KIZOTA-Chumbani kuhesabu kura

KIZOTA-Chumbani kuhesabu kura

Kila uchaguzi CCM hugalagazwa, mkiambiwa nyie ni wezi wa kura mnabisha haya sasa, bisheni tena

Bujibuji, Aliyezoe kuiba hakikosa cha kuiba anajibia vya kwake mwenyewe , kweli CCM kazi kweli kweli
 
hivi mbona mnajiaibisha jamani,sasa uchaguzi wa CCM wewe unakuhusu nini,whether wameibiana kura ama la nyie inawahusu nini,fanyeni ya kwenu,mbona nyie mlituma wazee wakamuomba zito atoe jina la kugombea uenyekit hakuna aliesema neno,haaaa haaa haa haaaa mfyuuuuuuuuuuu
mbona nachekacheka ovyo? siyo unadhani kila mtu anataka akupige0713, wengine hatutumii...!
 
Even my youngest kid can not accept to be cheated to that extent of CCM chairman election results.
 
Mtu mkubwa chamani kama mimi,najitoa kwa Press Conference.Nitawaanika vya kutosha wezi nyinyi.Namalizia kukusanya nyaraka muhimu

Unataka kuuchekesha umma kweli. Wewe unaonekana si mtu wa mabadiliko na hata mfumo huo wa CCM kwako uliuona ni sawa tu ndiyo maana ukadumu huko kwa muda mrefu bila kukemea maovu yaliyokuwemo.Machungu/makovu ya uchaguzi ndiyo yanakusumbua. Ukipewa ulaji wewe hautapiga kelele.

Hakuna kutishia nyau, kama kweli uko serious na ulikuwa ndani ya system ya ufisadi maovu yote ya CCM unayajua, toka huko ueleze ukweli si kutishia nyau.
 
Duh hii ni kali. Aliye tabiri CCM itafia mikononi mwa JK sasa naanza kuamini
 
kabla sijajidiclose hebu kwanza ww jitangaze majina yako
pili mm sio mwanachadema bali mpenda mabadiliko ya kweli
tatu jina sio tija hapa kwa sasa
kianchohitajika ni uzalendo wa kweli na sio wizi wa kimadaraka.
50 years tunajivunia nini kama sio siasa za maji taka?
nadhani tunahitahi rais diktata mwenye uchungu na nchi
acha kujifurahisha wewe, huna upiganaji wowote. kama kweli wewe ni mpiganaji na huogopi chochote hebu anza kwanza kudisclose jina lako halisi. Hata baba yenu Slaa aliwahi kuahidi nchi haitatawalika eti mtaandamana hadi kieleweke. Mbona bado anatawala/
 
Acha unafki wewe unakimbilia kuleta uzushi humu.Wewe ni Chadema unapambisha hapa eti nataka kuamia upinzani
 
tokea jana niliwaambia jamaa niliokuwa nao...... Haya matokeo yamechakachuliwa haiwezekani yakawa kama yalivyotangazwa....bado mengi yatafumuliwa..................mwanahalisi: Mambo yote yangekuwa hadharani

Kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi ni mkakati maalum maana ndilo pekee lilikuwa na uthubutu wa kunusa habari kama hizi na kuzianika. Kwa sasa kuna ombwe kubwa kwenye tasnia ya habari.Tumebaki na habari za kuripoti na kupamba kambi za kisiasa kwenye vyama
 
This is rubbish. reveal yourself who you are if at all you are standing on truth. Otherwise, wewe ni mzushi tu kama akina Slaa walipozusha kuwepo kwa makontena ya kura mwaka 2010 wakaadhirika walipothibitishiwa uongo wao. wakazusha wanataka kuuawa walipoitwa polisi wakaeleze ili wawasaidie kuwalinda wakaleta habari za mwaka 2008. Tabia hii ni ya Pro Chadema ndiyo inayotawala mtandao huu wa JF na ni tabia mbaya kimsingi.

Watu wenye akili hawawezi kuamini silly arguments zilizoandikwa katika thread hii. ni aibu tupuuuuuuuuuu. Wala hamuoni ukweli kuhusu barabara zenye urefu wa km 11,000 za lami zinazojengwa kote Tanzania. Hamuoni nchi ilivyounganishwa kwa barabara zinazopitika kipindi cha mwaka mzima. Rais gani alipata mafanikio haya katika wakati wake? Nyerere aliishia kutupangisha foleni ya unga, sukari na mchele. Semeni yote. Sisi tunangoja mafanikio yenu kwenye halmashauri zinazoongozwa na Chadema ili tupime uwezo wenu wa kuongoza. UKWELI utabaki CCM imekomaa kidemokrasia kuliko chama chochote hapa nchini. Mmesahau kwamba CHADEMA haina kabisa mfumo wa kidemokrasia? au tuwakumbushe?
 
Ilikuwa balaa.Usalama wa Taifa waliingia na kuteka uhesabuji kura. Wakadai kuwa wametumwa kuilinda nchi na mipasuko. Lahaula! CCM imeshakuwa nchi tena? Sisi tuliokuwa na jukumu la kuhesabu kura tukapigwa vikumbo. Tukaonekana hatufai.Wakati huo,tulikuwa tumeshahesabu nusu ya kura za Mwenyekiti baada ya zile za Makamu wa Mwenyekiti wa Bara na Visiwani.

Si kweli kuwa Dr.Shein na Mangula walipata kura zote. Dr.Shein alikataliwa na wapiga-kura 43 huku Mangula akikataliwa na 50. Hawa hawakushinda kwa asilimia 100. Kwa zile za Uenyekiti,mchuano wa 'NDIYO' na 'HAPANA' ulikuwa mkali. Hapo ndipo Ndugu Mackson Chizii alipotoka chumba cha kuhesabia kura na kwenda kusikojulikana.Aliporudi,akarudi na Usalama wa Taifa na Green Guard.

Jana,nimeamini kuwa kura zinazotangazwa sizo zilizopigwa hasa. Ndugu zangu,kwa umafia tuliofanyiwa jana,itakuwa ngumu kwa upinzani kushinda Urais wa nchi hii kama wachache watakwenda sirini kuhesabu kura kisha kuzitangaza. Amini nawaambia,kura huibwa.Matokeo hugeuzwa.Na sisi CCM ndio mchezo wetu.Hatutaachia kirahisi ushindi kwa mwingine.

Iko haja kwa mfumo wa kuhesabu kura kurekebishwa.Ikiwezekana,na mgombea naye awepo pamoja na Wakala wake. Ni jana tu,JK alibadilishiwa matokeo ili ionekane ameshinda kwa asilimia 99.2. Kuanzia jana,nipo tayari kujiunga na upinzani ili tuikomboe nchi hii.Sijiungi kwakuwa namchukia JK,najiunga kwa kuchukia uibaji wa kura ambao unakandamiza demokrasia nchini.Tunaongozwa na tusiowachagua na tunachagua wasiotuongoza.Ni hatari!

Chanzo: Mimi mwenyewe niliyekuwa chumba cha kuhesabia kura Kizota chini ya uangalizi wa Spika Anne Semamba Makinda. Sina muda tena wa kuogopa. Hawa watu hawafai.

We kuiba kura za wenzako ulikuwa unaona raha tangu 1995! sasa kura zako zimeibwa unalia nini? mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binaadamu Mchungu ati? sasa ndio unataka kukomboa nchi! heri unyamaze na ufute kauli yako!
 
Mie nianza kuona mikakati hiyo mapema pale ilipotakiwa kila mkoa upige kura zake.

Kama mambo yasingeenda sawa na kufanikiwa kupika kura hizo. hiyo mikoa mibabe wangekiiona.
 
Ilikuwa balaa.Usalama wa Taifa waliingia na kuteka uhesabuji kura. Wakadai kuwa wametumwa kuilinda nchi na mipasuko. Lahaula! CCM imeshakuwa nchi tena? Sisi tuliokuwa na jukumu la kuhesabu kura tukapigwa vikumbo. Tukaonekana hatufai.Wakati huo,tulikuwa tumeshahesabu nusu ya kura za Mwenyekiti baada ya zile za Makamu wa Mwenyekiti wa Bara na Visiwani.

Si kweli kuwa Dr.Shein na Mangula walipata kura zote. Dr.Shein alikataliwa na wapiga-kura 43 huku Mangula akikataliwa na 50. Hawa hawakushinda kwa asilimia 100. Kwa zile za Uenyekiti,mchuano wa 'NDIYO' na 'HAPANA' ulikuwa mkali. Hapo ndipo Ndugu Mackson Chizii alipotoka chumba cha kuhesabia kura na kwenda kusikojulikana.Aliporudi,akarudi na Usalama wa Taifa na Green Guard.

Jana,nimeamini kuwa kura zinazotangazwa sizo zilizopigwa hasa. Ndugu zangu,kwa umafia tuliofanyiwa jana,itakuwa ngumu kwa upinzani kushinda Urais wa nchi hii kama wachache watakwenda sirini kuhesabu kura kisha kuzitangaza. Amini nawaambia,kura huibwa.Matokeo hugeuzwa.Na sisi CCM ndio mchezo wetu.Hatutaachia kirahisi ushindi kwa mwingine.

Iko haja kwa mfumo wa kuhesabu kura kurekebishwa.Ikiwezekana,na mgombea naye awepo pamoja na Wakala wake. Ni jana tu,JK alibadilishiwa matokeo ili ionekane ameshinda kwa asilimia 99.2. Kuanzia jana,nipo tayari kujiunga na upinzani ili tuikomboe nchi hii.Sijiungi kwakuwa namchukia JK,najiunga kwa kuchukia uibaji wa kura ambao unakandamiza demokrasia nchini.Tunaongozwa na tusiowachagua na tunachagua wasiotuongoza.Ni hatari!

Chanzo: Mimi mwenyewe niliyekuwa chumba cha kuhesabia kura Kizota chini ya uangalizi wa Spika Anne Semamba Makinda. Sina muda tena wa kuogopa. Hawa watu hawafai.

Hii ni sawa na kujificha macho ukidhani usiyemuona hakuoni kumbe wewe ndiye anayekuona ilhali wewe humuoni.

Hawa CCM hawa....time will tell. Time.
 
Yote yanawezekana!! Taarifa hii inaweza kuwa kweli ama inatoka kwa walioumizwa na huo uchaguzi.
 
Makatibu walivyosikia kila mkoa na kapu la kura walitetemeka juu ya mikoa yao..matokeo ya kupangwa haya ili mwenyekiti asidhalilishwe.
 
Binafsi sishangazwi na hizo mbinu chafu za ccm na suala la kumuamini au kutokumuamini mleta mada sitaki kuhangaika nalo, lililokuwa lanipa mashaka ni MANGULA kushinda kwa 100% maana kwa jinsi CCM ilivyo sasa na misimamo ya MANGULA sio rahisi kukubaliwa na pande mbili zinazokinzana, maana tukisema kapata 100% ina maana watoa rushwa na wasiotoa rushwa wote wanamkubali kitu ambacho si kweli.

Hongera kwa kuona mwanga mzee Tupatupa najua wapo wengi kama wewe ambao hawaamini mpaka washuhudie, MUNGU ni mkubwa ipo siku watajua na watakuwa tayari kujiunga na wanyonge wa NCHI hii katika kuililia.*

Hata Jah amempigia kura Mangula?
 
Hata Jah People amempigia kura Mangula?
 
Jamaa wanachakachua mpaka wanapotea njia, ushindi wa mwenyekiti ni asilimia 81.5% labda wana calculator za kichina, we waache iko siku watachakachua kama kawaida yao wataweka kura halali za Slaa pamoja na jina lake kwa mgombea wao na za mgombea wao na kula zake, ngoma wakati wa kutangaza
 
Back
Top Bottom