KKK lawashambulia weusi kwa visu California

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,825
4,754
160228102525_kkk_california_624x351_bbc_nocredit.jpg


Watu watatu wamedungwa visu katika mapigano kati ya kundi linalowachukia watu weusi la Ku Klux Klan (KKK) na waandamanaji wanaowapinga katika jimbo la California.

Tukio hilo lilitokea karibu na eneo kulikopangwa mkutano wa hadhara wa wazungu wao wanachama wa KKK.

Watu wanne walitiwa mbaroni katika makabiliano hayo, akiwemo mwanachama mmoja wa KKK aliyemdunga mweusi kisu.

160228102604_kkk_california_624x351_bbc_nocredit.jpg


Msemaji wa polisi alieleza kuwa shida ilianza wakati wanachama wa KKK waliwasili katika uwanja wa Anaheim, karibu kilomita 50 Kusini Mashariki mwa Los Angeles, karibu na Disneyland.

Msemaji wa polisi alisema kuwa wanachama hao wa KKK walishambuliwa weusi walipokuwa wanatoka kwenye gari.

Mmoja aliangushwa chini.

Waandamanaji watatu wanaopinga KKK walidungwa visu katika makabiliano hayo.

160228102902_kkk_california_624x351_bbc_nocredit.jpg


Mtu mmoja aliyeshuhudia matukio hayo alisema kuwa wanachama wa KKK walikuwa wamelemewa.

Mmoja wa waliodungwa visu anaugua na amelazwa hospitalini


Chanzo: BBC
 
KKK psychologically wanaanza kuonesha kuzidiwa na Black people in America.

Racism! Kitu mbaya sana hii.
 
KKK psychologically wanaanza kuonesha kuzidiwa na Black people in America.

Racism! Kitu mbaya sana hii.

Wanazidiwa maana kuna wazungu/weupe wengi ambao wanachukia ubaguzi na wameungana na weusi dhidi ya hao wabaguzi.
Hizo picha hapo juu zinaonyesha wazungu waliobeba mabango dhidi ya KKK.

Hii ndio inafaa iwe taswira hata kwenye vita dhidi ya ugaidi, watu wasiishie tu kusema wanachukia ugaidi, lakini wahusike wote kabisa kwenye kupinga.
 
hata farao alitawala miaka mamia lakini siku ikafika utawala wao ukaangushwa. Sasa ni mida ya black kuwa juu ya wazungu. Hata trump naona ana wasiwasi sana na blacks.
 
Back
Top Bottom