Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 104
Baada ya kutoa kichapo cha goli 1-0 kwa Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika, Simba SC hii leo inashuka tena katika dimba la Mkapa kukipiga na African Lyon.
Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho la Azam Simba itakuwa ugenini na utapigwa majira ya saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kocha wa Simba Mfaransa, Da Rosa amethibitisha kuwa atapumzisha idadi kubwa ya wachezaji ambao walifanya jukumu dhidi ya mabingwa wa Afrika na kuwapa nafasi wachezaji wengine kwenye kikosi kuonesha walichonacho.
"Tutatoa nafasi kwa wachezaji wengine kwenye kikosi kuonesha mashabiki wao pia wako katika hali nzuri na wanaweza kufanya kazi kama kikosi kingine," Alisema Da Rosa
"Tunataka kutoa mapumziko kwa wanaoanza mara kwa mara, wamefanya kazi nzuri na lazima pia wapate likizo ya siku ili kupata utulivu, wanahitaji kupumzika ." Aliongeza Da Rosa
Simba ni mabingwa watetezi wa kombe hilo na wanatarajia kushinda tena msimu huu kwahiyo wamehimiza kikosi kutodharau African Lyon kwani wao pia wanataka kwenda mbali kwenye mashindano hayo.
Michezo mingine itakayopigwa hii leo ni kati ya Mwadui fc dhidi ya Gwambina saa 10 jioni, Mtibwa Sugar dhidi ya Jkt Tanzania saa 10 jioni, Rhino Ranger dhidi ya Tunduru Korosho na KMC dhidi ya Kurugenzi Fc.