Mtangazaji Dakota wa Clouds fm punguza Mahaba yako kwa Koffi Olomide kwani unatukwaza mno Wasikilizaji wako tuliotukuka

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,037
Una sifa zote za kuwa mtangazaji na nakukubali sana ila umezidi Kumpenda mno Koffi Olomide. Sikutalii kwamba Koffi yupo vizuri ila sidhani kama kweli amefikia uwezo wa Kuwazidi Wapinzani wake akina JB Mpiana wa Wenge Musica BCBG na Ngiama Makanda Werrason wa Wenge Musica MM.

Yaani kila Ijumaa / Jumamosi ukiingia katika Kipindi chako ni lazima upige Nyimbo kama 10 hivi za Koffi Olomide lakini unaweza usipige hata Wimbo mmoja wa JB Mpiana Mwanamuziki mwenye Kipaji, Uwezo na Mvuto mkubwa Congo DR nzima kuliko hata huyo Koffi wako.

au kama unampenda mno Koffi Olomide basi badilisha Jina la Kipindi chako na kuanzia sasa uwe unakiita ' Koffi Time ' kuliko kinavyoitwa ' Buzuki Time ' au vinginevyo Kinavyoitwa kwani nisikufiche huwa unatukwaza sana na kuna wengine kwa jinsi tulivyo na Jazba zetu za karibu huenda hata tungekuwa tunaonana nawe ana kwa ana tungeishia kukupa tu ' Nakozi ' za maana.

Sasa leo nakupa Siri ukitaka Kipindi chako kiwe na Mvuto na Wasikilizaji waongezeke kuanzia sasa uwe unapiga Nyimbo 5 tu za Koffi Olomide, 20 za JB Mpiana, 10 za Werrason, 2 za Ferre Gola, 4 za Fally Ipupa na 3 za Felix Wazekwa. Fanya kama vile anavyofanya Kocha wa sasa wa Taifa Stars Ndayiragije ambapo akiita Wachezaji wa Stars basi ni lazima tu wa Simba SC watakuwa wengi, Azam kidogo na wa Yanga SC wanakuwa Kiduchu kabisa au anawaita basi tu kutoa Lawama kwani hawajui Mpira.

Nitashukuru ukibadilika Mtangazaji Bora wa Miziki ya Kikongo ( Dansi ) nchini Tanzania Papa Dakota.
 
Hua ananishangaza halafu kusifu eti koffi anaimba bado rhumba ni dhambi kubwa kwa mashabiki wa muziki wa rhumba afadhali hata marehemu zuberi msabaha alikua hana msanii wake na alikua anapiga nyimbo kulingana na generation zake
 
Jb Mpiana bila ile wenge BCBG hakuna lolote ni makelele tu.Mimi binafsi naiheshimu sana ile combination lakini siyo walipogawanyika.
Kuna akina Madilu,Bozi Boziana,Tshala Muana,na wengineo wengi.

Hata hivyo hakuna mtu aliyeweza kuziba pengo la Zuberi Msabaha kwenye anga hizo.Yule jamaa alizijua hasaa.
 
Back
Top Bottom