Koboeni mahindi muondoe sumu

Koboeni mahindi muondoe sumu

Shirika lisilo la kiserikali la World Vision limesema kuna umuhimu wa kukoboa mahindi ili kuondoa sumu zenye athari kwa binadamu.

Akizungumza katika mkutano wa wazalishaji hao jana, meneja mradi wa urutubishaji vyakula wa World Vision, Symphrose Uisso alisema: “Kwanza uhifadhi wa mahindi katika nchi yetu uko duni sana. Matokeo yake mahindi huota sumu ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu kwani inaweza kusababisha saratani. Vilevile viuatilifu vinavyotumika kuzalisha na kuhifadhia nafaka vina madhara.“Baada ya kukoboa mahindi tunayo teknolojia ya kuongeza virutubisho vinavyokosekana kwenye unga wa mahindi,” alisema.

Shirika hilo pia linakamilisha mchakato wa kuwafadhili wazalishaji na wasambazaji wa unga wa mahindi jijini Dar es Salaam mashine za kuongeza virutubisho.
Kama kukoboa kunaondoa virutubisho kwanini isitafutwe njia sahihi ya kuhifadhi? Ukikoboa mahindi hakuna panya wala mdudu anaeyala kwa kuwa hayana lishe. Dona ndiyo mpango mzima.
 
eeeeh wameona watu wanakula dona sasa wanaona njia halis ni kuwapa sumu

..devil katik kuua
 
Huyu jamaa atatupotosha. Badala ya kuleta teknolojia ya kuongeza virutubisho angeleta teknologia ya kuhifadhi mahindi. Hatukoboiiiiiiiiiiiii tunakula dona. Pakua hiyo picha kisha nenda Moshi utawakuta barabarani kama km 10 baada ya njia panda ukielekea Moshi.View attachment 361484 au google www.riela.co.tz/

Pumbavu zao, wanataka tukoboe mahindi ili tubakie gentamycne. Nitamwambia wife AOSHE, ASAGE
 
Wana upungufu wa madini joto hao! Hiyo elimu waipeleke Ulaya! Tena ndio wamenizidishia hasira ya kula dona!
 
Nakula dona safi tu..dona lina mahindi,mchele,mhogo na ngano..
Wakoboe wale makapi wenyewe..
Haiwezekani panya amzidi binadamu akili..
Unanikumbusha Dr.Ndodi mkuu. Ameahidiwa 10% na wauaji eti watuongezee vitamin kumbe ni magonjwa na mabalaa wanatuwekea. Tushirikiane kuikataa sembe......DONAAAAAA ndo chakula
 
Tuna tatizo, huwa tunasoma vichwa vya habari na kuanza kuchangia pasi na kujua kilichoandikwa ndani. Mtaalamu hajakosea kusema alichokisema. Na hajakataza kula dona kama ni salama. Ukweli ni kuwa mahindi yana sumu nyingi sana zinazowekwa wakati wa kuyahifadhi. Sumu hizo zina madhara kwetu walaji kama hazitaondolewa.

Ila siungi mkono hiyo nyongeza ya virutubisho... Ni bora kufundisha namna bora ya kuhifadhi mahindi ili yaendelee kuwa bora kwa matumizi ya binadamu.
 
Unanikumbusha Dr.Ndodi mkuu. Ameahidiwa 10% na wauaji eti watuongezee vitamin kumbe ni magonjwa na mabalaa wanatuwekea. Tushirikiane kuikataa sembe......DONAAAAAA ndo chakula
Wanataka kutumaliza hawa..
Wazungu si watu Wa kuchekea kabisa..inabidi uwasikilize na kuyaacha hapo(baadhi ya mambo)
Jiulize kwanini vijana wanahangaika Sana na wimbo wa nguvu za kiume??

Wazungu hawataki kabisa muafrika ajiamini..angalia wamewaletea hizi camera ukipiga hata uwe mweusi kiasi gani..unatoka kama mchina..hii yote ni hawataki muafrika ajiamini kwa alichonacho..

Kwa sasa wanataka kututawala kifikra na wamefanikiwa kwa baadhi!!
 
N

Na wanawake wamewakamata kwenye mawigi na dawa za nywele wakifanikiwa kuwateka kwa unga wa kukoboa ndo tutegemee kuzaa kizazi cha watoto wenye upungufu wa kila namna halafu wanaanza kutengeneza madawa ya kutuuzia.
 
Hivi katika aina mbili za unga wa Mahindi ni upi ulikobolewa kati ya Sembe na Dona?
UHIFADI BORA WA MAHINDI. HAKIKISHA YAMEKAUKA VIZURI NA HIFADHI KWENYE CHOMBO KISICHOPITISHA HEWA HUTAITAJI DAWA YA KUIFADHI NA WADUDU WAZALISHA SUMU HIZO HAWATAISHI KWENYE HIFADHI YAKO HIYO BORA YA NAFAKA NYUMBANI.
Dona ni bora, ila mahindi yenyewe sasa ndio issue....mengi yameoza,yana dawa,wadudu ila kama umelima mwenyewe unajua umelimaje safi.

Tuna tatizo, huwa tunasoma vichwa vya habari na kuanza kuchangia pasi na kujua kilichoandikwa ndani. Mtaalamu hajakosea kusema alichokisema. Na hajakataza kula dona kama ni salama. Ukweli ni kuwa mahindi yana sumu nyingi sana zinazowekwa wakati wa kuyahifadhi. Sumu hizo zina madhara kwetu walaji kama hazitaondolewa.

Ila siungi mkono hiyo nyongeza ya virutubisho... Ni bora kufundisha namna bora ya kuhifadhi mahindi ili yaendelee kuwa bora kwa matumizi ya binadamu.
 
Hawa wanataka kuwaua wagonjwa wa kisukari
 
Sumukuvu daa!!
Hakika kila kona tunatafutwa.
 
Mi nafikiri wangetoa elimu jinsi ya kudhibiti hiyo sumu ,namna bora ya kulima mazao bila kuongeza sumu mfano kuua wadudu kwa njia ya biological control ile ya kwenye ecology na vinginevyo na si kutuletea mashine za kuongeza virutubisho kwa sababu vizazi vijavyo vinaweza vikaambukizwa utamaduni mbaya wa kuongeza virutubisho kwenye unga kwa gharama kubwa
 
Back
Top Bottom