Kizuri kula na wenzio

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
21,247
36,300
Habari zeinyuuu mabibi na mabwana wa MMU,

Poleni na hekaheka za kumaliza mwaka, maana mwisho wa mwaka una mambo wengine wanakesha kwa kufaha wengine wanajuta na kung'ata meno kwa huzuni kila mtu kutokana na tukio lake. Tuache hayo tufate yangu yaliyonileta hapa...............

Kama nilivotangulia kusema hapo juu, kizurii kula na mwenzio hasa ndugu yako, rafiki yako, bestito, swahiba, n.k. n.k.

Katika pilika pilika za kumaliza mwaka Kasie kaibuka na bingo, kuna dili moja imenidondokea yaani hadi raha, sikuwa nimeitegemea hata na dili yenyewe ilikuwa klini hivo na hela yake pia safi haina kweree hata Magu akileta oditi makaratasi meupeee kila kitu swaafee.

Nikasema kwasababu hii hela sikuwa nimeipangia wala kuitarajia wacha niitoe sadaka kiasi kwa Maulana, kisha kiasi nikaamua kuichangia serikali yangu (hapa naunga mkono jitihada za Magu) hivo nimelipia plate numbet ya kuweka jina langu na saa nikiendesha mtaani nasomeka KASINDE japo si Range Rover wala Prado New Model ni lile lile la siku zote ila sio ile bajaji hii ni ile ingine ndo inabandiko la KASINDE. Lakini mwaka ukiisha narudi kwenye plate number yangu maana nimelipia kwa hela ya dili looh!!

Sasa basi nikasema baada ya kuigawia serikali pesa yangu ya dili ambalo sikulitegemea kiasi kingine niwagaie wana MMU ambao ndo marafiki na maswahiba japo si wote, ila siwezi kurusha sandakalawe ntachezesha DRAW......

Iko hivi, popote utakapolikuta gari limebandikwa plate number ya KASINDE basi lipige picha kisha iweke hapa . Yule wa kwanza kutuma picha atajishindia Dola 100 za kimarekani yaani US $100.

Kisha kuanzia wa pili kuweka picha na wa tatu na wa nne kutuma picha wao watapata; wa pili dola za kimarekani 80 yaani US $80, wa tatu atapata dola 50 za kimarekani yaani US $50 na wa nne atapata dola 20 yaani US $20 pamoja na kupata ofa ya kuendeshwa na Kasinde town trip. Can be from nyumbani kwake to town kisha kumrudisha home.

NOTE ON TRIP: Awe anaishi Dar, au kama anaishi Mkoa nje ya Dar basi aje Dar ili apate kuzungushwa mjini akiendeshwa na Kasie. Trip haitahusisha mtu wa tatu (third party). Trip haitahusisha siku nzima ni asubuhi kukuchukua mahali ulipo na kukuacha unapoenda (could be kazini) kisha jioni Kasie anakupitia hapo au utakapokuwa na kukurudisha alipokutoa au utakapomwambia. (strictly iwe Dar na sio Pwani) Muda lazima uzingatiwe niko tayari kumchukua mlengwa kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa 4 asubuhi (hii ni kwa trip ya kumpeleka atakako). Muda wa kumrudisha atakako ni kuanzia saa 9 mchana hadi saa 2 usiku. Hii ni kuweza kunipa nafasi ya kujiandaa na misele yangu binafsi ya ku popo na kula ujana.

Kila la heri kaa tayari, kaa mkao wa kupokea dolari, weka kamera mkononi, popote upitapo kodolea plate number kisha tanga fotoo pwaaaah....!!! Ukiiweka hapa tutaimba wote Eeekootiteee Eeeekoootiteeeh............

Jinsi ya kupata dolari zenu kwa watakaoshinda ni kuni PM namba zenu za simu na nitawatumia kupitia aidha MPESA, TIGO PESA AU AIRTEL MONEY.


Najua kuna watakaosema badala ya ukipata hela usaidie watu unaipa serikali au uwekeze kwa faida yako ya baadae............. JIBU: Kawaambie walevi na mabazazi wanaohonga bia bar na kuwahonga vimada au serengeti boys wawekeze na waache kutapanya. Kasie sio mlevi wala mnywaji wala hana serengeti boys. Hela ya Kasie haina wa kumtegemea anakula yeye mwenyewe na ya baadae ipoo hivo hii ya sasa ni ka kutumia kadri inavokuja. (USIMUIGE UTAPASUKA MSAMBA!!!!)
Japo kuna wanaonichukia humu mie sina la kuwafanya zaidi ya kuwapa pole maana kila wakiona thread yako au mahali nime Quote wanakunja sura na kusonya, wengine wanatema na mate chini kabisaa, mie nawapa pole maana wanajipa presha za buree ilhali siwalishi siwavishi wala siwapunguzii pumzi (shangaa wanachukia nini) KASINDE anarudisha MALOVE kwao mara MIA ELFU.........Ndiooo *100,000.

Pesa ni matumizi haya yangu nayoni matumizi, Mipango nawaachia Manispaa....... Eeeekootitee

UPDATE: Photoshop hairuhusiwi wala picha ya kuchora hairuhusiwi. Wandugu kufanya hivi si kuwa nina shekeli za kumwaga lah nimejiskia kutoa kiasi ya nilichopata. KUTOA NI MOYO USAMBE UTAJIRI.
Usajili ulishakamilika tangu jumatatu hivo anytime wee twanga fotoo pwaaaah! !
Malipo yatafanyika in Tsh. kwa rate ya siku hiyo.

Kila la heri.

Nawatakia woooteee Heri na Fanaka ya Msimu huu wa Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya 2016.

Kasie.
 
Tupe uhakuka ? Sio tukodoe mimacho barabarani kumbe hata usajili bado, weka chochote kutuaminisha..
 
Gari lako hilo hapo..Naomba pesa yangu..Tusianze kusumbuana sasa
 

Attachments

  • DSC_9846.jpg
    DSC_9846.jpg
    323.1 KB · Views: 1,245
Kasinde kasinde!! Usijepiga picha wewe mwenyewe ukapost kwa Id nyingine ukase a kuna mtu kashinda?
 
USA baby:usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2:
 
USA baby:usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2:
Oooh nooh you are late.... The ship has just arrive....
 
That private registration costs more than your baby walker....u better get a second one! btw hio namba unakaa nayo zaidi ya mwaka mmoja
 
Back
Top Bottom