Smart Guy
JF-Expert Member
- Dec 19, 2016
- 6,701
- 6,658
Na haka kandege kanarusha mateke vibaya mno, jet li akasomeNa ndege anaitwa secretary,anatafuna kila nyoka atakayekatiza mbele yake
Na haka kandege kanarusha mateke vibaya mno, jet li akasomeNa ndege anaitwa secretary,anatafuna kila nyoka atakayekatiza mbele yake
Mambo ya Kutembea na Jungu achana na huo ujingaa mkuu... Vingine vyote point!!
Black Mamba au Koboko ni moja ya kiumbe hatari kuliko hapa duniani na hii ni kwa sababu ya mkusanyiko wa sumu kali alionao, nyoka huyu ana aina mbili za sumu ambazo hufanya kazi kwa pamoja na endapo mtu atang’wata basi ndani ya dakika 3 hadi 10 mtu huyu akikosa matibabu hupoteza maisha.
Nyoka hawa huwa na maeneo maalumu ya kung’ata ambayo ni kichwani, shingoni au kifuani kwani mara nyingi hukaa juu ya mti, na ukiwakuta chini urefu wao ni futi 16 na akiwa na hasira husimama nusu mwili wake ambapo ni sawa na futi 8.
Wataalamu wanashauri jinsi ya kumuua ni kuchemsha chungu cha maji ya moto au uji kisha kujitwika kichwani na kupita maeneo ambao wanapatikana nyoka hawa, wakitaka kung’ata katika maeneo yao huishia kudumbukia ndani ya chungu hiko chenye kimiminika cha moto, hufa.
Lakini pia nyoka huyu unaambiwa anauwezo wa kutembea mwendo kasi mkubwa sana ambapo anaweza kukimbia 23km hadi 25km ndani ya saa moja, huku binadamu wa kawaida ana uwezo wa kukimbia 12km ndani ya saa moja na endapo mnyama huyu ataamua kung’ata sehemu yenye kundi kubwa la watu basi anauwezo wa kung’ata kunzia watu/wanyama 70 nakuendelea bila kuchoka.
Hapa nchini kwetu nyoka aina hii hupatikana kwa wingi mkoani Tabora na sehemu zenye misitu mikubwa kama vile, Iringa, Morogoro, Milima ya Udzungwa huko wapo wegi sana.
Pia nyoka aina hii hutajwa katika orodha ya wanyama wanaoongoza kuuwa watu wengi zaidi duniani.
Na unaambiwa nyoka huyu akiwa msituni hapendelei kusikia kelele au milio ya gari na mara nyingi endapo atasikia mlio wa gari hupendelea kuufuatilia mlio huo nakufanya shambulio hivyo inashauriwa kufunga vizuri vioo vya magari wakati wa kupita msituni.
Na wataalamu wanashauri kuwa endapo nyoka huyu atakuwa amejificha katika upenyo wa gari basi ni vyema dereva kukimbiza gari hilo kwa mwendo kasi usiopungua 80 na kuendelea kwa ndani ya dakika 10 hadi 15 ili kusaidia kummaliza nyoka huyo kutokana na joto kali au kumchosha nyoka huyo na kumpunguzia makali ya sumu yake ya kudhuru watu.
Ni kweli kabisa.Na haka kandege kanarusha mateke vibaya mno, jet li akasome
mongoose anaweza akakimbia msosi akikutana na nyoka mbabe,ila huyo ndege ni balaa,ana miguu mirefu,anarusha mateke vibaya mno.Secretary bird kana miguu mirefu hivi yule ni kiboko ya nyoka.Watemi wengine wa nyoka ni honey badger na mangoose
hao wanaweza kuwa rangi yeyote,ila mdomoni kwa ndani ni peusi,ndiyo maana wanaitwa black mamba.Black mamba ni nyoka Wale wa kijani si huyo koboko
Na Sifa zake zote hizo ulizotaja lakini ndio chakula pendwa kwa Wachina, Wanamla vizuri na kumfurahia.
Kofia ngumu je akikupapasa shingoni ushahisi kitakachokutokea mkuu?maana bora chungu akishuka akikigusa hata kwa bahati mbaya atakuta nacho ni cha moto atainuka juu hiyo kofia ngumu akiigusa si ndo atatelezea hapo shingoni.
Honey badger yeye akigongwa na nyoka anazimia baadae anananyanyukamongoose anaweza akakimbia msosi akikutana na nyoka mbabe,ila huyo ndege ni balaa,ana miguu mirefu,anarusha mateke vibaya mno.
nyoka ndiyo msosi wake pendwa,siyo kama nyegere,anakula nyoka for fun tu.
Kweli kabisaHoney badger yeye akigongwa na nyoka anazimia baadae anananyanyuka
Green Mamba na Black Mamba Dugu MojaWanaokaa kwenye miti kumendea utosi si ni green mamba hao.
Ila ni species tofauti.Green Mamba na Black Mamba Dugu Moja
Ukisikia nyoka pendwa wa JF basi ujue ndio huyo mkuuHuyu nyoka anapendwa sana hapa JF.
Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani
Vipi umekumbana naye mkuu?Kweli huyu nyoka hatari sana.
Hapana niliona documentary yake ni hatari sana.Vipi umekumbana naye mkuu?
Ukweli ni upi?Huu ni uongo