Kocha wa ivory coast;naitamani taifa stars


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,873
Likes
8,693
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,873 8,693 280
Kocha Ivory Coast: Nipeni Taifa Stars

Kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coast Vahid Halilhodzic ambaye ametangaza nia yake ya kutaka kubeba mikoba ya Marcio Maximo ambaye anatarajia kumaliza mkataba wake wa kuinoa timu ya Taifa stars hivi karibuni.

Vicky Kimaro

KOCHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast, 'The Elephants' Vahid Halilhodzic amesema yupo tayari kubeba mikoba ya Marcio Maximo iwapo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), litamuhitaji.


Kocha huyo aliiongoza nchi hiyo kucheza fainali za Afrika zinazoanza kesho nchini Angola na Kombe la Dunia baadaye Juni. Timu hiyo iliyoweka kambi nchini, iliondoka jana kwenda Angola.


Akizungumza na waandishi wa habari juzi mara baada ya mechi yao na Rwanda ambayo Ivory Coast walitoka kifua mbele kwa mabao 2-0, Halilhodzic alisema mkataba wake na Ivory Coast unamalizika mara baada ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Afrika Kusini.


"Mkataba wangu unamalizika baada ya Kombe la Dunia, nimeshapata maombi mengi sana, Tanzania kama nao wataomba naweza kuwafikiria nikaja kufundisha.


"Nimeiona ni nchi nzuri yenye amani,"alisema Holilhodzic raia wa Bosnia alipoulizwa swali iwapo atakuwa tayari kuja kurithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa Juni.


Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kwa kushirikiana na serikali wameanza mchakato wa kumsaka kocha atakayerithi mikoba ya Mbrazil huyo.


Akizungumzia kiwango cha wachezaji wa Tanzania Holilhodzic ambaye ameshahaidi kurudi nchini kulipeleka Kombe la Mataifa ya Afrika kileleni mlima Kilimanjaro iwapo watalitwaa, alisema: "Tanzania ina uwanja mzuri lakini haina wachezaji wazuri, kama mnataka mafanikio ni lazima mfanye kazi sana, wa ya ziada, wachezaji wenu wamekosa mbinu na uwezo wa kujiamini.


"Tengenezeni safu ya ushambuliaji kuwe na washambuliaji watatu au wanne, badala ya kuishia kulinda goli, timu kama Ivory Coast inatumia washambuliaji watatu, mnapokutana na timu kama hii ni ngumu sana kushinda.


"Ni lazima mfungwe kwa sababu inashambulia sana, mnabaki mkilinda goli," alisema.


Akizungumzia mchezo wao na Rwanda, Holilhodzic alisifu kiwango cha Rwanda ingawa alidai vipo sawa na Tanzania kwani haikuwa rahisi kwao kushinda mchezo huo kwani wachezaji wake walitengeneza nafasi nyingi lakini kuna wakati washambuliaji wake walimuangusha.


Alisema ushindi wa mechi hiyo, umempa faraja kubwa kwani ni mechi yake ya 10 kushinda kati ya mechi za kirafiki walizocheza na hawajapoteza mchezo hata mmoja, hivyo anatumaini kufanya vizuri kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,222
Likes
883
Points
280
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,222 883 280
huyu kocha kaongea ukweli mtupu, tutengeneze washambuliaji sio wa kuokoteza mtaani kuanzia kwenye under 12, 15, 17 hapo tunaweza sema tuna watu walipikwa, na sio kubaki kumlaumu maximo wakati hamkuandaa wachezaji
 
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Messages
2,969
Likes
224
Points
160
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2008
2,969 224 160
Mtanzania halisi anapenda alale maskini aamke tajiri na uozo huu ndo umejaa kuanzia kwa wanasiasa, serikalini na hata michezoni.

badala ya TFF ijenge sports academy ambayo itachukua vijana wa under 15, 17, 19 na kuwafundisha mpira wao wanataka wachukue makapi kutoka ligi ya mchangani ya simba na yanga!
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Sasa huyo kocha wa Ivory Coast mbona ameanza kuweka defence hata kabla hajaja! Kadai hatuna washambuliaji, sasa yeye akija atawapatia wapi? Si sawa na Maximo ambaye alikuwa anadai anajenga timu "ya miaka mingi ijayo?" Na hao akina Leodger Tenga mbona hawafanyi chochote kuhusu shule za michezo ili kufundisha u-12, u-15, u-17, etc? Kazi yao ni kuangalia mapato tu ambayo hatuoni kama yanafanya chochote kuendeleza soka! Hapa solution ni serikali kutunga sheria kuhusu michezo! Mpira wa ridhaa usiwepo tena, uwe wa kulipwa. Kuwe na bima kwa wachezaji ili kulinda maslahi yao wakiumia au baada ya soka. Vilabu viwe na timu za vijana kuliko kupora wachezaji wa timu nyingine, nk. Kwa ujumla yafanyike mabadiliko makubwa kwenye soka na michezo kwa ujumla!
 
Bantugbro

Bantugbro

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2009
Messages
2,932
Likes
521
Points
280
Bantugbro

Bantugbro

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2009
2,932 521 280
Sasa huyo kocha wa Ivory Coast mbona ameanza kuweka defence hata kabla hajaja! Kadai hatuna washambuliaji, sasa yeye akija atawapatia wapi? Si sawa na Maximo ambaye alikuwa anadai anajenga timu "ya miaka mingi ijayo?" Na hao akina Leodger Tenga mbona hawafanyi chochote kuhusu shule za michezo ili kufundisha u-12, u-15, u-17, etc? Kazi yao ni kuangalia mapato tu ambayo hatuoni kama yanafanya chochote kuendeleza soka! Hapa solution ni serikali kutunga sheria kuhusu michezo! Mpira wa ridhaa usiwepo tena, uwe wa kulipwa. Kuwe na bima kwa wachezaji ili kulinda maslahi yao wakiumia au baada ya soka. Vilabu viwe na timu za vijana kuliko kupora wachezaji wa timu nyingine, nk. Kwa ujumla yafanyike mabadiliko makubwa kwenye soka na michezo kwa ujumla!
Ni kweli mkuu, lazima atueleze kinagaubaga ni jinsi gani atatubadilishia timu yetu na ni wapi atakapowatoa hao wachezaji anaowasema!. Ama kazi yake itakuwa ni kujakuwaongeza confidence wachezaji wetu?? maana kasema hawajiamini...

Hatutaki tena mambo ya ahadi za kibabaishaji ili tu mtu apewe kazi wakati akijua kabisa kazi yenyewe itakuwa ngumu. Tunataka mtu ambaye atatuendeleza kutoka hapa tulipo na sio kuanza tena upya. Akumbuke pia term limit ni miaka 3 tu.

Maximo amefanya kazi kubwa sana na wote tumeshuhudia akiwapika washambuliaji kama Tegete, Makasi, n.k. toka chini kabisa, siku hadi siku wanazidi kuimarika kimbinu. Kwanini Maximo anapendelea kujaza viungo wengi na kuwa defensive Vahid tayari nalo jibu, mwenyewe keshasema aina ya wachezaji tulionao ni tofauti! siku hizi wachezaji wetu wanamiili midogo(sijui kwa nini) lakini wanakasi sana kuliko wachezaji wa West Afrika ndio maana magoli yetu tunayapata kwenye counter attacks ama baada ya viungo wetu kuwapora mpira wapinzani. Tazama lile goli alilokosa Tegete (aliopiga mwamba wa pembeni) mpira ulianzia nyuma kabisa baada ya sisi kukoswakoswa alhamoud alipika shambulizi zuri la haraka kutokana na kasi na wepesi wa wachezaji wetu.

Hivi ameshasahau kuwa kwenye CHAN ambayo ilichezwa huko kwao Abidjan hao Stars waliifunga timu yake? hata kama atesema si timu hii ya akina Drogba lakini mfumo wa uchezaji wao kitaifa pamoja na aina ya maumbile yao ni ile ile!!

Mwisho, ni desturi ya makocha kupondana pale wanapotafuta ulaji, sijawahi kusikia kocha anayewania timu fulani kusifia hali/mfumo anaoukuta toka kwa kocha aliyekuwepo.

Karibu Tanganyika na pia hapa JF monsieur Vahid...
 

Forum statistics

Threads 1,238,061
Members 475,830
Posts 29,310,531