Historia ya KOFFI OLOMIDE ambayo wengi hatuijui

papag

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
1,137
1,608
01) Kwa Jina halisi hufahamika kama "AGBEPA MUMBA Antoine, Christophe.

Yeye ni Mwimbaji,Mpiga Gita,Mtunzi wa Nyimbo, Mpangaji, Mtayarishaji, Mzalisaji, Promota wa Muziki, Mmiliki wa Lebo "KOFFICENTRAL"
Kiongozi pia Mwanzilishi wa Group "QUARTIER LATIN INTERNATIONAL".

Antoine Christophe MUMBA AGBEPA kazaliwa Mjini "Kisangani" tarehe 11 August 1956.
Jina "KOFFI" kapewa kwakua kazaliwa Siku ya Ijumaa, kutokana na mila za upande wa Mama yake.
Babu mzaa Mama yake KOFFI OLOMIDE katokea Inchi ya SIERRA LEONE.
Kwa mila za huko Mtoto anapo zaliwa siku ya Ijumaa hupewa jina "KOFFI".

02) Wazazi wake "KOFFI OLOMIDE"

Kwa hapa yahitajika somo na ufafanuzi zaidi, maana baadhi ya Watu hua wakipotosha Umma kwa yale yasiokua na ushahidi hasa kuhusu Ukoo wake.

Baba yake Mzazi Mzee Charles AGBEPA ni Mkongomani Asilia, mwenyeji wa Mkoa wa "ÉQUATEUR" kwenye Kijiji cha "AKULA".
Mzee Charles AGBEPA alikua mchezaji mzuri wa mpira kandanda.
Maarufu sana kwenye miaka ya 1950 pale alipokua akijumuika na timu ya AS VITA CLUB Jijini KINSHASA.
Mzee Charles AGBEPA,Baba Mzazi wa KOFFI OLOMIDE,
Kafariki Jijini PARIS Mwaka 2016, tarehe 30 April.

Wakati Mama yake Mzazi Mama MOYAMI Amie (MAMAN AMY) ambae bado yuu hai, yeye ni mchanganyiko, Baba yake katokea SIERRA LEONE, katika Ukoo wa Watu ambao hufahamika kama (Coastmen).

Hawa ni kati ya Watu wakwanza kabisa waliotokea Africa magharibi nakuja kuweka kambi yao Inchini Congo kabla ya hata ya Uhuru.

Bibi yake "KOFFI OLOMIDE" Mzaa Mama ni Mkongomani asilia,kabila la Wasonge Mkoa wa "Kasai Oriental".

03) Kijana KOFFI OLOMIDE, kalelewa Jijini KINSHASA, kwenye Manispaa ya (LEMBA).Ndiko kasomea shule ya msingi.

Mwanafunzi huyo mwenye elimu sana tena wa kujituma, KOFFI OLOMIDE katokea kua pia mchezaji mzuri wa Kandanda kaufwata mkondo wa Baba yake.
Jamaa zake wakampachika Jina la (SEKELE) ikimaanisha ANASIRI YAKE YAUPEKEE KWENYE USAKATAJI KANDANDA.

Mtu wakwanza alie gundua Kipaji chake katika fani ya Muziki ni Mjomba wake "RESSE OLOMIDE",
Na ndie wakwanza pia kamfunza utumiaji wa Gita.

Ingawa Kapata upinzani mkubwa kutoka kwa Baba yake Mzee Charles AGBEPA, ambae hakua akipendelea katu Mwanae afanye kazi ya Muziki.

Hata hivyo, Mjomba RESSE OLOMIDE hajaishia hapo, kampeleka Mpwa wake kwa Jamaa yake "VERON" huyu ndie kamsaidia KOFFI OLOMIDE kulimudu vizuri Gita.

Na baadae maisha kama yalivyo, Mzee "VERON" kajakua Mwanamuziki wa KOFFI OLOMIDE ndani ya Group QUARTIER LATIN INTERNATIONAL kama mpiga Gita.

04) Mwaka 1970, "KOFFI OLOMIDE" kajiunga na Group la mtaani "SELE-SELE" kwenye Manispaa ya LEMBA, likiongozwa na Mwimbaji "TAKO-LEY". akiwa kama mpiga rhythmic Gita.
Huku akiendelea na shule, "INSTITUT SAINT JEAN" Manispaa ya LINGWALA.

KOFFI OLOMIDE kwenda kwake shule ilikua hasa kukidhi matakwa ya Baba yake ambae hajapendelea kumuona akifanya Muziki. Muziki ni kazi ya Wahuni. huo ulikua msimamo wa Mzee Charles AGBEPA.

KOFFI OLOMIDE aliendelea na kazi yake ya Muziki huku akizidi pia kujihimiza shuleni.

Pindi tuu kamaliza Sekondari, Baba yake kamtuma Chuo Kikuu Inchini FRANCE ambako kahitimu vizuri na kutunikiwa (DIGRII YA SAYANSI YA BIASHARA) CHUO KIKUU CHA BORDEAUX Inchini France.

05) Kama inavyo onyeshwa huko juu, KOFFI OLOMIDE, kaupenda muziki tokea akiwa bado Mdogo.
Umaarufu wake ukaanza kujitokeza sio kama Mwanamuziki kamili, bali kama Mtunzi wa nyimbo.
Wimbo "MERE SUPÉRIEURE" ulioimbwa na "PAPA WEMBA" mwaka 1977, umetungwa na KOFFI OLOMIDE na kumletea sifa nyingi sana.
Kipindi kile bado yupo chuoni UFARANSA.

Tungo hilo likapelekea apachikwe jina la (L'ÉTUDIANT LE PLUS CÉLÈBRE DU ZAÏRE / MWANAFUNZI ALIE MAARUFU KUWAZIDI WENGINE WOTE INCHINI ZAÏRE).

Alie muunganisha "KOFFI OLOMIDE" kwa kipenzi chake "PAPA WEMBA" ni Jhonniko AGBEPA, yeye ambae ni Kaka yake mkubwa wa kwanza tokea tumboni mwa Mamaye.

"JHONNIKO AGBEPA" na "PAPA WEMBA" walikua Marafiki wa nguvu sana.

Basi ikawa Upande mmoja "KOFFI OLOMIDE" anamtungia "PAPA WEMBA" nyimbo nae "PAPA WEMBA" kamuonyesha jinsi ya kuimba.
maana sio siri, KOFFI OLOMIDE alikua hajui kabisa kuimba.
Alichokua akifanya nikuiga uimbaji wa "TABU LEY" ama wa "MAXI MONGALI".

06) MWANZO WA KOFFI OLOMIDE KUIMBA.

"PAPA WEMBA" kasikika akisema kwamba, KOFFI OLOMIDE ni kijana wangu,
Ilifikia hatua wakati nikiwa kwenye dhiara ya Muziki, mimi na KOFFI OLOMIDE tunalala hotel moja kitanda kimoja. jambo ambalo sijawahi kumruhusu Mwanamuziki wangu yeyote.

KOFFI OLOMIDE alikua akinitungia nyimbo, na mimi ndie Mtu wakwanza kumpandisha Stejini.
Mic yake yakwanza kaishika nimemgea mimi.

Nae "VERCKYS KIAMUANGANA" kasema :
(Siku moja KOFFI OLOMIDE kaja VEVE Studio ambayo ni miliki yangu.

Walikua na mpango yeye na PAPA WEMBA wakurekodi wimbo.
Sasa baada ya masaa kupita wala PAPA WEMBA hajatokea.

Kuona hivyo, nikamshawishi "KOFFI OLOMIDE" achukue Mic na aanze kurekodi wimbo wake. huku tukiendelea kumsubiria PAPA WEMBA.
Nae bila kusita akaanza kuimba.

Baada ya KOFFI OLOMIDE kuimba, nikafanyia marekebisho kidogo ya Studio, wimbo wake ukawa tayar, nikamsikilizisha akawa mwenye furaha sana na kaguswa kweli.
Kumbe anaweza kuimba peke yake.
Ndivyo KOFFI OLOMIDE katokea kuwa Mwimbaji kwa namna moja ama nyingine.

07) Basi KOFFI OLOMIDE, keshakuwa mzoefu wa Studio, Alivyorudi tuu likizo KINSHASA, kaingia Studio akishirikiana na "PAPA WEMBA" wakarekodi nyimbo (Anibo, samba samba, Asso, Ekoti Ya Nzuba, Elengi Ya Mbonda, Marianne...).

Mwaka 1977, KOFFI OLOMIDE, kapata msaada wa Wanamuziki "ROXY TSHIMPAKA", "LIKINGA REDO" na "JEAN PIERRE NIMY" ambae alikua mpiga solo Gita mahiri sana wa Orchestra "YEYE NATIONAL".
Wakarekodi nyimbo (MENY na SORAYA).

Mwaka 1978, KOFFI OLOMIDE kapata ushirikiano wa DJUNA DJANANA wakarekodi wimbo (NDJOLI)
Kashirikiana kwa mara nyingine tena na "PAPA WEMBA" ukatolewa wimbo (CHÉRIE LIPASSA)

Mwaka 1979, KOFFI OLOMIDE kaingia Studio kurekodi wimbo (L'OISEAU RARE).
Ushirikiano wake na PAPA WEMBA.

08) Mwaka 1980, KOFFI OLOMIDE ndo kaanza kuwika vilivyo.
Ushirikiano kati yake na PAPA WEMBA pamoja na "KING KESTER EMENEYA" kwenye wimbo (SENZA) ukapelekea aanze kukubalika.

Mwaka 1982, kashirikiana na Group "LANGA LANGA STARS"
Zikatolewa nyimbo (ÉTOILE DU NORD na LONGOMO)
Nyimbo hizo kaziimba kwa pamoja na DINDO YOGO.

Mwaka ule 1980, KOFFI OLOMIDE, kashirikiana na Mwanamuziki DEBABA MBAKI DEBS, wakaanzisha Orchestra (HISTORIA MUSICA).

KOFFI OLOMIDE, mpenzi wa Mwanamke alivyokua, asilimia 90 ya tungo zake, hua akimchambua Mwanamke.

MWANAMKE HATA YUPO MWENYE HASIRA BADO YUU MWENYE NURU YAKE NA MWENYE KUNAWIRI.

SIWEZI NIKAHAMIA KUISHI MWEZINI HADI PALE NTAKAPO SIKIA KUNA WANAWAKE TAYAR HUKO. Interview ya KOFFI OLOMIDE Mwaka 1999 na gazeti la Black Match international.

09) Mwaka 1983, KOFFI OLOMIDE ndo kesha amua Muziki ndo utakua kazi yake rasmi.
Kapata ushirikiano wa JOSKY KIAMBUKUTA na RIGO STAR, chini ya usimamizi wa Producer JULES LUSANGI FATAKI maarufu kama TSHIKA TSHIKA, akatoa Album (NGOUNDA) ilio rekodiwa Jijini BRUSSELS.
ALBUM (NGOUNDA) INANYIMBO 10.


Ngobila,
Stéphie,
Motsio,
Ngounda,
Farousci,
Eminé,
Tokosamba Na Nzambe, Ngulupa,
Kifyoto,
Mamie La Fée…

10. Hawa ndo Marafiki na Watu wa mwanzoni kabisa kumpa sapoti KOFFI OLOMIDE :

TSHIKA TSHIKA
SERGE KAMITATU
GODARD MOTEMONA
GABIN YA TEMBO
BOUBOUL IYONDELA.
GUNTHER SUKAMBUNDU
JPK KITENGE
MOSKITO
IBUMA
PATRICK DIAMONA
BOB BOPESO

Itaendelea...
 
Nachojua mimi Koffi Olomide ana masters degree ya mathematics kutoka Paris university.

Ni wakati muafaka sasa Koffi akistaafu muziki arudi kufundisha hesabu chuo kikuu. Tunaweza kumuajiri hata hapa Bongo akafundisha udsm hesabu.
 
Nadhani ulitakiwa kuonyesha kuwa umekopy lubonji wa lubonji. Huyo ndio mwandishi mahili wa dansi ila hapendi kuibiwa material na mtu bila idhini yake. Nakutahadharisha ndugu
 
Sijaiba. Mimi huwa nikikuta kitu vizuri sehemu ambacho ni elimu ya bure kwetu.naeneza kwa wale ambao hawajaipata.ukikasirika basi usiiandike kaa nayo kichwani kwako.siitaji complement zaidi ya kupass information tu.
Nadhani ulitakiwa kuonyesha kuwa umekopy lubonji wa lubonji. Huyo ndio mwandishi mahili wa dansi ila hapendi kuibiwa material na mtu bila idhini yake. Nakutahadharisha ndugu
 
Back
Top Bottom