Kizazi kipya kinaelimika zaidi lakini kimeharibika zaidi. Je, tatizo ni Elimu au Malezi?

Kizazi kipya kinaelimika zaidi lakini kimeharibika zaidi. Je, tatizo ni Elimu au Malezi?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,152
Reaction score
1,696
Leo hii tuna vijana wengi waliomaliza shule, wana vyeti, wanaweza kutumia mitandao kwa ufasaha—lakini nidhamu iko chini, maadili yameporomoka, na heshima kwa wazazi au jamii haipo kama zamani.

Je, tatizo ni mfumo wa elimu unaotoa maarifa bila malezi? Au ni familia zinazokimbizana na maisha hadi kushindwa kulea watoto? Au labda teknolojia ndiyo inaua maadili kwa kasi?

Tunajenga taifa la watu wenye elimu lakini wasioweza kuishi kwa heshima na maadili ya msingi. Hili linaweza kuathiri taifa miaka michache ijayo kuliko tunavyodhani.

Je, suluhisho ni kurudi kwenye misingi ya mila? Marekebisho ya mfumo wa elimu? Au kutafuta njia mpya kabisa ya kulea kizazi hiki cha kidijitali?
 
Elimu pana ajabu, elimu pekee ya kujenga maadili na nidhamu ni elimu ya dini na utamaduni hizi nyingine za kuongea kingereza na kukariri mizingo ya duara hazina msaada wowote katika maadili na nidhamu
 
Nimetumiwa clip wale sijui shule gani hiyo,ila ukutani kuna mahali imeandikwa saa100 dome blah blah
Watoto wanakatika hadi kuonesha matiti,watoto shule naona walipelekewa singeli
Nawapa pole wazaz wa watoto zao hao maana nna imani wakipimwa marinda lazima yatakuwa yamefumuliwa pia
Naskkia waziri gwajima analifuatilia hilo suala+shule hiyo
Hata hivyo naona kama anajisumbua tu angeaachana nao maana ndy maisha waliyochagua na mfumo uliyopo unaahnga mkono hali hiii

Ova
 
Back
Top Bottom