konda mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

konda mtoto

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Sugar wa Ukweli, Apr 1, 2012.

 1. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shakira alimnunulia mtoto wake wa miaka 6 hivi kigari cha kuchezea chenye muundo wa basi. Siku moja wakati Shakira yupo jikoni mwanae alikuwa sebuleni anachezea kile kigari. Shakira akawa anamsikiliza mtoto wake wakati anaongea na kigari na vitoi vyake vingine. Mtoto akatoa sauti kama ya gari linavyofanya kisha akapiga breki na kusema “Haya mwisho wa gari sishobokei abilia wa mtu toeni makalio yenu katika siti muende makwenu. Na nyinyi mlio kituoni kama mna safari ingizeni makalio yenu katika siti haraka tunawahi mingo sasa hivi. Kama unajijua we ni denti nisikute makalio yako katika kiti nitakupasua bichwa lako” Shakira aliposikia maneno hayo toka kwa mtoto wake akaenda sebuleni kwa hasira na kumsema mtoto wake “Lugha gani hiyo chafu unayotumia humu ndani, nisikusikie tena. Nenda chumbani kwenu ukakae bila kucheza kwa muda wa masaa mawili kama adhabu yako.” Mtoto wake akaenda chumbani huku anatia huruma na kutumikia adhabu yake ya masaa mawili bila ya kucheza. Baadae akatoka na kuendelea kucheza. Shakira alikuwa bado yupo jikoni akamsikia mtoto wake akicheza tena na kuanza kama mwanzo. Yule mtoto alipofunga breki ya kigari chake akaanza tena “Wapendwa abilia watu tunashukuru kwa kuchagua gari letu, Huu ndio mwisho wetu wa safari na tunatumai mmefurahia huduma yetu, karibuni sana. Haya mlio kituoni karibuni sana katika gari letu ndio linaanza safari ya kuelekea mjini, safirini nasi kwa safari ya utulivu na salama” Shakira alipokuwa anasikia maneno haya akafurahi sana kuona mwanae amejeirekebisha, akaanza kutabasamu wakati mtoto anaendelea kuongea, mtoto akaendelea kumalizia kuongea na abiria wanaotaka kupanda gari “Na kama kuna abiria yeyote aliyesubiri kituoni kwa masaa mawili yaliyopita na amekasirishwa na kitendo hicho aende akapeleke malalamiko yake jikoni kuna jitu limeweka makalio yake katika kigoda kazi yake kunisikiliza na kunipa kifungo ninapokosea”
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
 3. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Huu ni uxxnge kukopi habari iliyopo ukurasa huu na kuipest hapahapa!
   
 4. driller

  driller JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 1,119
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mh mbona maneno makali sana jamani..!? kakosea kidogo tu wazee..!
   
Loading...