Kongamano la CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano la CHADEMA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Albedo, Jan 9, 2010.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jamani nimesoma kupitia vyombo vya habari kwamba leo CHADEMA watakuwa DDC Mlimani City na Kongamano la Wasomi wa vyuo vikuu!
  Kama lipo tupeane updates ya nini kinaendelea!
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  He hamna wana CHADEMA huko au kongamano limefulia?
   
 3. M

  Muheza Member

  #3
  Jan 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati mnaenda kongamano la wasomi DDC Mlimani City, CCM wanaenda vijijini kwa wananchi. Hapo kweli mtaweza kushindana na CCM?

  Wapiga kura wako wilayani na vijijini na wala sio hao wajanja wa mjini.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  halafu mnaenda DDC wakuu?
  si mngeenda hata N'KURUMAH HALL PALE?
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kule Nkrumah hall itakuwa vigumu sana na pia kumbuka hata sheria ambayo inakataza siasa katika vyuo vikuu lakini naona hata sheria yetu ni hafifu sana katika kujua na hata kutambua umuhimu wa siasa kwenye vyuo vyetu
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ....mbona enzi zile muungwana aliwahi kwenda,akaenda muzumbe university na aliuza sana kadi za UVCCM?
   
 7. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  lazima uende kwa wasomi ili kuattract able people kuja kwenye chama chako na sio kutegemea viongozi makanjanja.
  unahitaji watu wenye uwelewa kuwashauri watu (wapiga kura), ccm wao wanasimamisha mtu yeyote na pesa ndio inafanya kazi.

  kama ushindi dar basi huwezi kushinda TZ, mabadiliko yanaanzia mjini. ndio maana NCCR kilikuwa maarufu kwa ajili kilikuwa maarufu dar. ccm leo hii hawaachii hata jimbo moja la dar kwa ajili wanajua kitaeneza chama mpaka mikoa mingine, watu wa mikoani look up to what dar is doing.
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  wako busy na kongamano, unataka upewe update na wakati watu wanaconcentrate
   
 9. M

  Muheza Member

  #9
  Jan 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuna wasomi na able people ambao bado mpaka leo hawaijui CHADEMA, basi mna kazi.

  Tatizo sio kwa wasomi, tatizo ni huko wilayani na vijijini.

  Wasomi wengi ni opportunists na wanaangalia upepo. Wakiona chama kina nafasi ya kushinda, watakuja wengi tu. Kumbuka NCCR ya Mrema 1995.

  Nawatakia mafanikio mema kwenye kongamano lenu.
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jaribu kutazama uone jinsi gani CCM waliweza kufanya siasa katika vyuo vikuu na siyo vyama vya upinzania na hivyo ndio unaweza kuona kuwa CCm wanatumia nafasi yao katika kubana demokrasia, Katika Nchi za mwezetu kuna club ya Republican, Democratic katika vyuo karibu vyote America na hii ndio unaweza kupata viongozi bora. Labda mzee alijua kuwa hata kama akisema kuwa anataka kadi ya CCM hakuna mtu wa kumuliza
   
 11. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kongamano linaendelea Kamanda MBOWE amewakabidhi kadi wanachama wapya zaidi ya 500.. Ukumbi umefurika wanavyuo toka UDSM,UDOM,SUA,MZUMBE na vyuo vingine wamefika..Wana UDSM Tumeapa kumpigania Prof.Baregu..Sasa TUNDU LISSU anaongea...Mapambano yanaendelea..
   
 12. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru sana tunaomba uendelee kutupa habari zaidi wengine tuko mbali lakini tu pamoja.
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Asante sana Jambo, endelea kutujuza na kama ukiweza weka picha za Kongamano hapa

  Asante sana mkuu
   
 14. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu Geoff
  Mimi nafikiri cha msingi hapa tuangalie mada zenyewe si wapi zimetolewa, unaweza kutoa mada ghorofani isifae na iliyotolewa chini ya mti ikawa ndiyo muhimu zaidi.
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,640
  Likes Received: 21,851
  Trophy Points: 280
  Kusubiri kanga ,Tshirt na kofia? Hayo sio makusudio ya Chadema.
   
 16. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ungenisoma vizuri, sijasema wasomi hawaijui chadema bali kuwa attract (nimeji qoute hapo chini). kukijua chama ni kitu kingine na kuwavutia waingie kwenye chama ni kitu kingine.
  hata hao ccm wanaoenda vijijini sio kama wananchi wa vijijini hawaijui ccm hapana, bali ccm wanaenda kuwavutia.
  by the way mimi sio mwanachadema ni mtu ambaye napenda upinzani ukue TZ.

   
Loading...