Kiwanda cha Viatu cha Bora chakumbwa na janga la moto

MJIMPYA

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
506
272
Hatati
20190228_071455.jpeg



======


Askari wa Zima Moto wakiendelea na kazi ya

Askari wa Zima Moto wakiendelea na kazi ya kuzima moto uliokuwa ukiwaka kwenye ghala la Kiwanda cha viatu Bora, jijini Dar es Salaam
Kwa ufupi

Marino Machaso ambaye alikuwa mlinzi wa zamu, alieleza kuwa saa 11:00 alfajiri alianza kuona dalili za moto katika ghala hilo na kutoa taarifa kwa fundi umeme ili kuzuia athari.

Advertisement

Dar es Salaam. Vifaa na bidhaa mbalimbali ambavyo thamani yake haijajulika vimeteketea kutokana na moto uliozuka katika ghala.

Ghala hilo ni miongoni mwa maghala kadhaa yaliyopo ndani ya viunga vya kiwanda cha viatu cha Bora kilichopo Tazara jijini Dar es Salaam.

Moto huo ulioanza alfajiri ya jana uliteketeza kwa kiasi ghala hilo lililopangishwa kwa ajili ya kuhifadhia vifaa vya ujenzi.

Mwananchi lilifika kwenye kiwanda hicho na kushuhudia juhudi za kuzima moto huo zikiendelea na kujaribu kuokoa mali zilizomo kwenye maghala yaliyopo jirani yanayotunza bidhaa mbalimbali, zikiwamo za plastiki zinazotengenezwa na kiwanda cha Bora.

Marino Machaso ambaye alikuwa mlinzi wa zamu, alieleza kuwa saa 11:00 alfajiri alianza kuona dalili za moto katika ghala hilo na kutoa taarifa kwa fundi umeme ili kuzuia athari.

“Niliona moshi halafu na harufu ya moto, nikawahi kumtafuta fundi umeme ili akate umeme hilo likafanyika lakini moto tayari ulikuwa umeshika kasi nikawataarifu wenye kiwanda na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.

Ofisa usalama wa kiwanda hicho Sylivery Buyaga, alieleza kuwa huenda matukio ya moto yanayojirudia eneo hilo ni kwa sababu ya uchakavu wa miundombinu.

“Kiwanda ni cha muda mrefu na miundombinu yake iliwekwa muda mrefu hivyo kuna uchakavu ambao tunaweza kusema unasababisha moto kuzuka, ila uchunguzi ukifanyika utaweka wazi nini chanzo cha moto huu,” alisema.

Naye mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Temeke, Michael Bachubila alisema walifika eneo hilo punde baada ya kupata taarifa inagwa walizipata kwa kuchelewa.

“Nitoe rai ukiona cheche tu piga simu Zimamoto tukiwahi kufika madhara yanapungua, hawa wamechelewa walianza kupambana nao kupitia kampuni waliyoingia nayo mkataba,” alisema Bachubila.

Takriban 10 ya zimamoto yalionekana eneo hilo yakizima moto huo ambao ulisababisha kutanda kwa moshi mzito.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiwanda cha Bora kilichopo Nyerere Road kinaungua moto muda huu, Chanzo cha moto uo bado hakijafahamika.


1551333071477.png

1551333134181.png
 
IMG_20190228_090237.jpg

Kiwanda hicho kilichopo Tazara Jijini Dar kinateketea kwa moto

> Kikosi cha zimamoto tayari kimefika eneo la tukio ili kuuzima moto huo
 
Kiwanda cha Bora kilichopo nyerere road mkabala na kiwanda cha kutengeneza sigara kinawaka moto muda huu, jitihada za kuuzima moto unaendelea lkn moto ni mkali sana.

Source MCL
Screenshot_20190228-084038_Facebook.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom