Koffi Olomide amekuwa cheap, amefikia mwisho

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
15,862
35,190
Tunaomjua huyu mwamba kuanzia mwanzoni mwa muaka ya 90,hatuna budi kusema amefikia mwisho wa umaarufu.kipimo cha msanii aliyejuu ni kupitia diary yake,wasanii maarufu diary zao ziko full booked mwaka mzima au zaidi,sasa huyu mwamba kwa mwaka hui kazuru Tanzania mara nne kitu ambacho enzi zake isingewezekana,eti Kofi aletwe na mwanamziki wa kariba ya Nandi ale ugali samaki kwenye hotpot za plastic,au ale makande kwa shishi food, aje kuwatumbuiza kina Mama j pale kwa mkapa kwa kiingilio cha buku tano,huyo sio Olomide tunayemjua,mwamba ameshuka status
 
Duu kashuka status kwa kigezo kipi au labda ulitaka apige show venue gani ?

Huwezi niambia mtu aliyepiga show kwenye uwanja wa watu zaidi ya 50elfu ashuke status au labda sababu kafanya show ya YANGA.
Hata wewe ukimpigia simu ya dili fasta anakuja aliletwa na Nandy akaishia kula kambale na ugali kwenye hotpot za plastic
 
Unavyokuwa mtu mzima.. maringo huwa yanaisha automatically. Kutokana na experience na mafunzo uliyoyapata maishani. Kwa umri wa koffi ameshazika marafiki na ndugu zake wengi sana .

Mtu mzima anakuwa anajua siku zake za kuishi zimefikia ukingoni.. anaamua kujipa raha na kuwapa watu raha maana hana cha kupoteza..

Kwa mtu kama koffi ambaye ameshatafuta hela sana ujanani... ana kila kitu.. koffi wa sasa hivi hawazi kujenga nyumba wala kununua gari.. anachowaza ni yeye kujipa raha na kuwapa watu wanaompenda raha.. hata kama kwa hela ndogo yeye hana hasara.. maana kusafiri safiri napo ni kujipa raha ya kukutana na mashabiki wake na kuwapa raha...

Koffi anamwona nandy kama mmojawapo wa washabiki wake. Na kwa heshima nandy anayompa koffi kofi hata hajali vyombo vya plastiki wala nini.. hata bill gates alivyokuja tanga alikula wali maharage huku ana smile kwenye sahani ya ajabu. Ama tajiri akiwa na ndugu zake anakula chakula bila maringo hata kama juu ya majani ya mgomba
 
Duu kashuka status kwa kigezo kipi au labda ulitaka apige show venue gani ?

Huwezi niambia mtu aliyepiga show kwenye uwanja wa watu zaidi ya 50elfu ashuke status au labda sababu kafanya show ya YANGA.
Wale watu elfu 50 walikuja kwa ajili ya yake au kwa ajili ya Yanga?Hio Yanga day hata wangesema anakuja ku perform harmorapa pangejaa tu maana wanaifata team na sio msanii.
 
Unavyokuwa mtu mzima.. maringo huwa yanaisha automatically. Kutokana na experience na mafunzo uliyoyapata maishani. Kwa umri wa koffi ameshazika marafiki na ndugu zake wengi sana .

Mtu mzima anakuwa anajua siku zake za kuishi zimefikia ukingoni.. anaamua kujipa raha na kuwapa watu raha maana hana cha kupoteza..

Kwa mtu kama koffi ambaye ameshatafuta hela sana ujanani... ana kila kitu.. koffi wa sasa hivi hawazi kujenga nyumba wala kununua gari.. anachowaza ni yeye kujipa raha na kuwapa watu wanaompenda raha.. hata kama kwa hela ndogo yeye hana hasara.. maana kusafiri safiri napo ni kujipa raha ya kukutana na mashabiki wake na kuwapa raha...

Koffi anamwona nandy kama mmojawapo wa washabiki wake. Na kwa heshima nandy anayompa koffi kofi hata hajali vyombo vya plastiki wala nini.. hata bill gates alivyokuja tanga alikula wali maharage huku ana smile kwenye sahani ya ajabu. Ama tajiri akiwa na ndugu zake anakula chakula bila maringo hata kama juu ya majani ya mgomba
Hizo tabia zina apply kwa wazungu sio ngozi nyeusi
 
Wale watu elfu 50 walikuja kwa ajili ya yake au kwa ajili ya Yanga?Hio Yanga day hata wangesema anakuja ku perform harmorapa pangejaa tu maana wanaifata team na sio msanii.
Sawa ila jiulize kwa nini Yanga walimwitaji Koffi au labda fainali ya kombe la dunia 2010 na 2014 walimfuata Shakira au mechi ya fainali?
 
Tunaomjua huyu mwamba kuanzia mwanzoni mwa muaka ya 90,hatuna budi kusema amefikia mwisho wa umaarufu.kipimo cha msanii aliyejuu ni kupitia diary yake,wasanii maarufu diary zao ziko full booked mwaka mzima au zaidi,sasa huyu mwamba kwa mwaka hui kazuru Tanzania mara nne kitu ambacho enzi zake isingewezekana,eti Kofi aletwe na mwanamziki wa kariba ya Nandi ale ugali samaki kwenye hotpot za plastic,au ale makande kwa shishi food, aje kuwatumbuiza kina Mama j pale kwa mkapa kwa kiingilio cha buku tano,huyo sio Olomide tunayemjua,mwamba ameshuka status
Huyo ni legendary,yupo kwenye miaka sabini sasa,hana Cha kupoteza mchango wake kwenye muziki wa Afrika nicmkubwa sana.
Tangu miaka ya 90,wakati huo Kanda bongo man,aurlus mabele,mbili bell,wenge,wengine wote wamepotea,yeye Bado yupo na moto ule ule,
Hata akiamua kupumzika sasa hv,vita amevipigana
 
Sawa ila jiulize kwa nini Yanga walimwitaji Koffi au labda fainali ya kombe la dunia 2010 na 2014 walimfuata Shakira au mechi ya fainali?
Kwa sababu alipatikana kirahisi ba alikuwa cheap kulinganisha na wengine
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom