KIZOTA-Chumbani kuhesabu kura

KIZOTA-Chumbani kuhesabu kura

weka picha!!

[h=2]KIKWETE MWENYEKITI TENA CCM, MANGULA, DK, SHEIN MAKAMU WAKE[/h]Tuesday, November 13, 2012

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Makamu wenyeviti wawili, Spika wa Bunge Anna Makinda, baada ya kumtangaza kushinda nafasi hiyo ya Uenyekiti, katika uchaguzi uliofanyika hivi punde katika ukumbi wa Kizota, Dodoma, ikiwa ni kuhitimisha shughuli za Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM. Wapili Kulia ni Makamu Mwenyekiti Mpya wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dk. Moahamed Gharib Bilal
Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Jakaya Kikwete na Makamu wake wawili Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (Zanzibar) na Philip Mangula (Bara) wakiwa meza kuu baada ya kutangazwa kushika nyandhifa zao.
Wajumbe wakiserebuka baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangazwa kuwa mshindi wa Uenyekiti wa CCM, Taifa.
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akiongoza kikao baada ya kushinda tena kiti hicho. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phili Mangula.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

POSTED BY CCM BLOG AT 10:45 AM 0 COMMENTS EMAIL THISBLOGTHIS!SHARE TO TWITTERSHARE TO FACEBOOK

[h=2]RAIS JAKAYA KIKWETE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CCM[/h]

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM kwa kura 2395 kati ya 2937 zilizopigwa ambazo ni sawa na asilimia 99.92%

POSTED BY CCM BLOG AT 10:20 AM 0 COMMENTS EMAIL THISBLOGTHIS!SHARE TO TWITTERSHARE TO FACEBOOK

[h=2]MATOKEO YA NAFASI YA UMAKAMU MWENYEKITI BARA NA VISIWANI YATANGAZWA RASMI[/h]

[h=3]Matokeo ya nafasi za makamu mwenyekiti Zanzibar na Tanzania Bara yatangwazwa rasmi,ambapo hakuna kura iliyoharibika hivyo wamepita kwa asilimia 100%.
Dr. Ali Mohamed Shein ,Rais wa Zanzibar amepita kwa idadi ya kura 2397 na hakukuwa na kura za hapana, hivyo kutangazwa rasmi kuwa ndio Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,wakati huo huo Philip Mangula amechaguliwa kwa kura 2397, hakuna zilizoharibika ,hivyo Mh. Mangula ndio Makamu Mwenyekiti mpya kwa upande wa Tanzania Bara[/h]

CCM Blog
 
Mzee Tupatupa,

Huu uongo wako naona ni very advanced. Hapo chini ulipost bandiko lako ukijinadi kwamba wewe ni mamluki ndani ya CCM ukifanyia kazi mabosi wako wanaokulipa walio nje ya chama. Sasa leo umekuja unajidai ulikuwa mkereketwa wa chama kabla ya mkutano mkuu unajitoa kwa sababu za wizi wa kura loo! kweli njia ya muongo ni fupi tumekukamata.
Next time ukumbuke kwamba ukitaka kuwa mwongo uwe na kumbukumbu nzuri usichanganye madawa.Ona sasa mzee mzima ushaumbuka.

Mkuu, hongera kwa kumgundua huyu mwongo mkubwa nayekuja humu kuwafanya watu wajinga.
Ingekuwa vyema MODS wamshughulikie.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM kwa kura 2395 kati ya 2937 zilizopigwa yaaani wajumbe 542 hawamuhitaji.

Wakati huo
Dr. Ali Mohamed Shein ,Rais wa Zanzibar amepita kwa idadi ya kura 2397 na hakukuwa na kura za hapana, hivyo kutangazwa rasmi kuwa ndio Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Philip Mangula amechaguliwa kwa kura 2397, hakuna zilizoharibika ,hivyo Mh. Mangula ndio Makamu Mwenyekiti mpya kwa upande wa Tanzania Bara.

Tafisri yake ni nini kwa JK pale Makamu mwenyekiti anapopita kwa kura zote na Mwenyekiti kupoteza kura zaidi ya miatano?? . Haoni bado hakubaliki??

[TABLE="width: 64"]
[TR]
[TD="class: xl63, width: 64, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Uchaguzi wa CCM is AN ABSURD STUPIDITY, Halafu eti katika huo mkutano mkuu walikuwemo maprofessor (Sio akina Maji Marefu).

I agree! Even the sudden change of voting modality was a breach of democracy.

Ain't it ironic no professor had the guts to question it let alone notice that it was not right. It reminds me of the ousting of Mbeki.

Imagine citizens of South Africa voted for Mbeki to become president ironically only a bunch of few ANC NEC members drafted a letter to demand President Mbeki resignation

That was a coup! That wasn't democracy. Where were the so called professors to question that?

It's high time we learned to think for ourselves instead of entrusting others to think for us.
 
Ilikuwa balaa.Usalama wa Taifa waliingia na kuteka uhesabuji kura. Wakadai kuwa wametumwa kuilinda nchi na mipasuko. Lahaula! CCM imeshakuwa nchi tena? Sisi tuliokuwa na jukumu la kuhesabu kura tukapigwa vikumbo. Tukaonekana hatufai.Wakati huo,tulikuwa tumeshahesabu nusu ya kura za Mwenyekiti baada ya zile za Makamu wa Mwenyekiti wa Bara na Visiwani.

Si kweli kuwa Dr.Shein na Mangula walipata kura zote. Dr.Shein alikataliwa na wapiga-kura 43 huku Mangula akikataliwa na 50. Hawa hawakushinda kwa asilimia 100. Kwa zile za Uenyekiti,mchuano wa 'NDIYO' na 'HAPANA' ulikuwa mkali. Hapo ndipo Ndugu Mackson Chizii alipotoka chumba cha kuhesabia kura na kwenda kusikojulikana.Aliporudi,akarudi na Usalama wa Taifa na Green Guard.

Jana,nimeamini kuwa kura zinazotangazwa sizo zilizopigwa hasa. Ndugu zangu,kwa umafia tuliofanyiwa jana,itakuwa ngumu kwa upinzani kushinda Urais wa nchi hii kama wachache watakwenda sirini kuhesabu kura kisha kuzitangaza. Amini nawaambia,kura huibwa.Matokeo hugeuzwa.Na sisi CCM ndio mchezo wetu.Hatutaachia kirahisi ushindi kwa mwingine.

Iko haja kwa mfumo wa kuhesabu kura kurekebishwa.Ikiwezekana,na mgombea naye awepo pamoja na Wakala wake. Ni jana tu,JK alibadilishiwa matokeo ili ionekane ameshinda kwa asilimia 99.2. Kuanzia jana,nipo tayari kujiunga na upinzani ili tuikomboe nchi hii.Sijiungi kwakuwa namchukia JK,najiunga kwa kuchukia uibaji wa kura ambao unakandamiza demokrasia nchini.Tunaongozwa na tusiowachagua na tunachagua wasiotuongoza.Ni hatari!

Chanzo: Mimi mwenyewe niliyekuwa chumba cha kuhesabia kura Kizota chini ya uangalizi wa Spika Anne Semamba Makinda. Sina muda tena wa kuogopa. Hawa watu hawafai.

Kama kweli JF ina "Great Thinkers", tuone hapa mna-comment nini?? Kwa mtu mwenye akili zake timamu kabisa, ushindi huu unatia shaka: 99.92% 100% 100%?????????? katika watu 2000???? Na ikiwa mtoa mada analolisema ni la kweli basi watanzania tujiandae na janga la kitaifa katika miaka mitano ijayo. Hicho ndicho chama tawala halafu kinakuwa na utapeli wa ndani kwa ndani huku nje itakuwaje???? Huyu Makinda amekosa uzoefu wa kuchakachua akataka ajipendekeze kwa jk kumbe anaanika uchakachuaji wa kura. Ushindi huo kwa ccm ya leo haiwezekani hata kwa namna gani, na ukichukulia kulikuwa pia na upinzani uliojionyesha wazi kwa njia ya vipeperushi. Wakawadanganye watoto wadogo. Ngoja tusubiri tuone ndege inavyopaa
 
Ilikuwa balaa.Usalama wa Taifa waliingia na kuteka uhesabuji kura. Wakadai kuwa wametumwa kuilinda nchi na mipasuko. Lahaula! CCM imeshakuwa nchi tena? Sisi tuliokuwa na jukumu la kuhesabu kura tukapigwa vikumbo. Tukaonekana hatufai.Wakati huo,tulikuwa tumeshahesabu nusu ya kura za Mwenyekiti baada ya zile za Makamu wa Mwenyekiti wa Bara na Visiwani.

Si kweli kuwa Dr.Shein na Mangula walipata kura zote. Dr.Shein alikataliwa na wapiga-kura 43 huku Mangula akikataliwa na 50. Hawa hawakushinda kwa asilimia 100. Kwa zile za Uenyekiti,mchuano wa 'NDIYO' na 'HAPANA' ulikuwa mkali. Hapo ndipo Ndugu Mackson Chizii alipotoka chumba cha kuhesabia kura na kwenda kusikojulikana.Aliporudi,akarudi na Usalama wa Taifa na Green Guard.

Jana,nimeamini kuwa kura zinazotangazwa sizo zilizopigwa hasa. Ndugu zangu,kwa umafia tuliofanyiwa jana,itakuwa ngumu kwa upinzani kushinda Urais wa nchi hii kama wachache watakwenda sirini kuhesabu kura kisha kuzitangaza. Amini nawaambia,kura huibwa.Matokeo hugeuzwa.Na sisi CCM ndio mchezo wetu.Hatutaachia kirahisi ushindi kwa mwingine.

Iko haja kwa mfumo wa kuhesabu kura kurekebishwa.Ikiwezekana,na mgombea naye awepo pamoja na Wakala wake. Ni jana tu,JK alibadilishiwa matokeo ili ionekane ameshinda kwa asilimia 99.2. Kuanzia jana,nipo tayari kujiunga na upinzani ili tuikomboe nchi hii.Sijiungi kwakuwa namchukia JK,najiunga kwa kuchukia uibaji wa kura ambao unakandamiza demokrasia nchini.Tunaongozwa na tusiowachagua na tunachagua wasiotuongoza.Ni hatari!

Chanzo: Mimi mwenyewe niliyekuwa chumba cha kuhesabia kura Kizota chini ya uangalizi wa Spika Anne Semamba Makinda. Sina muda tena wa kuogopa. Hawa watu hawafai.
Acha kutuzuga dogo. Kwani wakati Dr. Slaa analalamikia usalama wa taifa kuchakachua kura za uraisi 2010, wewe ulikuwa TLP?
 
Hawawezi kuleta electronic voting itawaumbua ngoja tuone uchaguzi wa kenya kwanza itakavyokuwa.
 
Uchaguzi wa CCM is AN ABSURD
STUPIDITY, Halafu eti katika huo mkutano mkuu walikuwemo maprofessor
(Sio akina Maji Marefu).

I bet my neck, hata leo Mbinguni Mwenyezi Mungu akiitisha uchaguzi, I'm
sure 100% hawezi kupata KURA ZA KISHINDO za 100% Kama Mangula na Shein,
unless kwa CCM Mangula na Shein kwao ni zaidi ya Mungu. BTW ndiyo maana
yule Malaika Mkuu LUCIFER alimuasi Mungu.

Hata mimi leo nikiitisha uchaguzi nyumbani kwangu KURA za SIRI in the
real sense ya SIRI siwezi kupata kura 100% that is a plain truth,
sembuse watu > 2,000.

Matokeo ya uchaguzi wa mkutano mkuu wa CCM is MOCKERY of democracy.

Cheyo aliwahi kulalamika kwamba CCM ni mabingwa wa kuiba kura, kwani
hata katika kituo alichopiga kura yeye (Cheyo) alipata kura 0 watu
wakamucheka. Lakini UKWELI ndiyo huo.
CCM haijawahi kufanya uchaguzi wa
HURU NA HAKI.
Penye red mkuu hii ni kali ccm nambari wani!!
 
Mbona husemi kama na kura za Rais Kikwete zilikuwa za kuchakachua?
 
Duh hapo nimekubali yaishe,kumbe ndio mpango mzima wa magamba?lakini mzee tupatupa tumekuwa tukilalamika sana juu ya wizi wa kura lakini hamkutuelewa wala kutusikiliza,anyway nashukuru kama ni kweli tametokea hayo na umeyashuhudia basi chukua hatua stahiki za kuungana na makamanda kuikomboa nchi.
 
actually I BELEAVE YOU.ule haukuwa uchaguzi bali ulikuwa uteuzi.hakukuwa na umuhimu wa kuchakachua kura maana matokeo halali yangewasaidia kujenga chama kwa kuweka watu wanaokubalika,unlike what they have done.
 
Pole sana Mzee Tupatupa ingawa ni kama ulichelewa sana kutambua wizi kura na mapinduzi ya matokeo kwa chaguzi zote za ccm. Na kwa anayetaka picha, au uhalali wako kama chanzo, namshauri aipotezee hii thread. Lakini ukweli ndo huo. Haiwezekani kundi lote hilo likakupenda lote, ni logic ya kawaida tu hii wala haihitaji darasa! Nakubali kuwa hizo kura 100% ni feki kama kawaida yao.
 
unakumbuka shuka kumekucha pole mzee tupatupa na utatupa kweli kula yako.
 
Duh hapo nimekubali yaishe,kumbe ndio mpango mzima wa magamba?lakini mzee tupatupa tumekuwa tukilalamika sana juu ya wizi wa kura lakini hamkutuelewa wala kutusikiliza,anyway nashukuru kama ni kweli tametokea hayo na umeyashuhudia basi chukua hatua stahiki za kuungana na makamanda kuikomboa nchi.

Kuikomboa nchi au familia zenu? Hakuna kiongozi wa kweli kutoka CDM mwenye sura halisi ya kiukombozi ni genge la wasanii fulani wanaotafuta fedha kama wale madiwani wa Moshi waliojipangia safari ya mamilioni kwenda Rwanda eti Kujifunza.
 
Wala wewe siyo mwanaccm kabisa huo ni ujanja ujanja tuu wa kurubuni watu kama mlivyozoea. Waliokuwa wanahesabu kura ni wanafunzi wa chuo na wala sii wewe. Na kama ni hivyo kama unavyodai iweje usilalamike kwenye vyombo husika vya vyama? YOU ARE NOT A GREAT THINKER. Wewe ni mtupatupa thread tuu.
 
Ama kweli ulimwengu una majaabu, hata mi niliposikia mambo ya asilimia 100 sikuamini its impossible kuchaguliwa kwa ushindi wa aina hiyo, its a shame and farce, but its better I shut my mouth.

  • :shut-mouth:
 
Kuikomboa nchi au familia zenu? Hakuna kiongozi wa kweli kutoka CDM mwenye sura halisi ya kiukombozi ni genge la wasanii fulani wanaotafuta fedha kama wale madiwani wa Moshi waliojipangia safari ya mamilioni kwenda Rwanda eti Kujifunza.
Kwa u great thinker wako unadhani tufanyeje?unataka kutuaminisha kwamba hao magamba wako tuwaache waendelee?
 
Back
Top Bottom