Elections 2010 Kiyabo "arejea" CCM

Huyu hata hajanunuliwa kenda mwenyewe bure...mwanamme mzima unakuwa kama shoga vile unaturembulia vidume marijali, eti umekabwa ukifa tusikutafute kaburini bali kwenye mioyo ya watanzania kumbe fisadi mnafiki tumeshajuwa pakukutafuta kwa hao vibaraka wako waliokutuma uipotezee CCJ, shenz type...!
 
nampongeza kyabo kwa kugundua kwamba ccm ni kimbilio la wote hasa walipungukiwa na dalili za bright future, mageuzi ya kweli hayaji kwa myopic people

BTW, hivi huyu si ndiye alikua anatuhumiwa kwa ushoga??
 
Hii nchi haitakuwa na wapinzani wengi wa kweli kama watu kama hawa wapo na wataendelea kuzaliwa....Jinsi alivyokuwa akiiponda CCM then sasa hivi karudi kule kule.....NJAAAA...................
 
nampongeza kyabo kwa kugundua kwamba ccm ni kimbilio la wote hasa walipungukiwa na dalili za bright future, mageuzi ya kweli hayaji kwa myopic people

BTW, hivi huyu si ndiye alikua anatuhumiwa kwa ushoga??

ndiyo huyu huyu.....na aliemtuhumu ndo huyo huyo aliempa Kadi.....Cha kushangaza hawajasema kama kwa sasa jamaa haliwi......PUMBAVVVVV
 
ndiyo huyu huyu.....na aliemtuhumu ndo huyo huyo aliempa Kadi.....Cha kushangaza hawajasema kama kwa sasa jamaa haliwi......PUMBAVVVVV
kwahiyo makamba ameonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kumpokea shoga ... safi sana
 
Bwana Kiyabo alikuwa anahojiwa leo asubuhi kwenye kipindi cha patapata WAPO radio. Majibu yake yameniogopesha na kunistusha kwa sababu huyu jamaa ambaye alikuwa anataka kugombea 'the highest office in our country' hana msimamo na ana majibu mepesi sana.

Anadai ameondoka CHADEMA kwa sababu hakupewa ofisi na alikuwa anapigwa vumbi wala hakuwa na uwezo wa kuchangia chochote katika chama. Anajigamba yeye ni mtu safi kwahio hawezi kuongozwa na Dr. Slaa ambaye anapora wake za watu. Hivi kweli hii inamhusu yeye kivipi? Nadhani alihama kabla Dr. Slaa hajachafuliwa kwa uchu wa madaraka aliopoahdiwa nafasi ya kugombea Urais NRA.

Alivyokuwa NRA anadai kuwa alipata wadhamini katika mikoa yote mpaka Zanzibar ila mikoa 2 CHADEMA waliwahonga wadhamini kwahio wakabadili nia. Hivi CHADEMA wana pesa gani ya kuhonga watu, wao wenyewe hawana hata pesa ya kujitangaza.
Kuna mwenyekiti wa CHADEMA kule Tanga ambaye alirudi CCM eti kwasababu alipoumwa CHADEMA haikumtunza. Naomba kuwaasa watu wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi kuwa wasitegemee kusaidiwa bali wao ndio wasaidie wananchi kama unaona hujiwezi kwanini uwe kiongozi? Wawaache wenye nia ya kweli kama wapo wawasaidie wananchi.

Bwana Kiyabo tamaa yako itakuponza na mwisho wako hautakuwa mzuri. Cheap politics and popularity do not build a politician instead destroy completely. We are anxiously monitoring you to see your next move.
 
Hivi mpendazoe alivyohamia CCJ kweli alimjua mwenyekiti wake hadi kuwa msemaji wa Chama hicho? Kazi kweli kweli!
 
Jamani nimemtafuta Mwanakijiji naona mpaka sasa hajachangia hii tread.
Mwanakijiji where are you kikongwe??
 
Wakuu naomba kuuliza mambo mawili:

1. Hivi Kyabo aliwahi kuhama CCM?

2. Hivi tulishawahi kuwa na chama cha siasa kinachoitwa CCJ?


Ni hayo tu
 
Sura ya kish*g@! vile

2852134.jpg
 


MWENYEKITI mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ), aliyetangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Kiyabo, jana alianza rasmi kazi ya kuinadi CCM kwa kumshushia shutuma nzito, aliyekuwa msemaji mkuu wa CCJ ambaye sasa ni mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fred Mpendazoe.

Kiyabo alisema baada ya kumuomba Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kujiunga na CCM na kukubaliwa mbele ya vyombo vya habari ameomba kupewa kazi rasmi ya kuinadi CCM katika Jimbo la Segerea kwa vile ana kazi maalumu katika jimbo hilo.

Katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Kata ya Kimanga uliofanyika jana, Kiyabo alimshambulia Mpendazoe akisema ni mtu asiye makini na ambaye ana uwezo wa kushika wadhifa wa Balozi wa Nyumba Kumi tu na si vinginevyo.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita. Wengine waliohudhuria ni mgombea Ubunge katika Jimbo la Segerea kupitia CCM, Dk.

Makongoro Mahanga, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ilala, Suleiman Karanje na mgombea Udiwani wa Kata ya Kimanga, Pastory Kyombya.

Alisema ingawa Mpendazoe ni kaka yake wa damu, lakini hana uwezo wa kuongoza na kwamba udhaifu wake huo umesababisha kumfanya kushindwa hata kuiongoza familia yake na kuifanya kuishi kwa tabu na mashaka.

“Mpendazoe ni kaka yangu, tumenyonya pamoja lakini yeye mwenyewe hajitambui. Ni hatari kuongozwa na mtu asiyejitambua.

Familia yake ilimshinda na mimi ni shahidi kwani nilipata shida sana katika kumtunza mkewe na wanawe Vitalis na David, hafai kuwa kiongozi.

“Nawaombeni itakapofika Oktoba 31, (siku ya upigaji kura kwa uchaguzi mkuu), mgombea wa CCM katika Jimbo la Segerea (Dk. Makongoro Mahanga) apate ushindi wa asilimia 99.5.

Nawaomba msimpigie kura hata moja Mpendazoe maana hafai. “Kwa wakati huu Mpendazoe hawezi kumudu kuongoza nafasi yoyote labda wakati mwingine atakapoomba ndio tutamuangalia.

Na hata kama atarejea CCM mimi nadhani uwezo wake ni kuongoza katika nafasi ya Balozi wa nyumba kumi, tumpime kwanza katika ngazi hiyo kabla ya kumpa kazi nyingine yoyote,” alisema Kiyabo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Mahanga alisema ana uhakika wa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo na tayari ameshampata fundi wa kumshonea suti atakayoivaa wakati atakapokwenda bungeni Dodoma kuapishwa.

Kwa upande wake Kyombya alisema kutokana na kazi nzuri aliyoifanya akiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga na kupewa ridhaa ya kushika wadhifa huo katika vipindi viwili, sasa ni wakati muafaka kwake kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kimanga ili aweze kuingia katika vikao vya Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kuwasilisha matatizo ya wananchi wa Kimanga kirahisi zaidi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Guninita, alisema ana uhakika CCM kuibuka na ushindi mkubwa kutokana na kuwa na wagombea makini na wanyenyekevu kwa wananchi wakiongozwa na Rais Kikwete.

source: habari leo



Hivi wadau, huyu jamaa anafanya kazi gani? ili mkono uende kinywani, maanake unaweza kukuta njaa ndo inamsumbua hadi kuamua kumtukana kaka yake mpendazoe

 
This one is another Tambwe Hiza...atatumika kupiga debe watakaokula kwa matonge wengine
 
Anatafuta kilichompata Mtikila Tarime. Watu wanafiki na wasio na msimamo na wayumbishaji wa wengine si vema kuwaacha waendelee kupayukapayuka ovyo. Baada ya tukio la Tarime, Mtikila akili ilirudi na kukaa sawa, bado huyu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom