Komu: Magufuli akishinda tena urais, naacha Mageuzi na kurudi Kijijini kwangu kulima

Kijijini sio mahali ya watu walio filisika akili huku utakufa, kazi kwenda mbele huku ni uwezo wa kutumia nguvu mwili akili na nyenzo sio maneno
 
Deg6sRsXkAAMMwu.jpg

Mbunge wa Moshi Vijijini Antony Kalisti Komu ameamua kuweka nadhiri ya kuachana na siasa na kurudi kijijini kulima kwa kudai kuwa endapo katika uchaguzi mkuu wa 2020 watashindwa kumtoa rais Magufuli madarakani.

Nadhiri hiyo ya Komu imewekwa wazi na Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT, Ado Shaibu ambaye amesema kwamba Mh. Komu ameyatoa hayo ya moyoni mbele yake na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wakati wakiwa njiani kuelekea Kakonko kuupumzisha mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Kasuku Bilago.

"Miaka ya tisini tulikuwa na kizingiti cha kukabiliana na Nyerere. Yes, Nyerere campaigned against us, nchi nzima. Sasa hawana Nyerere. CCM imevurugwa maradufu na inaendelea kuvurugwa. CCM ya sasa si ile ya tisini au miaka iliyopita. Ni CCM mbovu iliyosheheni wageni na kuwaweka kando wabobezi na wakongwe" Komu.

Ameongeza "CCM ina-survive kwa nguvu ya dola na si nguvu ya hoja. Tukijipanga vizuri, tukawa well organised, tukawa focused kwenye kusimamia masuala yao na kuyaongoza vyema maeneo tunayoyaongoza, mambo yatabadilika. Jambo la msingi hasa nyinyi vijana ambao mnafuatwa na mnarubuniwa rubuniwa ni kusimama imara"

Mh. Komu amesisitiza "Kwa kweli mimi Magufuli tukimshindwa safari hii (2020) nitaachana na mageuzi na kurudi kwetu kijijini kulima".

Mbali na hayo Mbunge huyo amewataka wabunge wa upinzani kujipanga na kujua kutumia fursa ndani ya utawala wa rais magufuli ili watanzania pasipo kujali vyama vyao waweze kuwaunga mkono.

Chanzo:EATV
 
Kila jambo duniani hapa lina mwisho wake. Ipo siku inakuja ccm nayo itafikia mwisho wake. Naona watu wanatoa kebihi kwa kauli ya Komu lakini ipo siku, nami naiona haiko mbali sana Mungu atasikia kilio cha watanzania.
 
Mwambieni aanze safari sasa ya kurudi kijijini kulima maana ushindi kwa Rais Magufuli 2020/upo wazi, tena Watanzania Wazalendo tungependa atawale milele.
Masahihisho kidogo Tume ya uchaguzj na polisi wanampenda kinoma na ndiyo watakao mfanya ashinde wananchi wapige kura wasipige yeye atatangazw mshindi
 
Back
Top Bottom