Kodi ya Chumba.....

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Mfanyabiashara mmoja akiwa katika moja ya safari zake za kibiashara aliamua kwenda kwenye ukumbi wa burudani jioni baada ya siku ndefu ya pilika nyingi. Kulikuwa na bendi ya muziki wa dansi ikitumbuiza, na binti mmoja mrembo akiwa kwenye safu ya uimbaji ya bendi hiyo. Mfanyabiashara uvumilivu ukamshinda na akamtokea yule mrembo na wakakubaliana kulala wote usiku huo kwa malipo ya shilingi laki mbili.

Asubuhi lilpofika, mfanyabiashara akajikuta kapungukiwa fedha taslimu, kwa hiyo wakakubaliana na mrembo kuwa angemtumia fedha yake baadae kwa cheki (hundi) ofisini kwake yule binti ndani ya bahasha na juu ya bahasha angeandika "Kodi ya Chumba". Wakati wa kuandika ile hundi, mfanyabiashara akaona ugumu wa kulipa shilingi laki mbili kulipia huduma ambayo haikukidhi matarajio yake kulingana na muonekano wa binti, hivyo akaandika hundi ya shilingi laki moja tu na akaambatanisha barua iliyosema hivi:

Mpendwa bibie,

Nimekulipa laki moja badala ya mbili tulizokubaliana kwa sababu zifuatazo:

  1. Nilipokubaliana na bei nilitegemea chumba kingekuwa hakijawahi kutumiwa.
  2. Nilitegemea kiwe na joto la kutosha
  3. Nilitegemea chumba kingekuwa kidogo lakini badala yake kikawa kikubwa mno hadi kinakarahisha.

Baada ya muda mfanyabiashara akarudishiwa bahasha yenye hundi aliyomwandikia mrembo na barua yenye majibu haya:

Ndugu mpendwa,
Nakushangaa kutegemea chumba kizuri namna hii kiwe hakijawahi kutumiwa hata mara moja. Joto lilikuwepo, ila tu hukujua namna ya kuwasha. Je, ni kosa langu kwa wewe kutokuwa na fenicha za kutosha chumba nilichokupa?
 
Jamani ee, chumba ni chumba tu, kiwe kikubwa, kidogo, chembamba haijalishi. cha maana ni mtumiaji wa chumba anakipamba vipi kivutie? mapicha ya ukutani? udi? perfume? teh teh teh!!
 
Jamani ee, chumba ni chumba tu, kiwe kikubwa, kidogo, chembamba haijalishi. cha maana ni mtumiaji wa chumba anakipamba vipi kivutie? mapicha ya ukutani? udi? perfume? teh teh teh!!

Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom