Kodi ya SimCard sasa kuanza mara moja!

Kodi ya SimCard sasa kuanza mara moja!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,171
Reaction score
162,618
Mamlaka ya mapato nchini(TRA) imeandika waraka kwenda kwa makampuni ya simu nchini kuagiza kuanza utekelezaji wa kukata kodi ya laini ya simu.Kodi hiyo ni kuanzia July 30 mpaka september mwaka huu.Hii ina maana kwamba kila mtumiaji atakatwa sh 3000 ikiwa ni kodi ya mwezi July,August na September.Kwa maana hiyo mwenye laini mbili atakatwa sh 6000 na mwenye laini tatu atakatwa sh 9000.

Na katika hatua nyingine wateja milioni 8 simu zao kufungwa.

Kwa taarifa zaidi soma gazeti la Tanzania Daima

CHANZO:TANZANIA DAIMA ONLINE

MY TAKE:
Hii inaweza kuwa ni mbinu ya kuhamisha "attention" ya watu kutoka kwenye issue ya katiba na kutupeleka kwenye issue ya tozo za line za simu!

Tafakari na kisha chukua hatua!

WATUMIAJI wa simu wapatao milioni nane wapo hatarini kufungiwa simu zao ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, Tanzania Daima limebaini.

Tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeziandikia kampuni za simu waraka wa kuzitaka zianze kukata kodi mpya ya laini (simu card) mara moja kuanzia Julai 30, 2013.

Hatua hiyo inatokana na serikali kushindwa kufuta kodi hiyo ya sh 1,000 iliyopitishwa na Bunge kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete baada ya kukutana na wadau wa sekta ya mawasiliano.

Kwa maana hiyo kila anayemiliki laini moja ya simu atakatwa sh 3,000; anayemiliki laini mbili sh 6,000 na anayemiliki laini tatu sh 12,000, lengo ni kuhakikisha serikali inakusanya sh bilioni 178 zitakazopelekwa kwenye bajeti kuu ya serikali.

Watumiaji wa simu sasa watalazimika kulipia kodi hiyo ya miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba kwa wakati mmoja.
Bunge kupitia Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) lilitaka kuwapo kwa kodi hiyo ili kusaidia shughuli za bajeti ya Serikali Kuu.

Kupitishwa kwa kodi hiyo kuliibua malalamiko ya wanasiasa dhidi ya Chenge anayelazimisha kuwapo kwa kodi hiyo, huku akishindwa kuamini kwamba kuna Mtanzania anayekosa sh 1,000 kwa mwezi kwa ajili ya laini ya simu.

Malalamiko hayo yaliendelea hadi kwa wananchi na baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliotaka posho za wabunge zipunguzwe ili kuziba pengo hilo badala ya kuwabebesha wananchi mzigo.

Inadaiwa kwamba msimamo wa Chenge unaungwa mkono na Spika wa Bunge, Anne Makinda, jambo lililosababisha kutojadiliwa kwa hoja binafsi ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA) iliyohusu kodi hiyo katika mkutano wa Bunge lililopita kwa kisingizio cha kukosekana kwa muda wa kufanya hivyo.

Hata hivyo, takwimu zilizotolewa na kampuni za simu zinaonyesha kuwa miongoni mwa wamiliki wa laini za simu milioni 22; milioni nane wanatumia chini ya sh 1,000 kwa mwezi.

Baada ya malalamiko hayo, Rais Kikwete alikutana na wadau wa mawasiliano ambao ni wamiliki wa kampuni za simu Tanzania (MOAT), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kisha kuwaagiza waiondoe kodi hiyo.

"Rais alisema lengo kuu la mkutano huo liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la sh bilioni 178 zitakazopotea katika bajeti iwapo kodi hiyo itafutwa.

"Alisema hawezi kuifuta moja kwa moja kodi hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha kujazia pengo litakalotokeza huku tayari Bunge limezipangia matumizi," alinukuliwa Makamba baada ya kikao hicho na rais.

Kwa upande wake, rais alikaririwa akiwaambia wadau hao wa mawasiliano kwamba: "Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la sh bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito, na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu."

Licha ya agizo hilo la rais kutekelezwa kwa MOAT kutakiwa kuongeza kodi nyingine iitwayo ‘Excise duty' kutoka asilimia 14 hadi 17 bila kujali kwamba katika Bunge la bajeti kodi hiyo iliongezwa kutoka asilimia 12 hadi asilimia 14, tozo hiyo ya laini za simu haijaondolewa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa na mawasiliano walisema kutojadiliwa kwa mabadiliko ya kodi hiyo ya simu ni dalili kwamba Waziri wa Fedha amezidiwa nguvu na kiti cha spika kinachounga mkono hoja hiyo ya Chenge na kushindwa kutekeleza agizo la rais.
Wataalamu wa mawasiliano walilieleza gazeti hili kwamba kuongezeka kwa kodi hiyo kutaifanya Tanzania kuwa na kiwango cha juu cha kodi kuliko nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ushauri wa wataalamu hao ulibainisha kwamba kuongezeka kwa kodi hiyo kunaleta nafuu kidogo kuliko ile ya laini za simu inayomuumiza zaidi mwananchi wa kawaida.
attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • TRA 1..jpg
    TRA 1..jpg
    146.7 KB · Views: 1,395
  • TRA 2..jpg
    TRA 2..jpg
    164.6 KB · Views: 1,385
kwa line zaidi ya m20 ni wazi CCM watakuwa wakichukua 2bn kila siku..finally kila mwizi watakuwa na 60bn...za kutosha kabisa kuwaaambia watanzania hawana dhambi kwa vile uovu wa CCM 2015 utakuwa financed na watanzania wote wenye line za simu...
 
Mamlaka ya mapato nchini(TRA) imeandika waraka kwenda kwa makampuni ya simu nchini kuagiza kuanza utekelezaji wa kukata kodi ya laini ya simu.Kodi hiyo ni kuanzia July 30 mpaka september mwaka huu.Hii ina maana kwamba kila mtumiaji atakatwa sh 3000 ikiwa ni kodi ya mwezi July,August na September.Kwa maana hiyo mwenye laini mbili atakatwa sh 6000 na mwenye laini tatu atakatwa sh 9000.

Na katika hatua nyingine wateja milioni 8 simu zao kufungwa.

Kwa taarifa zaidi soma gazeti la Tanzania Daima

CHANZO:TANZANIA DAIMA ONLINE

MY TAKE:
Hii inaweza kuwa ni mbinu ya kuhamisha "attention" ya watu kutoka kwenye issue ya katiba na kutupeleka kwenye issue ya tozo za line za simu!

Tafakari na kisha chukua hatua!

Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.
 
Unajitolea kukatwa na wakati ushasema habari ni ya uongo kutoka jarida la udaku?Duh!

Unakataa na kukubali hapo hapo.:wink1::wink1:
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

Umezoea kukatwa eeeh?
 
CCM wamesha tuona sisi ni bendera fuata upepo.
Wanatuendesha kwa remote control a.k.a kitendambali
Mamlaka ya mapato nchini(TRA) imeandika waraka kwenda kwa makampuni ya simu nchini kuagiza kuanza utekelezaji wa kukata kodi ya laini ya simu.Kodi hiyo ni kuanzia July 30 mpaka september mwaka huu.Hii ina maana kwamba kila mtumiaji atakatwa sh 3000 ikiwa ni kodi ya mwezi July,August na September.Kwa maana hiyo mwenye laini mbili atakatwa sh 6000 na mwenye laini tatu atakatwa sh 9000.

Na katika hatua nyingine wateja milioni 8 simu zao kufungwa.

Kwa taarifa zaidi soma gazeti la Tanzania Daima

CHANZO:TANZANIA DAIMA ONLINE

MY TAKE:
Hii inaweza kuwa ni mbinu ya kuhamisha "attention" ya watu kutoka kwenye issue ya katiba na kutupeleka kwenye issue ya tozo za line za simu!

Tafakari na kisha chukua hatua!
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.
...sijawahi kuona mwanamke mnafki kama wewe...? ungekuwa karibu ningekunasa kibao..
 
unataka kukatwa, inaonekana unapenda sana kukatwa na huwa unasikia raha.
 
Mbona mnalipa kodi nyingine nyingi.

Badala ya kulalamikia PAYE ishuke mnalalamikia tozo la simu.

Hongera serikali kwa kutokukubali kuyumbishwa na wanasiasa.
 
...sijawahi kuona mwanamke mnafki kama wewe...? ungekuwa karibu ningekunasa kibao..

we binti unayetangatanga si wote wana hela kama wewe mfano vijijini hata mijini watu wanaishi kwa kubahatisha hivyo unavyotoa maoni usijiangalie wewe au maslai ya chama chako ukizani unakomesha hoja za wapizani
 
NGOJA TUTENGENEZE APPLICATION ZA FREE CALLING..... HATUWEKI VOCHA SISI NA PDproxy
 
Back
Top Bottom