KKKT Singida Usharika wa Emanuel

KKKT Singida Usharika wa Emanuel

asubuhi sana

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2015
Posts
1,669
Reaction score
1,418
Habari za jumapili ya leo wapendwa wanaJamiiForums.

Leo katika kanisa la Kiinjili la kiluteri Tanzania, Singida Usharika wa Emanueli (msalaba mrefu)

Nimetokea kupenda kauli ya msaidizi wa Askofu Singida, baada ya Mh. Lazaro Nyalandu Mbunge wa Maliasili na Utalii kuwa mmoja ya washiriki wa ibada kanisani akiwa na wasindikizaji wake katika safari ya kwenda Dodoma kuchukua form baada ya kutangaza nia yake ya Urais.

Kauli kutoka kwa msaidizi wa askofu, kasema, " Kanisa halina chama ila waumini wake ndio wenye chama" kafafanua zaidi kasema wapo CHADEMA, CCM, CUF na n.k

Hii ni kwamba wagombea wengi wanakimbilia sehemu za ibada kuwa sehemu zao za kupigia kampein au kutoa sera zao, musaidi wa askofu amempongeza mh. Lazaro Nyalandu kwa kutembelea sehemu za ibada na kuachana na imani za kukimbilia kwa sanga tit kujipatia mahirizi.

Hali ikoje huko mlipo katika sehemu zenu za ibada?

Nawasilisha
Mr. Asubuhi sana
 
Namshukuru Askofu kwa kuonyesha msimamo wa kanisa.



Siyo wale askofu njaa wa dar, poor!!
 
Makanisa ya Lutheran , Anglican na Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume yanajielewa. Hutaona hata siku moja viongozi wao wanaalikwa kwenye kampeni kumwomba Mungu majukwaani ili awape huyo mpiga kampeni kama Raisi wao. Jukumu la kiongozi wa dini ni kuomba kwenye nyumba za ibada ili Mungu awape kiongozi bora. Yeyote atakayechaguliwa basi huyu ndio Mungu aliye wapa na wanatakiwa wamuwekee mkono kwa kumbariki. Sasa kiongozi wa dini unapojipambanua wazi wazi jukwaani kwamba Mungu awape huyo mgombea !!!je akishindwa ni kwamba Mungu kakataa maombi yako!! au Mungu wako hana nguvu!!! na itakuwaje kama ambaye hukutaka awe raisi lakini MUngu akasema ndiye !! akija kwenye upeo wa himaya yako kama kusali utajisikiaje????
 
Rais wa Tanzania awe nyalandu?

Huwezi jua, jana yake kwenye uwanja wa namfua sgda alionesha kutowashambulia wapinzani kwa maneno kama watangaza nia wengine wanavyofanya, kiukweli hata wananchi walielewana nae
 
Hivi nyalandu anataka kuwa rais wa wapi labda kwa mfano?

Tanzania mkuu, ya mungu mengi, lakini hata mm nilishtuka kusikia anatangaza nia kwasababu mara ya mwisho kwenye mkutano wake jimboni kwake ilongero aliwahi kusema atagombea urais mwaka 2020 iv kama sijakosea, lakini cjajua nia yake kugombea hivi sasa
 
Nimeumis sana Usharika wangu. Enzi hizo kushoto Msifuni, kulia Angaza. Thanks best kuturudisha home.
 
Back
Top Bottom