FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
KOMBORA KIOTANI-34
Kiota cha mapenzi kati ya Dedani na mkewe kilichukuliwa kwa muda kidogo na utamu pamoja na hisia kochokocho zenye fukuto la mahaba kwa muda kidogo hakuna aliyeona sababu maalum ya kumbania mwenzake.Ilikuwa hisia kali sana kwa Dedani na kwa mara moja Dedani alitambua fika kulikuwa na penzi zito kati yake na Kilua lakini kwa sasa mgawanyo na picha iliyojijenga kichwani mwake kati yake na Shunie ilikuwa kubwa sana nakuonesha mfadhaiko wa saikolojia baina ya kufanya maamuzi nakutoa jambo lenye faida na hasara kwa mkupukuo.Hii picha mpya ya Shunie kwenye ramani hii ilionesha wazi kushuku msimamo wake kwa mkewe kama kweli alimpenda na nia yenye udhati wa asili ilikuwa na uwezo wa kukabiliana naye kwamba saikolojia imeingia mdudu mpya.Alipambana na mdudu huyuu mpya na hata kumpuuzia akiamini fika katika kuta za nafsi zake kulikuwa na mwanamke mmoja tu ambaye ni Kilua.
Busu la kati ya mke na mume lilikuwa katika uzito wa mahaba na wao walikuwa kidogo mbali.Mlio wa mlango kufunguka pengine hawakuusikia au waliusikia na kuupuzia maana ilikuwa ni wakati wao na Kilua hakutaka mtu kuingia pale alitaka faragha hiyo na mumewe bila kidudu mtu kuingilia eneo lile huyu punguani anayeingia ana ajenda gani?Alikasirika sana.Kilua pamoja na Dedani walikuta mtu kawasimamia.
Wawili katika kumbatio la upendo wao waligeuza shingo zao nakumtizama mfunguaji wa mlango ambaye alisimama huku akitumbua macho asiamini alichoona ni kitu gani?Kilua alishtuka kumkuta ni Serambovu!Moyo ukampiga mkambi na yeye kutweta kwa wasiwasi uliomkubwa sana!Ni kama dunia ilisimama kwa sekunde kadhaa huku maasimu na wapenzi walikuwa mbele ya uwepo wao.Mara ya mwisho Dedani anakumbuka bwana huyu alimfumania ofisini kwa mkewe wakiwa katika mazingira hatarishi sana.Alikuwakuta mubashara wakizini na mkewe.Na tangu wakati huo hadi leo Dedani hakuwa na nafasi ya kumhoji mkewe na pengine kumshutumu kwa jambo lolote au hata kuwa na wasaa wakujua ilikuwaje Kilua na Dedani!Ujio wa Dedani ulichipua hasira kali sana kwa Dedani na kwa mara moja alijtamani kumshambulia huyu bwana kwa nguvu zote aweze kumdhibiti kabisa!Hasira!
Dedani aliona kama Serambovu anamtukana kwa kujitokeza mbele zao.Anajua fika mkewe alitoa angalizo kwa kuhitaji faragha na mumewe.Hata walinzi wa mkewe walihakikisha hilo sasa iweje huyu fala anakuja hadi hapa?Dedani alihisi kichefuchefu kikimpanda nakujiapiza kichwani mwake kwamba angemshughulikia huyu mwendawazimu kwa kuthubutu kumlia mkewe.Na angemshughulikia vilivyo alihitaji nafasi tu!
Kilua alitumia mwanya huyo kumuonesha Serambovu kwamba mumewe yupo kwenye ngome yake na yeye alihitaji faragha ya kutosha kwa mumewe bila kidudu mtu kuleta propaganda.Lakini pia hatia ilimla maana chumba hikihiki Kilua amekuwa akikitia najisi hasa alikitumia mara kadhaa kuchepuka na bwana Serambovu leo tena yupo na mumewe.
"Unafanya nini hapa?"alihoji Dedani kwa hasira akimtizama Serambovu.Ni wazi chuki kati yao ilikuwa dhahiri shairi bila kuificha.
"Samahani bwana Dedani sijajua upo hapa.Nilitaka tu kuongea na mheshimiwa."alijitetea Serambovu maana mbali na uadui wa kuibiana mke wawili hawa wana historia fulani huko nyuma ya kaurafiki.Dedani aliwahi kuwa msaada mkubwa sana kwa Serambovu nyakati fulani.Na hicho ndicho kitu kilimfanya Serambovu akikutana na Dedani uso kwa uso alikuwa hajielewi japo alidhamiria fika kumuangamiza kabisa na kumfuta kwenye ramani ya uso wa dunia.
"Hukujua huoni kwamba nipo sehemu maalum na mke wangu?"alihoji Dedani kibabe.Serambovu alinywea kwa tishio lile.Ni hatari sana Dedani kuwa karibu na Kilua.Hilo lilionesha ulinzi wa hali ya juu kwa familia ya Kilua.Ni sio siri Serambovu anamjua fika Dedani si mkurupukaji huonekana kama mtaratibu na asiyekurupuka lakini ni mtambo unaojua namna ya kupangilia na kama kweli Dedani amejua kutekwa kwake kuna mkono wa Serambovu bila shaka sasa hivi Serambovu angekuwa ameshamfutilia mbali au kuna mbinu kali sana ambayo Dedani atakuwa anataka kuitumia kumdhibiti.Alimuibia mke na sasa kamtia mimba mkewe nani anajua atafanya nini jingine?Nani anajua kisasi cha Dedani kwa Serambovu?
Serambovu hakutaka kabisa Kilua na Dedani wawe katika halli ileilionesha kuna uwezekano Kilua anairudisha ndoa yake.Lazima Kilua airudishe ilikutuliza maswali yaliyozuka kwamba rais hana mume na familia yake haijulikani ilipo?Anakumbuka sharti kubwa lilikuwa kuhakikisha siri ya kutekwa familia yake isivuje katika jamii na hocho Kilua alifanikiwa kukidhibiti akitumia wanausalama wachache kufanya operesheni ya kuirudisha familia yake lakini sadfa Shunie aliweza kumkomboa mumewe jambo ambalo lilionekana laajabu na halikutegemewa kabisa.
Dedani akamuachia mkewe nakumfuata Serambovu,"Unajua sijui ni kwanini upo hapa?Nasijui ni kwanini unaendelea kuifuata familia yangu?"
Serambovu alijikuta akishikwa na kigugumizi!Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo!
Kabla hajatafuta neno la kusema ilikuwa ghafla sana Dedani alimkunja shati Serambovu nakumvuta karibu na uso na kwa kasi ya ajabu Dedani alimpiga kichwa kitakatifu kama kondoo anavyomshambulia mwenzake!Pigo lilitua kwenye pua ya Serambovu nakumtikisa mfupa ulio puani kisawasawa!Hali iliyopelekea damu kumvuja puani kwa haraka.Dedani hakumuachia aliendelea kumkunja shati nakumshindilia tena vichwa kadhaa.Akamuachia mkono mmoja na kumshushia pigo lingine takatifu la ngumi kwenye mdomo!Kuu!Alimfumua kwa kishindo tena na tena na ngumi kadhaa za harakaharaka zilikuwa zimeshauharibu uso wa Serambovu pamoja na kuutotesha michirizi ya damu!Dedani alihakikisha anampiga kwa haraka kabla walinzi hawajaingilia kati jambo hilo.
KIlua aliogopa sana.Alijua Dedani alikuwa bado na hasira na alitegemea hilo.Alipanga nyuma kwamba angehakikisha wawili hao hawakutani lakini alifanya kosa kubwa sana kuwaruhusu walinzi wamuachie Serambovu aranderande ikulu bila kumdhibiti na hilo alilimeza na matokeo yake.Ni nini anafanya sasa!
Ilibidi aingilie kati kwa haraka ajaribu kuwaachanisha.
"Stop it you two!"alisema Kilua akimshika mumewe bega nakumvuta pembeni huku akipitisha mikono kiunoni mwa mumewe na kutokeza tumboni akamshika vizuri nakuulaza uso wake mgongoni mwake.
"Mme wangu nakuomba upunguze hasira!"alimhini mumewe.
Serambovu aliyumbayumba nakuanguka chini huku akiugulia maumivu.Mke wa mtu ni sumu maziwa ya Serambovu yalimtokea puani!HII ilikuwa ishara mbaya sana kufanyika ikulu na habari hii ilitakiwa isifike hata mlangoni.
"Huyu mbwa atokee hapa nitamuharibu!Nitakuua!"Dedani aliwaka!kilua hakujua kama mumewe alikuwa mbogo kwa namna hii.Alikuwa amekasirika sana bwana Dedani na pengine angefanya jambo baya kama hata dhibitiwa maapema kabisa.
"Dedani please control yourself!"alisema Kilua huku akijihisi hatia sana moyoni mwake.Dedani hakuonesha ishara ya maelewano kati yake na huyu afriti.
"Sielewi!Kafuata nini?"
"Unaona anavyonishambulia?Dedani nitakushtaki kwa kunishambulia nikiwa ikulu!"aliropoka Serambovu!
"Unaona bado unaoubinafsi hadi leo hujajifunza!"alisema Dedani akiwa na hasira sana!
"Hebu tulieni mtakabiliana hivi hadi lini?"Kilua alijaribu kutuliza kidogo.
"Hadi mmoja wetu akubali kukaa mbali na wewe!"aliropoka Dedani hasira ikimzidia nakujikuta akishindwa kujidhibiti
Kilua aliona wakati mgumu kuwadhibiti.Manukato ya ikulu yalikuwa mazuri sana.Hadhi ya jumba lile liliwafanya wote wajihisi ni kama hawakupaswa kuwa pale na ni kosa kubwa sana kufanya ugomvi ule pale.Lakini hasira zilimzidi bwana Dedani.
"Dedani unanionea bure."alijitetea Serambovu.
"Nyie wawili mmekuwa mkinila mgongo nyuma yangu!"alisema Dedani akizidi kughadhabika sana.
"Dedani tafadhali hebu come down kwanza."alijaribu KIlua.
"You brought your lover here then utegemee nimchekee?"aling'aka Dedani akipumua kwa hasira zisizo shuka.Kijacho chembamba kilipita usoni kuonesha mwili unachemka kwa hasira na sasa zimetota!
"Dedani chunga kauli zako!Mimi na Kilua tuna historia hata kabla wewe hujaja kwenye maisha yake sisi tulikuwa na dunia yetu!"alisema Serambovu akiamua kulipua bomu!Mambo yalikuwa yameiva sasa na Serambovu alipeleka mtanange kule alipotakiwa kuukwepesha.
"Unasemaje wewe hayawani?"alihoji Dedani akikosa stahamala ya uvumilivu nakuona kama nafsi yake inasalitika kwa mashtaka ya hawa wawili.
"Ndiyo kwani uongo!Mimi na Kilua tunapendana wewe ndo tatizo!"
Kilua alilaani hatua hiyo ya Serambovu ilikuwa yenye makali sana!
"Serambovu unavuka mipaka!"aling'aka binti Kilua mwana wa nyumba kubwa! Aliona ndoa yake inaeelekea kubaya sana shutuma za Serambovu na kama hawatamdhibiti siajabu akawaumbua.
"Mipaka gani wakati ndo ukweli?"ilikuwa kauli nzito sana
"Serambovu behave yourself!"alifoka Kilua akimwangalia kwa macho yaliyoomba ustaarabu!
"Ohh what?Utaniweka kizuizini tena?"alihoji Serambovu kwa kiburi.Akili yake ilibadilika kwa ghafla na kile kitendo cha Dedani kumpiga kilikuwa kichocheo na njia pekee ni kumshutumu Kilua hadharani mbele ya mumewe!
Kilua akaona huyu atampanda kichwani na amani aliyoweza kuijenga kwa muda mfupi ilikuwa inapukutia sasa!Serambovu anazidi kumtia matatizoni.Ni wazi SeraMBOVU anaenda kumharibia sana mwana mama huyu kuliko siku zote zile na bila kudhibitiwa atalipua bomu.
Kilua akamuachia Dedani aliwatizama wote wawili macho yalionesha hatia sana kwa kitendo alichokifanya.
"Kilua!"aliita Dedani!Lakini mabishano yale yaliwafanya walinzi wasikie nakuingia kwa kasi ya ajabu pale ndani.
Kilua akawapa ishara inatakiwa Dedani na Serambovu wawekwe vyumba tofauti muda uleule.Jambo lile likafanyika kwa haraka.Kilua akamfuata Dedani.Alimkabili japo wasiwasi ulikuwa mkubwa sana!
"Dedani wewe ni wangu peke yangu sipo tayari kukupoteza kwa lolote.Nitafanya lolote uwe ubavuni mwangu.You are my husband."alisema Kilua akimwambia Dedani aliyekuwa amewekwa chumba kingine akiwa amesimama karibu na dirisha huku mwanga wa jua ukipenya nammulika.Pazia lilichezacheza kwa ujio wa upepo mwanana uliopambwa na manddhari ya ikulu.Dedani alikuwa amechukizwa sana na kitendo cha Serambovu kuwa karibu na mkewe kiasi kile.Anakumbuka habari alizopewa na zee Kavu.
Kilua alimsogelea Dedani nakumbusu shavuni kwa lazima.
Dedani alimgeukia mkewe,"Kama unataka kuiokoa ndoa hii basi mfutilie mbali Serambovu.Ikiwezekana auawe!"alisema Dedani akimaanisha!Hilo la kuuawa lilimtisha sana Kilua.Amuue mwanaume aliyempenda sana wakati fulani?Amuue baba wa...hapana?Ataanzaje kwanza kumuua.Iistoshe ilionekana fika Serambovu anamnyororo wa yeye Kilua kumpata binti yake pamoja na kuwadaka watu walio na mtandao wa nyaraka za jalada za 13;14.Kwa vingine inatakiwa Serambovu awe karibu ili Kilua aweze kumdhibiti akiwa mbali atafanya mabaya zaidi ya yale ya mwanzo lakini akiwa karibu Serambovu na genge lake watakuwa bize kutaka kumdhibiti bi Kilua kwa kumsoma hatua anazochukua kuongoza nchi na mwenendo wa faili nambari 13;14.Hapo watakuwa na kasi ya polepole kupanga vikwazo kuliko Serambovu akiwa mbali.Ulikuwa wakati mgumu sana kwa Kilua!
"Tutajadili jambo hili.Ondoa hofu."ilibidi amtulize Dedani ingawa moyoni ilikuwa vigumu sana.Aliondoka mule ndani nakumfuata Serambovu aliyekuwa amewekwa kwenye chumba kingine.Kilua alionekana kuelemewa sasa huku mumewe anataka jambo gumu sana ingawa alikuwa tayari kwa lolote ila hilo.
Serambovu alipomuona Kilua alipamba moto.Aliinuka alipokuwa ameketi,"Kilua naomba umkanye mumeo!Unaona alichonifanya?Hajui nafasi yangu kwako?"
"Serambovu control yourself.Yule ni mume wangu sio takataka!"Kilua akawa mkali.
"Tangu lini Dedani akawa muhimu?Mimi nina nafasi kubwa kwako.Mimi ni chifu wako wa staffu najua mengi ya utawala wako."
"Narudia tena jishushe!"
"No!No!No!...Mimi ni mwanaume wa maisha yako unanipenda kuliko huyo fala.Tena nakutahadharisha mheshimiwa usipomdhibiti mumeo nitasema ukweli kwamba una mimba yangu!Isitoshe Shani ni mwanangu ile ni damu yangu ni Serambovu blood!"
Lilikuwa tishio kubwa sana kuwahi kulipata!
"Sitaki kumuona Dedani hapa ikulu!"alisema Serambovu kwa sauti kavu kisha akaendelea,"Ninauwezo wa kuichafua image yako vibaya sana.Kilua mimi nakupenda wewe nipo tayari kwa lolote hata kama nikuua kwaajili nitaua.Nataka kitu kimoja tu.Sihitaji uwepo wa Dedani hapa ikulu mrudishe jimbo la Kibatari kwa sasa."