MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,090
- 22,373
Akiwa jijini Dar es Salaam, Manispaa ya Ubungo, Ndugu Kawaida ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa amerekodiwa akisema CCM ndiyo iliyopigania uhuru na pia imehusika na mapinduzi ya Zanzibar. Na baada ya hapo ndo ikaleta muungano.
Ikumbukwe uhuru wa Tanzania ulipatikana 1961 kupitia chama cha TANU wakati mapinduzi ya Zanzibar ni 1964 kupitia ASP. CCM ilizaliwa mwaka 1977 baada ya TANU na ASP kuungana.
Ifike sehemu hawa vijana wawe wanatafakari kabla ya kuongea jambo.
Pia Admin wa page ya UVCCM nae ni wa kulaumiwa kwa kukurupuka kupost. Komredi Kawaida alikuwa na point kubwa ila hakuiweka vizuri mwanzoni.
Ni kweli CCM ina uchungu na nchi hii ila kusema CCM ilipigania uhuru ni kuivuruga na kuipoteza historia ya nchi.
Mimi kama mzalendo ninawaasa vijana wa CCM wasikurupuke kutamka mambo wasiyo na uhakika nayo. Pia wajisomee mambo mbalimbali kuhusu historia ya nchi yao pendwa.