Kizungumkuti cha BRT

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,666
729,796
Tunaingia mwezi wa pili sana yaani February mradi hauanzi na mamlaka husika ziko kimya...!
Tatizo ninini?
Ufumbuzi wake ni upi?
Je, hii barabara ilikuwa ya mapambo?
Washika dau ni nani katika hili?
Tunachoshuhudia ni mradi wa notification Kwa traffic police kuwaumiza wananchi kwa sheria za barabara mpya ambazo ni tofauti na wanazozifahamu na hizo mpya hawajapewa elimu kupitia njia za kawaida za vyombo vya habari

Hivi hii nchi ikoje?
 
Afu mbona kama yale mabasi na vituo vilivyojengwa haviendani? basi zipo chini vituo vipo juu apo sijui walemavu wanaingiaje.
 
Afu mbona kama yale mabasi na vituo vilivyojengwa haviendani? basi zipo chini vituo vipo juu apo sijui walemavu wanaingiaje.
Nina mashaka mengi huu mradi tumeingizwa mjini..kuna faults nyingi sana ambazo zitakuja kujulikana utakapo anza kazi
Mpaka leo hii havijatolewa hata vipeperushi vinavyotoa elimu ya jinsi mradi utakavyofanya kazi
Michoro na maelezo ya Jinsi ya kupanda
Michoro na maelezo ya jinsi ya kushuka
Michoro na maelezo itokeapo dharura
Ulipaji wa nauli kwa mashine nknk
Hivi vitu havihitaji kusubiri mabus yawe barabarani ndio tuanze kufundishana. .haya yangefanyika sasa
 
Wameunda tume ya kuyachunguza je yanafaa au kuna harufu ya rushwa...

Baada ya hapo italetwa ripoti kamili hayafai na zabuni kurudiwa upya..

Kwa kipindi chote hicho hizo barabara zitakua parking...
 
Wameunda tume ya kuyachunguza je yanafaa au kuna harufu ya rushwa...

Baada ya hapo italetwa ripoti kamili hayafai na zabuni kurudiwa upya..

Kwa kipindi chote hicho hizo barabara zitakua parking...
Wawaachie wananchi wazitumie kwa muda basi wakati wanamaliza hizo figisu figisu zao
 
Huo mradi una uhusiano na UDA? Kama jibu ni ndiyo, huenda hiyo ikawa moja ya sababu, kwani hilo shirika la UDA halijulikani undani wake kama ni la umma au la binafsi kiujumla.
 
1455160510145.jpg
1455160498965.jpg
 
Back
Top Bottom