Kongamano la Kitaifa la kumpongeza Rais Magufuli lasitishwa ghafla

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kongamano kubwa la kitaifa la kumpongeza Rais John Magufuli kwa ushindi aliupata, Lililokuwa limeandaliwa na Taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa Qaadiriyah, lililokuwa lifanyike jijini Arusha, Novemba 30 mwaka huu limeahirishwa.

Akiongea na vyombo vya habari, msemaji wa Twariqa Taifa, Sheikh Haruna Husein alisema kuwa kongamano hilo lililokuwa linajumuisha taasisi mbalimbali za dini,viongozi wa Mila, viongozi wa vyama vya siasa na serikali ,limeshindwa kufanyika kwa muda uliopangwa hadi hapo litakapoandaliwa tena.

"Tupo hapa kuwajulisha waalikwa wote wa kongamano la Kumpongeza rais Magufuli
Kwamba, kongamano hilo lililopangwa kufanyika hapo kesho Novemba 30 mwaka huu limeahirishwa hadi hapo litakopangwa tena, hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza"alisema Haruna

Naye Asheikh Sirajunuur ,Halifa wa mkoa wa Singida aliwashukuru viongozi wa dini waliosimama kidete kuliombea taifa katika kipindi cha uchaguzi na kupelekea uchaguzi kufanyika kwa amani na kuwataka waendelee na majukumu yao hayo na kuepuka kutumika kisiasa.

IMG_20201129_121159.jpg
IMG_20201129_120756.jpg
 
Taasis za dini ziache kujipendekeza na kujikomba kwa mamlaka.
Hii tabia ya kupongeza mambo ya kawaida ni unoko.
 
Kila mtu anajuwa kura zimeibwa, mashehe na wachungaji pia wanajua hilo, ila wameamua kujitoa ufahamu,
Bashiru nae eti anawapongeza mabalozi badala ya wakurugenzi na watendaji, hili kuficha aibu ya wizi!
 
Hizoo hela za kongamano kwanini wasizitumia kueneza dini? Au Mungu wao Ni ccm.

Hawajatoa tamko kulaani chadema kuwafukuza COVID 19.
 
Back
Top Bottom