KKKT lahaha kumsafisha Askofu Malasusa

KKKT lahaha kumsafisha Askofu Malasusa

Kaka kumbuka huyo anayeshutumiwa ni mwanadamu sio malaika, usijekuta izo shutuma ni za ukweli, labda Kama huyo mlalamikiwa sio rijali ni hanisi.. ,,na ilo gazeti pia sio kwamba wanalishambulia kanisa bali ni MTU km MTU kwa alichofanya,,,,
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu. Lakini tunachopinga kwanini Mwanahalisi wanaandika habari za upande mmoja? Bila ya kuwa na uthibitisho? Mambo haya yangefanywa na shigongo, siyo kubenea! Credibility ya mwanahalisi imeshuka sana!
 
Huu upuuzi wa Mwana Halisi utafikia kikomo lini, naona mleta mada wa awali kaamua kubadili ID kabisa...
Dayosisi ya Mashariki na Pwani wenyewe Wazaramo, Wakutu, Wakwere na Wazigua wanaitaka. Sasa hivi imekuwa ya Wachagga na Wanyakyusa. Malasusa ni kikwazo kikubwa kwa Wazaramo kufikia lengo. Kwa style ile ile ya **** Kapuya na Tanzania Daima, shughuli imehamia kwa Malasusa. George Fupe na kundi lake wanajitahidi...
 
Wewe ndio mpuuzi mwili mzima; kwani unamkingia kifua muhuni; mgoni eti mtumishi wa Mungu anayeshiriki kuvunja taasisi takatifu ya ndoa! Ushindwe na ulegee kwa jina la Yesu!
Kama Malasusa ni msafi ajitokeze hadharani akanushe taarifa hizi yeye
mwenyewe au kama ni taarifa za kizushi akafungue mashtaka; tumechoka na mitumishi mifirahuni inayojificha nyuma ya jina la kanisa! Malasusa come clean; kunyamaza kwako kunalidhalilisha kanisa la Mungu!
Mwanahalisi wameitengeneza hili habari wakijua kuna kunguru kama wewe utaamini habari za kuokoteza okoteza zilizoungwa ungwa kwa malengo maalum. Ni masikitiko makubwa kunguru mpo wengi sana, mtaamini huu umbea na kuusambaza. Hivi ni vita tu kama vilivyo vita vingine. Soon Mwanahalisi watakaa kimya na wenye akili watasonga mbele
 
TAMKO limeandaliwa ili kusafisha tuhuma zinazomkabili Dk. Alex Malasusa, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania, (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), anaandika Josephat Isango.

Taarifa kutoka kwenye kanisa hilo zinaelezwa kwamba, tamko hilo limeandaliwa ili kushawishi waumini wapuuze taarifa zilizoandikwa kuhusu Askofu Malasusa na kwamba, yeye (Malasusa) hatotakiwa kusema lolote kuhusu tuhuma zake.

MwanaHALISI online, limeona waraka unaotarajiwa kusambazwa wakati wowote kuanzia sasa ambao umeelekezwa kwa wakuu wa majimbo, wachungaji, viongozi, wakuu wa vituo na taasisi pamoja na washirika wote.

Wakati kanisa likiandaa tamko hilo, Dk. Malasusa hajaandika wala kukanusha tuhuma zinazoelekezwa kwake wala kuzungumzia sakata la Muhimbili, sakata la watoto watatu ambao walitarajiwa kusafiriwa nje ya nchi.

Mzazi wa watoto hao, Venance Mwakilima aliiomba Mahakama ya Mwanzo Maili Moja kumpa amri kamishana wa uhamiaji azuie watoto wake wasisafiri nje ya nchi kama ilivyodaiwa.

Tamko hilo halijawataja Sijenuna Venance Mwakilima, mwenye hati ya kusafiria Na. AB 524934, Stephania Venance Mwakilima Na. AB 524933, Simon Venance Mwakilima Na. AB 599057 na mama yao Leita Ngoyi Mwakilima Na. AB.524932.

Tamko linasomeka “Wapendwa watu wa Mungu. Habari zilizoandikwa na gazeti la MwanaHALISI na Mseto yanayomilikiwa na kampuni moja ya Hali Halisi Publishers Ltd, kuhusu Askofu wetu sio za kweli,”
ChSlCkLVEAEvXF7.jpg:large

Linaongeza kwamba, “Kanisa limetafakari kwa kina kuhusu habari hizo na malengo ya mwandishi huyo kuandika kwenye magazeti yote mawili kwamba, alilenga kulishambulia Kanisa kwa sababu anazozijua mwandishi na mmiliki wa magazeti hayo.

“Kanisa linapenda kuwaomba waumini wote na jamii kwa ujumla, kuwa wavumilivu na kuendelea kuliombea Kanisa na uongozi wake huku hatua stahiki zikichukuliwa.”

Baadhi ya wachungaji walioongea na mwandishi katika Ibada za Jumuiya leo Jumamosi, wamesema Kanisa halihusiki na tuhuma za mtu binafsi, kwani Kanisa halikuenda Muhimbili, wala halikuandika ujumbe wa simu za kimahusiano na mke wa mtu, wala kutoa maelekezo ya kuwaficha watoto.

“Hilo ni suala lake binafsi, na watu wanapolalamika hawalalamikii Kanisa, wanalalamikia tabia ya mtu,” amesema mchungaji aliyedai kuwa anamfahamu Dk. Malasusa kwa karibu.

Kwa upande mwingine, familia ya Venance Mwakilima wamezungumza na mwandishi na kuahidi kuwa, wanasubiri tamko hilo lakini kama watakuwa na suala la kujibu watasema kwani wao hawana ugomvi na Kanisa bali tabia ya Dk. Malasusa.

“Nimemwandikia Askofu ujumbe mfupi kwa njia ya simu ukisema, Baba Askofu nilikwambia tukae kikao ukadharau, ukanipuuza sasa mambo yalipofika huku ndio unafurahi?”

Amesema Asime Mwakilima, kaka wa mume ambaye ameahidi kuwa, akirejea kutoka Mbeya atazungumza mengi zaidi huku akimlaumu Askofu kwa kutojibu ujumbe wa simu aliomwandikia.

Aidha mume aliyelalamika na kumtuhumu Askofu Malasusa, ameyashukuru magazeti ya MwanaHALISI na Mseto kwani baada ya habari hizo kuandikwa, kesi alizokuwa anabambikizwa zimefutwa zote, na watoto wote walikuwa wamefichwa wamerejea nyumbani leo asubuhi tarehe 30 Aprili 20016.

Askofu Malasusa anatuhumiwa kujihusisha kimapenzi na mchungaji wa kanisa hilo ambaye ni mke wa mtu.

Anayemtuhumu Dk. Malasusa ni Mwakilima, mkazi wa eneo Vikawe, Bagamoyo ambaye ni mfanyakazi wa Shule ya Msingi Dunda.

Dk. Malasusa anadaiwa kuwa na uhusiano na Leita Ngowi, mchungaji na mkurugenzi wa idara ya wanawake usharika wa Azania Front, Jijini Dar es Salaam aliyepandishwa cheo siku za karibuni na askofu huyo.
 
Bado kuna wajinga sana na wehu hapa tanzania,malasusa ni mtu kama wengine,ana mapingufu kama wengine,nyie mnansemea nyie kina nani? Familia yake au wasemaji wake? Na kwa nini kanisa liandae waraka wa kumsafisha? Kama ametenda ukweli utajulikana,na vilevile kama hajatenda.acheni ujinga kumtetea mtu wakati yeye yuko kimya.
Au ndo mafundisho yenu? Na wengine leo mnaliponda mwanahalisi kwa kuwa limemwandika malasusa,
 
Wewe ndio mpuuzi mwili mzima; kwani unamkingia kifua muhuni; mgoni eti mtumishi wa Mungu anayeshiriki kuvunja taasisi takatifu ya ndoa! Ushindwe na ulegee kwa jina la Yesu!
Kama Malasusa ni msafi ajitokeze hadharani akanushe taarifa hizi yeye
mwenyewe au kama ni taarifa za kizushi akafungue mashtaka; tumechoka na mitumishi mifirahuni inayojificha nyuma ya jina la kanisa! Malasusa come clean; kunyamaza kwako kunalidhalilisha kanisa la Mungu!
Nashindwa kuelewa watu wanaotetea uovu... Kama ni kweli malasusa kafanya hilo basi lazima awajibike

Malasusa ni mlutheri lakini ulutheri sio malasusa.m so kanisa halitakiwi kutetea uovu na waumini pia wasiunganishe kanisa na mwovu
 
chichi waumini tumecha jua huyu bwana anatembeza ZAKARI yake ovyo hata aibu nkubwa nzima baaaaaa tunsifu yesu kristu
 
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu. Lakini tunachopinga kwanini Mwanahalisi wanaandika habari za upande mmoja? Bila ya kuwa na uthibitisho? Mambo haya yangefanywa na shigongo, siyo kubenea! Credibility ya mwanahalisi imeshuka sana!
Upande mmoja vipi wakati malasusa hata wanafamilia wanaolalamika hakuwajibu ujumbe!
Halafu kwani malasusa hajui kusoma au kuandika?
Anakaaje kimya kwenye tuhuma nzito kama hizi?si jitokeze aseme na yeye?
ATAKUWA NI MZINZI TU.
 
Dunia ya sasa hakuna siri na jambo lolote ukilifanya chini ya jua useme hakuna atakae jua hiyo sahau.
Uongozi ni karama toka kwa Mungu ila hakuna tena binadamu wateule kwa kwa ajili ya kazi ya Mungu.
Habari ni hii inamuhusu kiongozi wa kiroho tena mkuu wa kanisa kitu ambacho ni chukizo mbele za Mungu
Ni wakati tu ukweli utadhihiri majibu yatapatikana lkn je atafaa tena kusimama madhabahuni kulisha kondoo wa bwana? La.
Kama ni tuhuma hazikustahili kwa kiongozi kama yeye.
Poleni kkkt kwa kuwa na viongozi wa tuhuma
 
Upande mmoja vipi wakati malasusa hata wanafamilia wanaolalamika hakuwajibu ujumbe!
Halafu kwani malasusa hajui kusoma au kuandika?
Anakaaje kimya kwenye tuhuma nzito kama hizi?si jitokeze aseme na yeye?
ATAKUWA NI MZINZI TU.
Hebu huyo Mwanahalisi afanye ufukunyuku kwa kufuatilia mambo aliyotenda akiwa Dodoma. Kule walimstahi ila huko naona wanamwanika hadharani.
 
Upande mmoja vipi wakati malasusa hata wanafamilia wanaolalamika hakuwajibu ujumbe!
Halafu kwani malasusa hajui kusoma au kuandika?
Anakaaje kimya kwenye tuhuma nzito kama hizi?si jitokeze aseme na yeye?
ATAKUWA NI MZINZI TU.
Haya Asante, wewe uhukumuye, nawe pia utahukumiwa kwa kipimo hiki hiki! Ila MWANAHALISI limejipoteza kwenye ulimwengu wa Habari, bora lingeendeleza ule udaku wake wa kwenye siasa, ila huku dinini wameingia chaka!
 
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu. Lakini tunachopinga kwanini Mwanahalisi wanaandika habari za upande mmoja? Bila ya kuwa na uthibitisho? Mambo haya yangefanywa na shigongo, siyo kubenea! Credibility ya mwanahalisi imeshuka sana!
Mkuu husomi kuwa upande wa pili umegoma kuongea?
 
Upande mmoja vipi wakati malasusa hata wanafamilia wanaolalamika hakuwajibu ujumbe!
Halafu kwani malasusa hajui kusoma au kuandika?
Anakaaje kimya kwenye tuhuma nzito kama hizi?si jitokeze aseme na yeye?
ATAKUWA NI MZINZI TU.
Haya endeleeni kutoa hukumu, ila jambo moja nina uhakika nalo ni hili!...
Hakuna hata mmoja wenu aliyeshuhudia tukio hili la "UZINZI" wa Askofu MALASUSA, wote mnashabikia tu uzushi wa akina SAED KUBENEA!
 
Mwenye macho haambiwi Tazama na Mwenye Masikio haambiwi Sikia iweje uchafuliwe na gazeti alafu ukae kimya
 
Una ushahidi au Porojo tu za akina KUBENEA na wenzie!
Haziwezi kuwa porojo na kwa ubaya wa hizo porojo,mtumishi wa kiroho akakaa kimya kiasi cha kutiliwa shaka kubwa.
Porojo hizi zina chembe chembe za ukweli ndani yake na ndiyo maana mchunga kondoo amekubali kuwa kimya ahukumiwe kwa namna yoyote ili YAISHE(YESHEEE)
 
Back
Top Bottom