Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,198
- 25,517
Waungwana wa JF nawasalimu,
Nipo safarini kuelekea Kigoma kikazi. Hivi sasa tunatua Uwanja wa Ndege wa Tabora kwakuwa tunapitia hapa kwenda Kigoma. Tupo na Ndege TC 128 aina ya bombardier. Nalazimika kulipongeza Shirika letu la Ndege kwa kuimarisha huduma.
Nimekuwa nikisafiri na Ndege za AirTanzania kwa muda mrefu hapa nchini na hata nje ya nchi. Nikiri kuwa kwa safari za ndani ya nchi,huduma zimeimarika sana. Kuanzia Cabin Crew, Marubani na Watumishi wengine wa AirTanzania, ukarimu na umakini unatamalaki.
Kwa safari zangu za Kigoma kwa Ndege za kuelekea Burundi na kupitia Tabora, leo nimeshuhudia Ndege yetu ikibakiwa na siti tupu tatu tu. Ni jambo la kutia faraja na kuonyesha wananchi kuridhishwa na huduma za AirTanzania. Kongole sana kwenu AirTanzania!
Kuimarika kwa huduma za AirTanzania ni kuisimamia kwa vitendo ndoto ya Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli aliyejitoa kwa uwezo na maarifa yake yote kuhakikisha AirTanzania inaimarika na kuwa nembo yetu kitaifa.
Najivunia AirTanzania, najivunia kuwa mtanzania!