Kizazi kilichojaa chuki, wivu na sononi

Kizazi kilichojaa chuki, wivu na sononi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,266
Reaction score
871,811
Unaweza kushangaa ama kuumizwa na yanayoendelea Tanzania na nje ya mipaka yake. CHUKI iliyopitiliza kwenye lolote kwenye chochote. Jamii imeathirika na kuathiriwa. Sio siasa sio awamu ni kizazi tulichonacho. Pamoja na kwamba siasa zinaweza kuwa kichokoo lakini nyakati ndio kiasili na msingi. Tunahitaji uono mpana nje ya mipaka ya tafakuri kulitambua hili.

A generation full of hatred, envy and frustrations / stress. Tunaishi kizazi cha washindwa. Kizazi cha msongo mkubwa wa mawazo. Kizazi cha vurugu za kimaono, kuchanganyikiwa na kukata tamaa. Kizazi cha kutaka short cut! Na usidhani ni vijana ama ni umri. La hasha. Ni kizazi kilichowazoa mpaka viongozi na waheshimiwa ambao kwa makosa makubwa kabisa wamekabidhiwa dhamana ya kuongoza!!!

Kizazi hiki cha chuki kinaenda kwa madaraja. Kuanzia kwenye social media mpaka kwenye duru za uongozi wa nchi siasa na usalama. Tunaziishi nyakati.

Nyakati ambazo unapokuwa na mtazamo tofauti na wengine wewe ni adui. Nyakati ambazo unapokuwa na kitu cha ziada kuwazidi wengine wewe ni mjuaji.

Nyakati ambazo unapotumia muda wako mwingi kwa jamii unaambiwa kuna kitu unatafuta. Madaraka, sifa au cheo.

Mitandoni tunawaona wapondaji wa watanzania wenzetu waliofanikiwa kutoka kimaisha nchini na kimataifa.

Wapondaji wa Hasheem Thabit. Mcheza kikapu Ulaya
Wapondaji wa Mbwana Samatta. Mcheza kabumbu Ulaya
Wapondaji wa Diamond. Msanii wa muziki aliyetutoa kimasomaso Tanzania.

Ukija kuwaaangalia wote ni kapuku wasiomiliki chochote cha maana. Ni washindwa!

Achana na hao njoo kwa wanasiasa washindwa waliojawa na fukuto la chuki. Ona wanavyotangaza kiama cha mauaji kwa wale wanaotofautiana nao kimtazamo. Unabaki na mshangao

Chuki za mafanikio kwa wengine. Chuki za tofauti kimtazamo ndo gumzo maarufu nyakati hizi.
Mbaya zaidi nobody cares. Iwe kiongozi wa kidini.
Iwe kiongozi wa kisiasa
Ama iwe kiongozi kwa taaluma.
Hata mitandoni hakuna restrictions. Yoyote anaweza kusema chochote kwa yoyote ni chuki chuki chuki.

Hatushangilii ushindi wa wengine. Hatushangilii kupata kwa wengine. Hatushangilii mafanikio ya wengine.
Wakipigika na kufanya jitihada za mafanikio na kupata zaidi hatusemi kitu. Wakifanikiwa tunawaponda mwanzo mwisho!! Heri kukutana na mchawi kuliko mshindwa anayedhani kushindwa kwake kuna mkono wako.

Hali hii imesababisha kuwafanya wazawa kuwa tayari kuwasaidia wageni wakuja kuliko kumsaidia poti. Hali hii imesababisha hata wazawa kushindwa kutambulishana huko ughaibuni. Wako wako tayari kuukana utaifa wao ili tu wasijulikane wao ni akina nani.

Ukiona kuna haters ndani ya JF usiwalaumu wala kuwachukia. Hawa ni sehemu ya wale washindwa wengine huko kwingine kote. Unachoweza kufanya ni mawili aidha kuwapotezea mazima AMA kuwaelimisha kwa weledi!? lakini je mshindwa ni mtu wa kuelimishwa? Changamoto iko hapa...!!!!

Jr™️
 
Nyakati ambazo unapokuwa na mtazamo tofauti na wengine wewe ni adui....
Nyakati ambazo unapokuwa na kitu cha ziada kuwazidi wengine wewe ni mjuaji
Nyakati ambazo unapotumia muda wako mwingi kwa jamii unaambiwa kuna kitu unatafuta.. Madaraka, sifa au cheo...
Ungeishia hapa tu mkubwa maana pamebeba meseji tosha
 
Sio mada ya kisiasa
Asilimia kubwa ni wapinzani hasa vijana waliokimbia shule au kukosa cha kufanya wanaamini kujaa roho za chuki dhidi ya wengine walifanikiwa kutawafanya watoke.wanafikili wakiichukia serkali watapata ahueni kumbe maisha ndio vita ya mmoja mmoja


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr[emoji769]
 
Asilimia kubwa ni wapinzani hasa vijana waliokimbia shule au kukosa cha kufanya wanaamini kujaa roho za chuki dhidi ya wengine walifanikiwa kutawafanya watoke.wanafikili wakiichukia serkali watapata ahueni kumbe maisha ndio vita ya mmoja mmoja


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Naogopa kuzisoma changizo zako. Nadhani ungepewa jembe ungewamaliza wapinzani tena kwa siku moja tu. Kuumaliza upinzani si kuuchukia bali kuukubali
 
Lakini mkubwa mshana hivi hakuana njia ya kufanya zindiko maalum la kuwabadili mindset hawa watu wa type hii maana wanawaumiza sana watu halafu nahisi hawapo tu Africa maana ukiusikiliza wimbo wa God's plan wa Drake utagundua hata kule US watu wa aina hii bado wapo sana
 
Unaweza kushangaa ama kuumizwa na yanayoendelea Tanzania na nje ya mipaka yake.... CHUKI iliyopitiliza kwenye lolote kwenye chochote... Jamii imeathirika na kuathiriwa... Sio siasa sio awamu ni kizazi tulichonacho.... Pamoja na kwamba siasa zinaweza kuwa kichokoo lakini nyakati ndio kiasili na msingi.. Tunahitaji uono mpana nje ya mipaka ya tafakuri kulitambua hili

A generation full of hatred, envy and frustrations / stress... Tunaishi kizazi cha washindwa... Kizazi cha msongo mkubwa wa mawazo... Kizazi cha vurugu za kimaono, kuchanganyikiwa na kukata tamaa... Kizazi cha kutaka short cut..!!! Na usidhani ni vijana ama ni umri... La hasha... Ni kizazi kilichowazoa mpaka viongozi na waheshimiwa ambao kwa makosa makubwa kabisa wamekabidhiwa dhamana ya kuongoza!!!

Kizazi hiki cha chuki kinaenda kwa madaraja... Kuanzia kwenye social media mpaka kwenye duru za uongozi wa nchi siasa na usalama.... Tunaziishi nyakati.. Nyakati ambazo unapokuwa na mtazamo tofauti na wengine wewe ni adui....
Nyakati ambazo unapokuwa na kitu cha ziada kuwazidi wengine wewe ni mjuaji
Nyakati ambazo unapotumia muda wako mwingi kwa jamii unaambiwa kuna kitu unatafuta.. Madaraka, sifa au cheo...

Mitandoni tunawaona wapondaji wa watanzania wenzetu waliofanikiwa kutoka kimaisha nchini na kimataifa..
Wapondaji wa Hasheem thabit... Mcheza kikapu ulaya
Wapondaji wa Mbwana Samata.. Mcheza kabumbu Ulaya
Wapondaji wa Diamond.. Msanii wa muziki aliyetutoa kimasomaso Tanzania..
Ukija kuwaaangalia wote ni kapuku wasiomiliki chochote cha maana.. Ni washindwa!
Achana na hao njoo kwa wanasiasa washindwa waliojawa na fukuto la chuki... Ona wanavyotangaza kiama cha mauaji kwa wale wanaotofautiana nao kimtazamo.. Unabaki na mshangao
Chuki za mafanikio kwa wengine.. Chuki za tofauti kimtazamo ndo gumzo maarufu nyakati hizi ....
Mbaya zaidi nobody cares.. Iwe kiongozi wa kidini..
Iwe kiongozi wa kisiasa
Ama iwe kiongozi kwa taaluma...
Hata mitandoni hakuna restrictions.. Yoyote anaweza kusema chochote kwa yoyote ni chuki chuki chuki..

Hatushangilii ushindi wa wengine.. Hatushangilii kupata kwa wengine... Hatushangilii mafanikio ya wengine.. Wakipigika na kufanya jitihada za mafanikio na kupata zaidi hatusemi kitu.. Wakifanikiwa tunawaponda mwanzo mwisho...!!! Heri kukutana na mchawi kuliko mshindwa anayedhani kushindwa kwake kuna mkono wako...

Hali hii imesababisha kuwafanya wazawa kuwa tayari kuwasaidia wageni wakuja kuliko kumsaidia poti... Hali hii imesababisha hata wazawa kushindwa kutambulishana huko ughaibuni.. Wako wako tayari kuukana utaifa wao ili tu wasijulikane wao ni akina nani...

Ukiona kuna haters ndani ya JF usiwalaumu wala kuwachukia.. Hawa ni sehemu ya wale washindwa wengine huko kwingine kote.... Unachoweza kufanya ni mawili aidha kuwapotezea mazima AMA kuwaelimisha kwa weledi!? lakini je mshindwa ni mtu wa kuelimishwa? Changamoto iko hapa...!!!!

Jr[emoji769]
WEWE TULIA WEWE-

NYINYI ND'O MNAOTUROGA HUKU KITAA TUSIPATE AJIRA,

NA MNATUROGA HADI KWA MHINDI TUKIENDA KUBETI MIKEKA INACHANIKA!!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka mshana ntaenda kumwambia Yule jamaa maana alifungua hadi Uzi eti kisa umemzidi maaarifa Yule jamaa mashamba sana


Wewe Mzee Wa Jiwe Gizani Umeyakanyaga Mzee ha ha ha ha
 
~hatushangilii ushindi wa wengine
~hatushangilii kupata kwa wengine
~hatushangilii mafanikio ya wengine
~wakipigika na kufanya jitihada za mafanikio na kupata zaidi hatusemi kitu
~wakifanikiwa tunawaponda mwanzo mwisho

~heri kukutana na mchawi kuliko mshindwa anayedhani kushindwa kwake kuna mkono wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom