aibu tupu! Unaombaje uongozi wa jamii, ilhali nyumba yako inakushinda kuongoza?
Tatizo siyo Kiyabo na CCM wake bali njaa za walio ndani ya CCM
MWENYEKITI mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ), aliyetangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Kiyabo, jana alianza rasmi kazi ya kuinadi CCM kwa kumshushia shutuma nzito, aliyekuwa msemaji mkuu wa CCJ ambaye sasa ni mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fred Mpendazoe.
Kiyabo alisema baada ya kumuomba Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kujiunga na CCM na kukubaliwa mbele ya vyombo vya habari ameomba kupewa kazi rasmi ya kuinadi CCM katika Jimbo la Segerea kwa vile ana kazi maalumu katika jimbo hilo.
Katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Kata ya Kimanga uliofanyika jana, Kiyabo alimshambulia Mpendazoe akisema ni mtu asiye makini na ambaye ana uwezo wa kushika wadhifa wa Balozi wa Nyumba Kumi tu na si vinginevyo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita. Wengine waliohudhuria ni mgombea Ubunge katika Jimbo la Segerea kupitia CCM, Dk.
Makongoro Mahanga, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ilala, Suleiman Karanje na mgombea Udiwani wa Kata ya Kimanga, Pastory Kyombya.
Alisema ingawa Mpendazoe ni kaka yake wa damu, lakini hana uwezo wa kuongoza na kwamba udhaifu wake huo umesababisha kumfanya kushindwa hata kuiongoza familia yake na kuifanya kuishi kwa tabu na mashaka.
"Mpendazoe ni kaka yangu, tumenyonya pamoja lakini yeye mwenyewe hajitambui. Ni hatari kuongozwa na mtu asiyejitambua.
Familia yake ilimshinda na mimi ni shahidi kwani nilipata shida sana katika kumtunza mkewe na wanawe Vitalis na David, hafai kuwa kiongozi.
"Nawaombeni itakapofika Oktoba 31, (siku ya upigaji kura kwa uchaguzi mkuu), mgombea wa CCM katika Jimbo la Segerea (Dk. Makongoro Mahanga) apate ushindi wa asilimia 99.5.
Nawaomba msimpigie kura hata moja Mpendazoe maana hafai. "Kwa wakati huu Mpendazoe hawezi kumudu kuongoza nafasi yoyote labda wakati mwingine atakapoomba ndio tutamuangalia.
Na hata kama atarejea CCM mimi nadhani uwezo wake ni kuongoza katika nafasi ya Balozi wa nyumba kumi, tumpime kwanza katika ngazi hiyo kabla ya kumpa kazi nyingine yoyote," alisema Kiyabo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Mahanga alisema ana uhakika wa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo na tayari ameshampata fundi wa kumshonea suti atakayoivaa wakati atakapokwenda bungeni Dodoma kuapishwa.
Kwa upande wake Kyombya alisema kutokana na kazi nzuri aliyoifanya akiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga na kupewa ridhaa ya kushika wadhifa huo katika vipindi viwili, sasa ni wakati muafaka kwake kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kimanga ili aweze kuingia katika vikao vya Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kuwasilisha matatizo ya wananchi wa Kimanga kirahisi zaidi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Guninita, alisema ana uhakika CCM kuibuka na ushindi mkubwa kutokana na kuwa na wagombea makini na wanyenyekevu kwa wananchi wakiongozwa na Rais Kikwete.
source: habari leo
Hivi wadau, huyu jamaa anafanya kazi gani? ili mkono uende kinywani, maanake unaweza kukuta njaa ndo inamsumbua hadi kuamua kumtukana kaka yake mpendazoe
..Kumbe anavyosema alimsaidia mke wa mpendazoe alikuwa anamsaidia ktk majamboz?Richard Kiyabo,
Mkuu wangu kama Mpendazoe ni kaka yako basi wee huna hata aibu na ustaarabu kwani kutoa siri za nyumba ya ndugu yako inatisha sana. Na mbona hukuzungumza kwamba uliwahi kumsalandia pia mkewe Mpendazoe? Au unataka vijana wa mjini tukutoe uchi na ufuska wako!
Aisee. naona unapiga madochi ya uso mkuu.Nafikiri Kiyabo ndo hana uwezo wa kuongoza maana angekuwa nao, CCJ isingemfia mikononi mwake.
Jamani kwa nini Mnamlaumu? Labda sasa ameshasoma sera za CCM na kuzielewa