamuzi hayo ya kuwa mtangazaji bado ni fursa nzuri naomba nikutakie heri na wanaJF tumtakie heri mbunge huyu mstaafu wa Mikumi.

--
Clouds kupitia mitandao ya kijamii wameandika haya

Jana kwenye mitandao yetu ya kijamii tulisema leo kwenye #PowerBreakFast kwa mara ya kwanza utasikia sauti ya usajili mpya... Ladies and gentlemen na huyu @ProfessorJayTz ndiyo usajili mpya ndani ya PB.

Hii Kwake sio kama ajira,inawezekana anatumika kwa umaharufu wake,ni mwanamuziki,aliwahi kuwa Mbunge,kwahiyo ana wafuasi wengi kwenye jamii,
Why not use tallent and popuralism to make extra monies!!!?
 
Wewe ndiye uliyesapoti kuwa jamaa anafanya utangazaji hapo redioni na ukawananga wale wanaosema hawasikilizi clouds redio ya ccm. Umesahau au umejisahaulisha!?
Sijasahau hoja yangu nimeijenga kutokana na maada ilivyo andikwa, so unaweza ukaMP aliye andika hii thread akakupa majibu.
 
Back
Top Bottom