Kuna knowledge gap hujaiona hapo. Usipokuwa makini nayo unaweza kusema watu wana chuki kumbe sio bali ni mirengo/sides tuu waliyonayo watu. Na hii ni kawaida kwa binadamu, roho/nafsi zetu zimeundwa zikiwa na no&yes au positive&negative sides.
Analysis yako umeifanya kwenye yanayoendelea kwenye social networks, ambapo kwa nchi za Kiafrika ni vitu vigeni na watu wengi saikolojia zetu(Waafrika) hazijajengwa kuhandle consequences za maoni ya mtandaoni.
Hata wazungu pia wapo ambao huwa yanawashinda na wanafikiaga kufuta kabisa pages zao za social networks ili wasiathiriwe na maoni hasi toka kwa followers walio mrengo tofauti na wao.
Mifano
Ukiingia kwenye pages za Trump, utakutana na lundo la matusi ya nguoni yanayoelekezwa kwake.
Ukienda kwenye pages za Obama, utakutana na utitiri wa watu wakimporomoshea kashfa na matusi kedekede.
Ingia pages za Ronaldo, Messi, Neymar, Mmbape, Salah, De Bruyne n.k utakutana na negativities kadha wa kadha zikiwaendea kila siku.
Tembelea pages za akina P Didy, Jay Z, Eminem, Drake, Rihanna, Beyonce n.k ni mwendo ule ule wa kushushiwa matusi na vichambo heavy kutoka kwa watu wasiowajua.
Sasa jiulize kinachofanyika hapa nchini mwetu kina tofauti na wenzetu?
Jibu ni hamna tofauti.
Sasa tatizo liko wapi?
Tatizo liko kwa hao wanaopelekewa hayo maneno. Wanashindwa kuhandle hayo maneno wanayopelekewa.
Kivipi?
Mwanasiasa unasoma comments hasa za negativities zinazokuhusu mitandaoni unazibeba na kuanza kupambana nazo kwa kutokujua kwamba hizo ni normal human behaviors, sio kwamba wanakuchukia wewe in person bali ni kwa sababu tuu upo mrengo fulani ambao ni tofauti na wao.
Msanii unatukanwa mitandaoni kwamba umetoa wimbo mbayaaa, na wewe usivyo na akili unabeba hizo comments kwamba may be kweli umeboronga. Kumbe nyuma ya pazia wamekuponda kwa kuwa tuu wao ni team Kiba na wewe ndio Diamond ambaye ni No. 1 rival wa Kiba. Hao wanaokuponda nyuma ya keyboard utakuta mbele ya keyboards zao wamefungulia sabufa kwa sauti nene wakienjoy nyimbo zako.
Au unakuta watu wanamponda Samata, ukichukulia kiwepesi wepesi utasema hawa watu sio wazalendo maana Samata katutoa kimasomaso na anaiwakilisha nchi vyema kunako mpira wa majuu. Lakini kumbe inawezekana wanaomponda ni kwa sababu tuu Samata alitokea Simba na wao ni Yanga. Wanajilaumu kwa nini Samata hakutokea kwao wanayanga. Ukienda majumbani mwao utawakuta hawakosi kuangalia mechi za Aston Villa ili wamshuhudie Samata wetu anavyolisakata kabumbu.
Hivyo ndivyo ilivyo.
Nini kifanyike?
Icon wa taifa, viongozi na wananchi kwa ujumla wafundishwe faida na hasara za social networks. Wafundishwe namna ya kuhandle haya mambo in a positive way.
Siku zote binadamu ana yes/no, positive/negative, east/west, north/south. Huwezi kulazimisha watu wote wawe mrengo mmoja ulioko wewe, hiyo siyo nature ya binadamu.
Kinachosikitisha zaidi hiki kitu kimeingia mpaka kwa viongozi wakubwa wa nchi. Wanashindwa kabisa kuhandle hizi mambo, wanashindwa kabisa kujua kwamba these are normal human behaviors na sio kwamba watu wana chuki bali ni mirengo/sides tuu ambazo mioyo yao imependa kuwa huko.
Ukiwa kiongozi na ukashindwa kujua haya utaishia kugombana na watu wako kila siku na ukitumia mabavu utajikuta unaumiza raia wako bure kwa kutojua small issues kama hizi.
Social medias ni zimwi kali mnoo ambalo wazungu wamelileta. Wao walishalitengenezea dawa na wala haliwasumbui, ila huku kwetu ni majanga, tusipoangalia litatutafunia na kutuulia umoja na mshikamano wa nchi zetu, mwishowe tutarudi kutawaliwa kirahisi sana.
Unforgetable