VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,006
Ilikuwa balaa.Usalama wa Taifa waliingia na kuteka uhesabuji kura. Wakadai kuwa wametumwa kuilinda nchi na mipasuko. Lahaula! CCM imeshakuwa nchi tena? Sisi tuliokuwa na jukumu la kuhesabu kura tukapigwa vikumbo. Tukaonekana hatufai.Wakati huo,tulikuwa tumeshahesabu nusu ya kura za Mwenyekiti baada ya zile za Makamu wa Mwenyekiti wa Bara na Visiwani.
Si kweli kuwa Dr.Shein na Mangula walipata kura zote. Dr.Shein alikataliwa na wapiga-kura 43 huku Mangula akikataliwa na 50. Hawa hawakushinda kwa asilimia 100. Kwa zile za Uenyekiti,mchuano wa 'NDIYO' na 'HAPANA' ulikuwa mkali. Hapo ndipo Ndugu Mackson Chizii alipotoka chumba cha kuhesabia kura na kwenda kusikojulikana.Aliporudi,akarudi na Usalama wa Taifa na Green Guard.
Jana,nimeamini kuwa kura zinazotangazwa sizo zilizopigwa hasa. Ndugu zangu,kwa umafia tuliofanyiwa jana,itakuwa ngumu kwa upinzani kushinda Urais wa nchi hii kama wachache watakwenda sirini kuhesabu kura kisha kuzitangaza. Amini nawaambia,kura huibwa.Matokeo hugeuzwa.Na sisi CCM ndio mchezo wetu.Hatutaachia kirahisi ushindi kwa mwingine.
Iko haja kwa mfumo wa kuhesabu kura kurekebishwa.Ikiwezekana,na mgombea naye awepo pamoja na Wakala wake. Ni jana tu,JK alibadilishiwa matokeo ili ionekane ameshinda kwa asilimia 99.2. Kuanzia jana,nipo tayari kujiunga na upinzani ili tuikomboe nchi hii.Sijiungi kwakuwa namchukia JK,najiunga kwa kuchukia uibaji wa kura ambao unakandamiza demokrasia nchini.Tunaongozwa na tusiowachagua na tunachagua wasiotuongoza.Ni hatari!
Chanzo: Mimi mwenyewe niliyekuwa chumba cha kuhesabia kura Kizota chini ya uangalizi wa Spika Anne Semamba Makinda. Sina muda tena wa kuogopa. Hawa watu hawafai.
Mzee Tupatupa wa Lumumba