Kocha yupi kati ya hawa alikuvutia zaidi katika EPL?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,718
45,125
Zama huja na kuondoka. Lakini legacy hubaki. Hapa kuna makocha wanne tofauti ambao kwa nyakati tofauti waliongoza vilabu vyao kutwaa mataji kadhaa ya EPL. Kila kocha alikuwa na rekodi zake pamoja na mbinu zake. Ni yupi unamkubali zaidi?

1. Sir Alex Ferguson - Man Utd
Huyu ametwaa mataji 13 ya EPL akiwa Man Utd. Aliifanya Man Utd itambe na kuogopwa sana EPL. Alitwaa mataji matatu mfululizo ya EPL mara mbili tofauti. Tangu kuondoka kwake Man Utd inalegalega.

2. Arsene Wenger - Arsenal
Wenyewe the gunners walipenda kumuita “Profesa” alileta mapinduzi makubwa ya namna ya uchezaji katika EPL. Nani asiyejua jinsi alivoitengeneza Arsenal na kuwa mwiba mkali Highbury usingeweza kutoka salama. Mpaka anasatafu alitwaa mataji mawili tu ya EPL

3. Jose Mourinho - Chelsea
Kipindi chake cha kwanza pale Chelsea mwaka 2004-2007 Jose alikuwa kocha mwenye rekodi lukuki.
Msimu wa 2005 aliweka rekodi ambayo mpaka leo haijavunjwa. Clean sheet 24 za EPL katika mechi 38 sio mchezo huku Chelsea ikiruhusu magoli 15 tu katika mechi 38. Chelsea ilikuwa haishikiki. Alitwaa mataji mawili mfululizo.

4. Pep Guardiola ( Man City )
Master Pep mpaka sasa ana mataji matano ya EPL. Kwasasa ndio ameishika EPL. Ameweka rekodi ya kufika point 100 kwa msimu katika EPL. Anacheza soka la kisasa mno. Huku akileta mbinu zake ambazo zamani hazikuwahi kuwa applicable na makocha wenzake.

Nani angeweza kuleta kipa ambaye anatakiwa kuwa na footwork nzuri kuliko kudaka, nani angeweza kumfanya full back aingie ndani kucheza kama kiungo, nani angeweza kuchukua taji la EPL bila ya kuwa na natural striker namba 9
Hayo yote Guardiola kayaweza kufanya na kafanikiwa.

Kocha yupi unamkubali zaidii?
A4426E07-0836-4D9E-9F8B-88A5723BAE15.jpeg
 
Binafsi namkubali sana tena sana hadi kesho "The special one" -Jose Mourinho.

Aliongeza radha Epl kipindi ambacho Sir Fergie na mwenzie Prof Wenger walikuwa untouchable.

Tena kubwa kuliko alifanya mapinduzi makubwa ya kuifanya Chelsea mbovu kuwa Beberu wa soko la Epl tofauti na Pep ambaye anaendeleza walipoishia wenzake.
 
Ni wakati uliopita au uliopo?

Mzee ferggy
ni mwalimu wa boli..Kaibua vipaji ambavyo mpaka leo bado vinakiwasha kina CR7,DDG n.k ni zao la Fergy

Wenger
nae si haba!!Enzi izo arsenal na Man U zilikua kama paka na panya..Wenger nae anavipaji vyake kina T.Henry na sasa kina Theo walcott bado wanakiwasha.

Baba josee
Wanamuita rinyo boy huyu ni kama maskini jeuri.Mpira anaujua na chokochoko anazijua..Hapendi mambo mengi mpira wake ni long balls na kadi nyingi sana..Ndie kocha anaeongoza kwa kadi sio yellow au Red.Vilevile team atayofundisha lazima iwe na watukutu...Kafua team nyingi sana huyu mchaga Spurs,Man U,Chelsea,Madrid,Roma

Pep mzee upara
Huyu ni technician..Mzee analijua boli anajua mbinu.kifupi ni scientist wa mbinu.Ndio alianzisha mambo ya Modern football..Anaamini kwenye mpira wa holding.Yani team ipige mipasi mingiii isimpe nafasi adui.Mfano ile barca ya Pep walikua wanapiga pasi kama 1000+

Badluck pep ni technician na wachezaji wake wamepita mlemlee..wakitoka kwenye mikono yake wanakua wazito sana

Enewei Naona Pep akichukua quadraple kama sio treble tena kwakua Community shield vs kibonde Aseno,UEFA super cup kibonde sevilla, bado hajaongeza FA,Carabao,UEFA,na EPL

Huyu mtu azuiwe..asipozuiwa pale EPL hakuna timu ya kubato na city hii ya pep.Klopp alianza kujipata ila kakata moto.Binafsi naona upara mwenzie ETH ndo atampa changamoto msimu ujao

Kenge nina mengi ya kueleza.nisiposhikiliwa naweza kuandika uzi juu ya Uzi wa mtoa mada.acha niishie hapa

Kwa ufupi wote wanajua kwenye prime yao sisi HATUWADAI
 
Tena kubwa kuliko alifanya mapinduzi makubwa ya kuifanya Chelsea mbovu kuwa Beberu wa soko la Epl tofauti na Pep ambaye anaendeleza walipoishia wenzake kutwaa mataji.

Man city kabla ya pep ilikuwa na mataji mangapi na after pep ina mataji mangapi ?
Binafsi namkubali sana tena sana hadi kesho "The special one" -Jose Mourinho.

Aliongeza radha Epl kipindi ambacho Sir Fergie na mwenzie Prof Wenger walikuwa untouchable.

Tena kubwa kuliko alifanya mapinduzi makubwa ya kuifanya Chelsea mbovu kuwa Beberu wa soko la Epl tofauti na Pep ambaye anaendeleza walipoishia wenzake.

Pep ameifanya EPL iwe farmers league.. kila msimu bingwa yeye tu
 
Pep amekuta Man city ina muda mchache chini ya miaka 2 toka ichukue ubingwa wa ligi(2014 chini ya Pellegrini City alikuwa bingwa).

Pia ameikuta timu iko top 4 ya Epl almost kwa misimu kadhaa mfululizo.

Njoo sasa kwa Morinho, huyu mwamba aliikuta Chelsea ni timu inayocheza isishuke daraja, pia timu ilikuwa na miaka 54 mara ya mwisho tangu ichukue ubingwa lakini msimu wake wa kwanza akamaliza nafasi ya 2 Epl, msimu uliofuata akawa bingwa wa Epl huku akiweka rekodi ya kufungwa goli 15 pekee na cleansheet 24.

Hakuishia hapo msimu uliofuata alibeba tena ndoo ya Epl mbele ya makocha vigogo Fergie, Rafa Benitez na Wenger.

Kwa mazingira hayo hiyo kazi anaiweza The special one pekee.

N.b

2002 Morinho alichukua Ueropa akiwa na kikosi cha kawaida cha Fc Porto

2003 Morinho alichukua Uefa akiwa na kikosi cha kawaida cha Fc Porto wakati Pep ameshindwa kupata ubingwa wowote wa Ulaya akiwa na timu bora ya Bayern Munich, pia amepambana muda mrefu kuchukua Uefa akiwa na City licha ya kuwa na kila kitu.

Morinho ndiye kocha PEKEE Ulaya ambaye amechukua vikombe vyote kwa ngazi ya klabu, kikombe cha mwisho amechukua mwaka jana akiwa na As Roma cha Uefa conference league.

Kwa hoja hizo HAKUNA kama Morinho.
Hao wengine iliwachukua muda mrefu kutoboa japo walikuwa na kila kitu.
 
1.Soma kichwa cha habari cha topic ya uzi kisha ndio urudi tubishane.

2. Jose mourinho anamzidi pep kwa taji gani ?
 
1. Kichwa kinasema kocha yupi unamkubali pale Epl kati ya aliowaorodhesha mtoa mada, binafsi nimesema namkubali Morinho

2. Mataji ambayo Jose amechukua ila Pep hajachukua ni Europa league na Europa conference. Ila kwenye mataji haya tusiyape kipaumbele kwa vile Pep hajayashiriki mashindano yake.
 
Binafsi namkubali sana tena sana hadi kesho "The special one" -Jose Mourinho.

Aliongeza radha Epl kipindi ambacho Sir Fergie na mwenzie Prof Wenger walikuwa untouchable.

Tena kubwa kuliko alifanya mapinduzi makubwa ya kuifanya Chelsea mbovu kuwa Beberu wa soko la Epl tofauti na Pep ambaye anaendeleza walipoishia wenzake.
Kuhusu Pep wengi watakupinga ila mambo yako hivyo ulivyosema.

1. Aliikuta Barca iloachwa na Frank Rjikard ikiwa na moto wa vijana wengi wazuri.

2. Alienda Bayern ikiwa bado ni mbabe wa Bundesliga na mpaka kesho bado watakuwa ni wababe wa bundesliga.

3. Kaenda Man City ikiwa bado ina tawala vizuri tu soka la EPL, hakutumia nguvu kubwa sana kuibadilisha Man City.

Yote ktk yote nakubali jamaa pia ni mwalimu mzuri, tena sana tu.
 
Ni wakati uliopita au uliopo?

Mzee ferggy
ni mwalimu wa boli..Kaibua vipaji ambavyo mpaka leo bado vinakiwasha kina CR7,DDG n.k ni zao la Fergy

Wenger
nae si haba!!Enzi izo arsenal na Man U zilikua kama paka na panya..Wenger nae anavipaji vyake kina T.Henry na sasa kina Theo walcott bado wanakiwasha.

Baba josee
Wanamuita rinyo boy huyu ni kama maskini jeuri.Mpira anaujua na chokochoko anazijua..Hapendi mambo mengi mpira wake ni long balls na kadi nyingi sana..Ndie kocha anaeongoza kwa kadi sio yellow au Red.Vilevile team atayofundisha lazima iwe na watukutu...Kafua team nyingi sana huyu mchaga Spurs,Man U,Chelsea,Madrid,Roma

Pep mzee upara
Huyu ni technician..Mzee analijua boli anajua mbinu.kifupi ni scientist wa mbinu.Ndio alianzisha mambo ya Modern football..Anaamini kwenye mpira wa holding.Yani team ipige mipasi mingiii isimpe nafasi adui.Mfano ile barca ya Pep walikua wanapiga pasi kama 1000+

Badluck pep ni technician na wachezaji wake wamepita mlemlee..wakitoka kwenye mikono yake wanakua wazito sana

Enewei Naona Pep akichukua quadraple kama sio treble tena kwakua Community shield vs kibonde Aseno,UEFA super cup kibonde sevilla, bado hajaongeza FA,Carabao,UEFA,na EPL

Huyu mtu azuiwe..asipozuiwa pale EPL hakuna timu ya kubato na city hii ya pep.Klopp alianza kujipata ila kakata moto.Binafsi naona upara mwenzie ETH ndo atampa changamoto msimu ujao

Kenge nina mengi ya kueleza.nisiposhikiliwa naweza kuandika uzi juu ya Uzi wa mtoa mada.acha niishie hapa

Kwa ufupi wote wanajua kwenye prime yao sisi HATUWADAI
Naongea kama shabiki nguli wa mda mrefu wa Barca, Barca ya peo haikuwa inapossess vizuri mpira kama ya Frank Rjidkard.

Achana na Barca ya Frank mzee. Guardiola aliondoka Barca akijua tayari utawala wa Barca umeshaanza kuanguka pale Spain.

Barca ile ya Guardiola, asingekuwa mbaguzi na mambo yake meusi, ile Barca ilikuwa ni ya kuchukua UEFA hata miaka 5 mfululizo.
 
Zama huja na kuondoka. Lakini legacy hubaki. Hapa kuna makocha wanne tofauti ambao kwa nyakati tofauti waliongoza vilabu vyao kutwaa mataji kadhaa ya EPL. Kila kocha alikuwa na rekodi zake pamoja na mbinu zake. Ni yupi unamkubali zaidi?

1. Sir Alex Ferguson - Man Utd
Huyu ametwaa mataji 13 ya EPL akiwa Man Utd. Aliifanya Man Utd itambe na kuogopwa sana EPL. Alitwaa mataji matatu mfululizo ya EPL mara mbili tofauti. Tangu kuondoka kwake Man Utd inalegalega.

2. Arsene Wenger - Arsenal
Wenyewe the gunners walipenda kumuita “Profesa” alileta mapinduzi makubwa ya namna ya uchezaji katika EPL. Nani asiyejua jinsi alivoitengeneza Arsenal na kuwa mwiba mkali Highbury usingeweza kutoka salama. Mpaka anasatafu alitwaa mataji mawili tu ya EPL

3. Jose Mourinho - Chelsea
Kipindi chake cha kwanza pale Chelsea mwaka 2004-2007 Jose alikuwa kocha mwenye rekodi lukuki.
Msimu wa 2005 aliweka rekodi ambayo mpaka leo haijavunjwa. Clean sheet 24 za EPL katika mechi 38 sio mchezo huku Chelsea ikiruhusu magoli 15 tu katika mechi 38. Chelsea ilikuwa haishikiki. Alitwaa mataji mawili mfululizo.

4. Pep Guardiola ( Man City )
Master Pep mpaka sasa ana mataji matano ya EPL. Kwasasa ndio ameishika EPL. Ameweka rekodi ya kufika point 100 kwa msimu katika EPL. Anacheza soka la kisasa mno. Huku akileta mbinu zake ambazo zamani hazikuwahi kuwa applicable na makocha wenzake.

Nani angeweza kuleta kipa ambaye anatakiwa kuwa na footwork nzuri kuliko kudaka, nani angeweza kumfanya full back aingie ndani kucheza kama kiungo, nani angeweza kuchukua taji la EPL bila ya kuwa na natural striker namba 9
Hayo yote Guardiola kayaweza kufanya na kafanikiwa.

Kocha yupi unamkubali zaidii?
View attachment 2701560
Naichukia nyumbu,siipendi asheno...ila kiukweli HAWA makocha Fergie na Wenger walikuwa ni makocha haswaaa...hawa wengine ni wahuni TU,walitembelea na wanatembelea nyota za wamiliki za kuwa na pesa za usajili...

YNWA
 
Kuhusu Pep wengi watakupinga ila mambo yako hivyo ulivyosema.

1. Aliikuta Barca iloachwa na Frank Rjikard ikiwa na moto wa vijana wengi wazuri.

2. Alienda Bayern ikiwa bado ni mbabe wa Bundesliga na mpaka kesho bado watakuwa ni wababe wa bundesliga.

3. Kaenda Man City ikiwa bado ina tawala vizuri tu soka la EPL, hakutumia nguvu kubwa sana kuibadilisha Man City.

Yote ktk yote nakubali jamaa pia ni mwalimu mzuri, tena sana tu.
Pep sio mwalimu,wapenzi wa soka plz tofautisheni mwalimu na Technician..Mchezaji gani alietoka kwenye mikono ya pep akaenda na moto uleule? Achana na messi aliemkuta akiwa na moto wake

Hawa kina f.torres,zincheko,Sterling,G.jesus,cancelo
 
Back
Top Bottom