Uko wapi Eliza?

c h o l o

Member
Dec 9, 2023
92
156
Nawasalimu.
Juzi bhana nilikuwa naelekea kijijini kwa ajili ya shughuli ya kilimo baada ya kujipa likizo ktk kazi yangu ya kuuza matunda mjini. Wakati nikiwa katika moja ya usafiri wa kwenda bush nikiwa sina hili wala lile, alikuja abiria mmoja aliyeketi kando yangu.

Nilipokea salamu yake then nikamwangalia kama ishara ya mwitikio chanya wa salamu yake.
Aloo! Macho na moyo wangu vilipata shock kwa sekunde kadhaa baada ya kuiweka taswira ya mrembo Eliza kwenye mboni zangu💞.

Nikajifanya kama sina attention naye ili asijue taabu alonipa kwa muda ule. Akili ilivurugika, moyo ukadunda kwa kasi mnoooo. Nikajikuta naanza kuimagine mambo mengi, nikahisi nimeketi na mke wangu, nikawaza kila aina ya mawazo chanya juu yangu na mrembo yule.

Kwa mwonekano ni binti wa around 17 hadi 19 yrs, ngozi flan hv maji ya kunde ilokosa nuru kwa matunzo madogo, macho flan hv meupeeee, meno ya wastani yalopangiliwa vzr na mwenyezi Mungu, lips za kawaida na kamwili kake portable.

Nliamua kuvunja ukimya kwa kumsemesha angalau nisikie vocal cord yake inatoa toni gan ya sauti. Aloo, Eliza ana sauti kusema za ukweli. Tuliongea vingi sana wakati tukisubir abiria wajae angalau tuanze safar ya kuuacha mji, kwenda huko tulipozaliwa.

Kilichoniua zaidi ni vile Eliza ni mpenda utani sanaaaa, nikumuuliza swali atajibu kama hataki vile, then wakati natafakari jibu ataniangalia na kunipa jibu sahihi likiwa limepambwa na tabasamu flan hivi. ELIZA NI MZURI BWANA.

Baada ya kuzoeana nilimwomba namba, akanipa na kuniomba nifanye ku beep naye apate yangu.... sikufanya ajizi, nikachomoa Tablet yangu nlouziwa na mwalimu mmoja kwa bei ya mjini, maana simu ndogo haikuwa na laini. Nikasev namba ya Eliza.

Safar ilianza majira ya saa 6 mchana, tuliongea mengi sana na Eliza, hadi tulipomaliza kilomita 46 za safari. Hapo ulikuwa ni mwisho wa safari yangu, japo yeye alienda hadi mwisho wa gari. Nilishuka, nikashusha mifuko yangu 50 ya mbegu za kisasa, mbolea mifuko 7 na mazagazaga mengne kwa ajili ya kusongesha maisha kijijini.

Eliza alishuka akanikumbusha kuwa atanijulisha atakapofika aendapo. Niliagana nae akazama garini na kutokomea.

Mabibi na mabwana... Akili yangu yote haikuwa tena kwenye mamifuko ya mbegu na mbolea. Naweza sema Eliza aliondoka na akili yangu.

Nikampigia simu kumuuliza kama amefika au la!, ilihali gari bado niiona kwa macho ikisepa😁. Alicheka sana akinijibu kuwa ndo ashapokelewa na nduguze, kisha akanijibu kuwa bado hata hajafika. Nilikata simu na kurudisha mawazo yangu kwenye ubebaji wa mazagazaga yangu. Nlipata usafiri nikafika nilipokuwa naenda kufikia.

Baadae iliingia meseji kutoka kwa Eliza, ikisomeka hivi "Nimefika Salama baba angu". Nikapiga simu natukaongea kwa dk1 kisha akaniaga kuwa atanichek akimalza kujuliana hali na watu wa kwao. Niliendelea na ratiba zangu hadi saa 2 usiku. Sikuona ujumbe wala call kutoka kwa Eliza. Niliamua kumpigia simu. Huwez amini hakuwa akipatikana. Nilipiga sana simu hadi saa 5 za usiku bila mafanikio ya kumpata. Nikajipumzisha kwa imani kuwa atapatikana kesho. Haikuwa hivyo pia😥😥. Leo ni siku ya tatu Eliza hapatikani.

Nimejikuta naumia as if n mtu nilojuana nae toka long. Yote nilotaka kumweleza sijui ntamweleza nani.

UKO WAPI ELIZA??
20231210_201044.jpg
 
Si wanasema mnaotumia samsung mna akili nyingi, sasa mkuu we mbona kama kuna vi upungufu 😁

Miaka 17 aisee… fanyeni mambo kama vile hamna mayai, wahuni watafilimba na wako labda uzae kiume tupu.
 
Back
Top Bottom