Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Huyu kijana hakujua kama kagongwa alidhani koboko kamchubua kidogo tu.baada ya muda kidogo akaanza kulalamika haoni vizuri na akaanguka na kufa.
Sahihi kabisa nadhani angekua amekulia Tabora au kwingineko kwenye Koboko wengi angeshasema nimeng'atwa, sasa UK wanaona nyoka kwa TV,,, huyo nyoka hatari sana asee.
 
Nyoka wengi hua wana aibu na huwa wa kwanza kuretreat unless wawe cornered, koboko hajui kuretreat, ana accuracy, speed na bado yeye ndiyo ataanzisha ugomvi.

Iwe iwavyo ninachojua hachomoki mbele ya honey badger.

Kwa CHUI pia hagusi...bora nikutane na mnyama wa aina yeyote hapa ulimwenguni ila sio Chui/Jaguar
 
Huyu nimeshawahi kukutana nae juu ya muembe alikua na urefu wa mita mbili.........asee acha kabisa nlikua kileleni nafuata maembe kumbe yalipo maembe ndipo alipo yeye ....ila uzuri alianza kuniona yeye sasa wakati me naweka mkono kwenye embe bwana we natupa jicho vizuri kajaa yeye nilishuka kwa speed ya jet halafu ye wala hakua na habari na Mimi alitulia tu.........nlivofika chini nikaita wanaume wakaua
Kipindi hicho ww hukua mwanaume eeeeh?
 
Ukikutana na simba au chui anakukimbiza na kukuua na kukutafuna mara moja. Ukikutana na Black Mamba anakimbia kujilinda tofauti ni kubwa kati ya nyoka na hawa wafalme wa pori. Black mamba anakuwa mkali sana kama umemkanyaga au atakapohisi amezingirwa na hana pa kutorokea/kukimbia. Ukikutana nae uso kwa uso anakimbia sana, labda kama hana pa kukimbilia ndio atakuattack. Kwa wale wenye DSTV Channel 136 saa moja na nusu usiku Jumatatu mpaka Ijumaa kuna kipindi kinaitwa snakes in the city wale jamaa wanakampuni ya kukamata nyoka ukiona nyoka unawapigia wanakuja kumchukua faster, wamebase South Africa wanakamata nyoka kwa mikono mitupu akiwemo huyo black mamba.
Ndio nyoka mwenye kasi kuliko wote duniani.
Nilimsikia mkamata nyoka anasema Black Mamba kabla hajakung'ata anakupa tahadhari!! Sasa maelezo ya humu yako mchanganyiko sana.

Wengine wanasema Koboko ni mshari hata kama hujamchokoza atakufata akung'ate.
 
Hatari za nyoka
1. COBRA (wanaitwa spitting cobra) wanatema sana mate yanafika hata mita kumi, mara zote wanalenga macho na wakikupata unakuwa kipofu ukichelewa kunawa haraka na maji. Wataalamu wanasema wako precise kiasi kwamba akiamua kutema ana uhakika lazima yakupate machoni, hatemi ovyo ovyo.

2. Mambas (Black&Green) wanameno makali sana kama sindano yana tundu katikati (kama sindano ya hospitali) kwa ajili ya kupump sumu, akikung'ata anapump sumu kwa kiwango cha ukubwa wa adui, kiwango anachopump kwa panya sio sawa na anachopump kwa binadamu. Kwa wakati mmoja anakuwa na sumu ya kuua watu 20 kwa mara moja. Huyu black mamba anaongoza kwa mbio akikimbia unaona kama anateleza na kicha anakiinua kidogo wakati anakimbia.

3. CHATU (python) huyu hana sumu kabisa yeye anatumi nguvu tu kumnyonga adui mpaka afe. Ana misuli ina nguvu sana akikuvingirisha ni ngumu kujinasua, wataalam wanashauri akikukamata upambane nae sana usiogope sura yake mbaya tumia nguvu sana kujinasua.

MUHIMU: Kwa haraka haraka jinsi ya kumjua nyoka asiye na sumu na mwenye sumu.

-Nyoka mwenye macho ya round na makubwa hana sumu kabisa mshike tu hawezi kukufanya chochote (ni kama toy)

-Nyoka mwenye macho yaliyochongoka (yako umbo la oval) ukimuona kimbia sana atakuua huyo.

Duniani nyoka wenye sumu ni asilimia 25 tu 75 hawana sumu kabisa.
Uchambuzi mzuri sana
 
NI NYOKA WENYE SUMU KUBWA SANA,MFANO TUU BLACK MAMBA AMBAYE HUKU NDIO TUNAMWITA KOBOKO ANAUWEZO WA KUKUGONGA MARA 120 BILA KUCHOKA WALA KUPUNGUZA KIWANGO CHA SUMU ANAYOTEMA KILA ANAPOKUGONGA,SUMU AMBAYO INAKWENDA KUHARIBU NEVA ZA FAHAMU,PIA CHEMBE ZA KUGANDISHA DAMU ILI USITOKE KWENYE JERAHA YAANI PLATELETS HUWA HAZIWEZI ZUIA DAMU ISIACHE KUTOKA,NA PIA HUATHIRI MFUMO MZIMA WA DAMU,NI NYOKA HATARI SANA,

Sio Green Mamba Eastern green mamba - Wikipedia
 
huyo mtaalam... huwa hafanyi makosa akiwa kazini, kipind cha zaman kidogo.... wazungu walienda tabora... wakasikia habari ya kiumbe huyu( kama ilivyo marufuku kumtaja jina)... wakabisha sana juu ya habar zake... maana wao walikuwa wanaamin hakuna kama cobra..

shauku ilivyowajaa... wakatoa dau zuuri... kwa kijana atakayemkamata 'mtaalam' na kuwaletea..... ghafla akajitokeza masai mmoja kwa kujiamin.. kuwa wampe siku tatu... atakuwa ameshamkamata....

masai akazama vichakani.... katika kupitapita... akamkuta mtaalam anakula asali..... masai akamvalisha gunia mtaalam pamoja na mzinga wa asalii.....

aisee... itaendelea... nisije nikafungua uzi ndan ya uzi....
Koboko ni jamii ya cobra
 
Koboko ni hatari mno katika nyoka. Ila kwa simba, chui or jaguar hafui dafu...watamvunja vunja mpaka bas.
Mkuu Simba naturaly ni muoga wa nyoka kuliko sisi wanadamu.nilishuhudia video moja swila alimgonga Simba na watoto wake watatu,watoto ni pale pale lakini mama Simba aliteseka siku mbili mate yakimwagika..hatari sana.
 
Koboko ni hatari mno katika nyoka. Ila kwa simba, chui or jaguar hafui dafu...watamvunja vunja mpaka bas.
Atakae vunjwa ni nani hapo
Koboko ni hatari sana halafu isitoshe yeye anatambaa na wakati mwingine ananyanyua mwili wake kwa theluthi.
Yeye ni kugonga tu nilishuhudia kangonga ng'ombe haikuchukuwa mda povu na kunya hapo hapo halafu miguu ikanyooka

Hatuwezi kufananisha ugomvi wa simba au chui kwa nyoka maana mshindi always ni nyoka
 
Mkuu Simba naturaly ni muoga wa nyoka kuliko sisi wanadamu.nilishuhudia video moja swila alimgonga Simba na watoto wake watatu,watoto ni pale pale lakini mama Simba aliteseka siku mbili mate yakimwagika..hatari sana.

Duhh! Hatari sana
 
Duhh! Hatari sana
Kuna jamaa aling'atwa na Koboko kwa bahati nzuri alipona wakati yuko hospitali anatibiwa na shots za anti venom alikuwa anasikia kila kitu hata maongezi ya watu alikuwa anawaelewa lakini kila akijaribu kufungua macho anashindwa baada ya siku nne ndio kufungua macho.

Sumu ya Koboko ikishakuingia kwanza unaparalaiz halafu ndiio inasimamisha moyo.
 
Mkuu Simba naturaly ni muoga wa nyoka kuliko sisi wanadamu.nilishuhudia video moja swila alimgonga Simba na watoto wake watatu,watoto ni pale pale lakini mama Simba aliteseka siku mbili mate yakimwagika..hatari sana.
Aisee niliiona hiyo clip
 
Back
Top Bottom