Komu: Magufuli akishinda tena urais, naacha Mageuzi na kurudi Kijijini kwangu kulima

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,840
"Magufuli Akishinda Tena Urais, Naacha Mageuzi na Kurudi Kijijini Kwangu Kulima": Nasaha za Ndugu Antony Kalisti Komu kwa Wanasiasa Vijana.

Na Ado Shaibu
Juzi, mimi na Ndugu Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama chetu tulisafiri pamoja hadi Kakonko Mkoani Kigoma kukiwakilisha ACT Wazalendo kwenye mazishi ya Mwalimu Bilago Mbunge wa Buyungu, Naibu Waziri Kivuli wa Elimu, Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi (Kigoma, Katavi na Tabora) na Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA.

Tulipofika Dodoma, Ndugu Antony Komu Mbunge wa Moshi Vijijini na Mmoja wa wanasiasa wa mwanzoni kabisa wakati wa vuguvugu la mageuzi ya vyama vingi alijiunga nasi kwenye gari.Moyoni nilifahamu kusafiri mamia ya kilomita na Ndugu Komu na Zitto kwa pamoja ilikuwa ni fursa maridhawa ya kujifunza.

Baada ya mazungumzo ya hapa na pale baina yake na Ndugu Zitto kuhusu masuala ya Bunge, mwelekeo wa nchi na legacy ya Marehemu Bilago, Ndugu Komu alinigeukia mimi na kuniuliza kwa sauti ya utulivu na udadisi kama ilivyo desturi yake; "Ado unaionaje hali ya siasa nchini hivi sasa?". Ninamjibu upesiupesi "Hali ni mbaya sana". Ndugu Komu anacheka na kunitania "Hali inawezaje kuwa ngumu wakati upo kwenye gari kama hili na Kiongozi wako amekuweka siti ya mbele Kama Waziri?" (Anacheka tena na kuendelea). "Enzi zetu wakati mageuzi yanaingia nchini hatukuwa na magari. Tulijenga mageuzi mguu kwa mguu. Ukitaka gari labda upate lifti ya Dk. Tenga. Yeye alikuwa na gari la Legal Aid. Kwa hiyo ukitaka kutoka Chuoni kwenda kwenye harakati anakusokomeza nyuma huko usionekane.

Selasini (Mbunge wa Rombo) alikuwa Transport Officer wa Tanzania Housing Bank. Yeye alitoa kwa siri gari la kazini kwake tukalitumia kwa kificho kwenye harakati za mageuzi. Unatia majembe kwenye gari utadhani mnakwenda kwenye kazi maalum kumbe mnakwenda kwenye mageuzi. Mkifika karibu gari mnaliacha njiani mnaanza kutembea kwa miguu hadi eneo mlilokusudia. Mnawahubiria watu kuhusu mageuzi hata Kama ni watatu.."
"Lakini, tofauti na zama zenu, hali ya mambo sasa ni mbaya sana. Haturuhusiwi kufanya siasa. Mikutano imefungiwa, vyombo vya habari vinezibwa midomo na usalama wa wanasiasa na wasemakweli wengine upo mashakani" Ninamdadisi

"Ni kweli. Demokrasia imevurugwa. Lakini, mimi ninautazama utawala wa Rais Magufuli Kama "A blessing in disguise" (Neema katika kadhia). Utawala wake umeshindwa kila mahala. Ni dhahiri kwamba uwezo wake wa kusimamia uchumi wa nchi ni mdogo. Kila sekta imevurugwa na hali ya maisha ya watu ni mbaya sana. Hii ni fursa kwa Wapinzani. Utawala wake ni 'a big failure' na unaishi kwa propaganda.

Swali la kujiuliza, Je wapinzani tumeitumia fursa hiyo ndani na nje ya Bunge? Tunao wajibu wa kuwa more organized na focused. Tumeweza kuwafanya wananchi waelewe madudu ya Magufuli? Tukilifanya hili vizuri watanzania bila kujali vyama watatuunga mkono kwa sababu utawala huu unamuathiri kila mtu"

Anasimama kiasi kisha anaendelea:
"Miaka ya tisini tulikuwa na kizingiti cha kukabiliana na Nyerere. Yes, Nyerere campaigned against us, nchi nzima! Sasa hawana Nyerere. CCM imevurugwa maradufu na inaendelea kuvurugwa. CCM ya sasa si ile ya tisini au miaka iliyopita. Ni CCM mbovu iliyosheheni wageni na kuwaweka kando wabobezi na wakongwe. CCM ina-survive kwa nguvu ya dola na si nguvu ya hoja.

Tukijipanga vizuri, tukawa well organised, tukawa focused kwenye kusimamia masuala yao na kuyaongoza vyema maeneo tunayoyaongoza, mambo yatabadilika. Jambo la msingi hasa nyinyi vijana ambao mnafuatwa na mnarubuniwa rubuniwa ni kusimama imara"

Anacheka kidogo kisha anaongea kwa sauti ya utani "Kwa kweli mimi huyu jamaa (Magufuli) tukimshindwa safari hii (2020) nitaachana na mageuzi na kurudi kwetu kijijini kulima". Kisha anacheka tena.

Tunazungumza mambo mbalimbali ya nchi na wakati mwingine ya nje ya mipaka. Komu ni mfano wa Kitabu muhimu cha mageuzi. Anakumbuka karibu kila mtu na matukio muhimu kwenye vuguvugu la mageuzi ya kuleta vyama vingi Miaka ya tisini.

Ndani ya ACT Wazalendo, mfano wake ni Msafiri Mtemelwa, Naibu Katibu Mkuu Bara ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Vijana wa NCCR Mageuzi Miaka hiyo ya tisini. Naye akianza kukusimulia vitimbi na visa vya miaka hiyo, hamfiki mwisho. Bila shaka vijana wa sasa tunao wajibu wa kujifunza kutoka kwa Watangulizi wetu;
Urithi gani wa kufaa wanatuachia?
Mambo gani yasiyofaa na yakiyokwamisha kustawi kwa mageuzi waliyokumbatia nasi twapasa kuyaacha?
Mambo gani ni lazima kuyaendeleza?
Ni upi wajibu wetu wa sasa wa kimapambano? Tujiulize.

Ado Shaibu
Kibondo, Kigoma.
31 Mei 2018
 
Mwambieni aanze safari sasa ya kurudi kijijini kulima maana ushindi kwa Rais Magufuli 2020/upo wazi, tena Watanzania Wazalendo tungependa atawale milele.
Kama ni kushinda ni kwa kutumia Jeshi la Polisi na NEC ya CCM ni kweli ushindi uko wazi.

Lakini kama uchaguzi utakuwa HURU na wa HAKI, nami najiunga na Komu na kutamka kuwa kama kweli Magu atashinda nafasi ya Urais, nami pia nitajiunga na Komu kwenda kijijini kwangu na kwenda kulima Matembele!
 
Kumbe hamjajipanga? Halafu mnatilia shaka ushindi wa Maghufuli? Namuomba Komu aje aishi kwa kauli yake na isije ikawa vinginevyo! Nasubiri kuona!
 
Back
Top Bottom