Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza suala la bandari CCM kuzunguka nchi nzima

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Inashangazwa kuona nguvu kubwa inatumika kwa viongozi wa wilaya mikoa manaibu mawaziri na mawaziri wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm wakihaha huku na kule kuwahutubia wananchi waunge mkono sakata la bandari kupewa DP World ya Dubai.

Wahenga walishasema "Kizuri chajiuza ila kibaya chajitembeza". Usemi huu umethibitika kwenye sakata la bandari kwani CCM baada ya kugundua kuwa wananchi wanapinga mchakato wa bandari wameamua kujitembeza mitaani kuwahadaa wananchi ili wakubali uwekezaji ambao una mkataba wa hovyo.

Naamini mkataba wa bandari ungekuwa mzuri wenye tija kwa nchi na wananchi suala la bandari lingejiuza lenyewe bila CCM na viongozi wake kuzurura kuwashawishi wananchi.

Narudua tena suala la bandari wananchi tunataka mchakato uanze upya wenye nchi tushirikishwe.
 
Inashangazwa kuona nguvu kubwa inatumika kwa viongozi wa wilaya mikoa manaibu mawaziri na mawaziri wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm wakihaha huku na kule kuwahutubia wananchi waunge mkono sakata la bandari kupewa DP World ya Dubai.

Narudua tena suala la bandari wananchi tunataka mchakato uanze upya wenye nchi tushirikishwe.
Watanganyika tunasema hivi , hatudanganyiki tena
 
Wazunguke, ila wajibu hizo hoja...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Walitakiwa watangaze nia yao mapema ya kubinafsisha uendeshaji wa Bandari upya. Walipaswa waseme mapema TICTs wameshindwa na wanatafuta wawekezaji au wamempata DPW, badala yake wamefanya mambo kisirisiri mpaka wamefikia hapo walipo. Wamekurupushwa na kukamatiwa Unyagoni.Wameumbuka na ndoa yao ya mkeka.
Wanahangaika. Sasa wanawezaje kufanya marketing kitu ambacho wameshauza? Huo kama sio kujikanyaga unaita nini hilo?
Ulaghai? Kwani bunge lilifanya nini kama sio kusema"Wananchi wameridhia na kuukubali Mkataba"?

Wanachokipeleka huko ni nini kama sio kupoteza fedha za walipa kodi?
Mnawalazimisha wanachi sasa, Nawasubiri kwa hamu kuja na matokeo na mrejesho wa zoezi hilo.
 
Hawana imani na Wajumbe wa kikao cha Bunge kilichopitisha utumbo huu. Kweli CCM kumejaaa matope.
 
Back
Top Bottom