Koffi Olomide ashitakiwa kwa kupigana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Koffi Olomide ashitakiwa kwa kupigana

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pasco_jr_ngumi, Aug 17, 2012.

 1. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,802
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Koffi Olomide, ambaye ni mwanamuziki mashuhuri
  barani Afrika ameshitakiwa kwa kumpiga
  Mtayarishaji wake wa muziki. Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika
  kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani
  jumatano. Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja
  mjini Kinshasa. Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya
  Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja
  kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin
  akiwa kizimbani. Kesi hiyo iliharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati
  atakaposhitakiwa rasmi. Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide
  aliwakilishwa na mawakili 10. Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi
  wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola
  $3,680. Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa
  atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi
  sita. Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous",
  mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer", lenye
  maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji
  wake vile vile wanatambulika kwa kunengua
  maungo.

  Source. bbc swahili
   
 2. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Tayari katiwa hatia na kapatiwa kifungo cha miezi mitatu iwapo atafanyakosa jingine tena wakati huu.
   
 3. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,802
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Loo, simpendi huyu....,
  Mambo yote ni Werasson
   
 4. C

  Chipolopolo JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 876
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii si habari njema hata kidogo.Kiio cha jamii kinapochafuka...watazamaji wataonaje sura zao katika kioo hicho??Ninasikitika.
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,019
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 180
  Ndo maana aliwahi kucharazwa bakora hadharani miaka ya 90.
   
 6. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,687
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mambo yote jb mpiana,dance kinkole!
   
 7. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  achana kabisa na koffi ni noumer, hao wote wanafuata nyuma, mengine hayo ni upepo tu unapita
   
 8. c

  chiborie JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  We JB hamna kitu hapo! Wera bana! uliicheki techno malewa?
   
 9. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 3,485
  Likes Received: 959
  Trophy Points: 280
  ngoja akapakatwe kidogo na masela wa kinshasha jela ili akitoka ajirekebishe na aheshimu utu wa wengine
   
 10. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  binafsi nam-feel ile kinoma huyu jamaa. kwanza bonge la TOOZI, show yake pale Mwanza Yatch Club 2006 nili-enjoy vya kutosha. POLE SANA PAPA MOPAO MOKONZI. MAKILA MABE, BOLINGO NANGAI, ha ha haaa!!!!
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,676
  Likes Received: 2,754
  Trophy Points: 280
  Nampenda sana huyu msomi msanii. yatapita tu papaa pole sana.
   
 12. varavara

  varavara Senior Member

  #12
  Aug 18, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  wewewe!koffi ni noma wanakuja wanapita lakini huyu jamaa kasimama huyu jamaa ni mkare!
   
 13. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,176
  Likes Received: 873
  Trophy Points: 280
  Waswahili bana,badala ya kujadili kesi wameanzisha malumbano ya nani zaidi,mnapotosha mada kama wabunge wa CCM
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 38,463
  Likes Received: 3,350
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo jamaa hivi sasa yupo jela?
   
 15. Master jay

  Master jay Senior Member

  #15
  Aug 18, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  bila simba hakuna yanga. Uwepo wa timu hizo huongeza ushindan ambao huwafanya waongeze bidii. Uwepo wa olomide na werra huwafanya kila mmoja ajitahid kufanya vizur il ampite mwenzie, matokeo yake wewe shabiki wake unata kitu supa.
   
 16. GP

  GP JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,076
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mopao Mokonzi ni MKOROFI SANA, hili sio tukio la kwanza kupiga wadau wa muziki wa kundi lake. walishwai kuzichapa na Felix Wazekwa akimtuhumu kumuiga staili ya uimbaji
   
 17. GP

  GP JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,076
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  feux de l'amour, hii ngoma ilikua MEGA HIT, haijawai kupata kutokea rhumba kali congo DRC kama hii iliyoporomoshwa na JB Mpiana. inshort Mopao hatii mguu kwa Jean Bedel Mpiana haswa kwa muziki wa rhumba.
   
Loading...