Kwahiyo nikisema 'MADE IN TANZANIA' nakosea kwani?Nachokifahamu ni kuwa owners wa hiki kiwanda kwa sasa ni wa Kenya, niko tayari kusahihishwa.
Mbona walikuwa wana export toka zamani sana.Baada ya kusua sua kwa mda mrefu, kiwanda hiki kilichopo Arusha hivi sasa kina mpango kabambe wa kujiimarisha kimataifa ikiwemo kuanza kuuza bidhaa zake nje ya nchi ikiwemo Kenya, Rwanda, Zanzibar na Burundi..! Hii inatokana na ubora wa hali ya juu sana wa bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo.., pia wanapokea order za kimataifa kwa sasa..!
1.)Tranformer (MADE IN TANZANIA)![]()
2.)Switch gear (MADE IN TANZANIA)![]()
![]()
Source
Mkuu hivi majiko yao yapo mpaka leo?kwaani nayahitaji sana
Kwa taarifa yako tu,TANELEC ni mali ya jirani zetu Wakenya, Tanesco/ABB kiliwashinda, ndipo kikabinafsishwa kwa Wakenya. Cc: Ngongo.
Vv
Hiyo nembo yao ina matatizo kibiashara ‘Bulit in Africa forAfrica'
Ina maana soko lao ni Afrika tu. Mtu wa Indonesia au Poland atajisikiaje hasa tukizingatia image mbovu ya bara hili.
Tukiwa na mipango sahihi tunaweza . Tatizo letu ni rushwa
The Boss watu wanaagiza kutoka India kwasababu ya 10%. Hilo linaua viwanda vyetu vidogo
Pia, ubora wetu ni wa muda. Hatuna mipango ya kuwa na ubora wa kudumu.
Tanelec inanikumbusha Sahara, Tanganyika packers, General tyre, Tanbond n.k. vilivyokuwa na bidhaa nzuri tu
Tujiulize kwanini tunaagiza matairi ya mitumba ikiwa general tyre ilitupa matairi bora sana siku hizo?
Kwanini kiwanda kilikufa?
Kiwanda kama cha betri na radio za 777 kilikuwa na betri bora Afrika mashariki. Leo vimekufa tunaagiza betri. Kwanini?
Shida ya hiki kiwanda ni moja tu
TANESCO
Tanesco wananunua transfomers ghali zaidi na mbuvu zaidi kutoka kwa importers wahindi
why wanafanya hivyo no one knows for sure
Ahsante kwa kauli zakoWatu ambao siyo intelligent kama wewe huwa wananikera sana!
Tanelec wanatengeneza Transformer kwa ajili ya soko la nchi za Kiafrika na ndiko soko lao kuu lilipo sasa ulitaka waseme wanatengeneza transformer for Polish market?
Kwa sasa hivi wanexport Kongo, Uganda, Malawi, Kenya n.w na Transformer za nchi za Kiafrika ziko tofauti kuna mambo ambayo wanayaongezea kutokana na uzoefu walio nao kwa mfano Afrika au TanZania watu wanaiba mafuta ya transformer tanelec wameweza kutengeneza Transformer ambazo huwezi kuiba mafuta sasa hilo ni tatizo lililopo nchi za Kiafrika tu hivyo watengeneza Transformer wengine nje ya Afrika kwa kuwa hawalijui hili tatizo (wizi wa mafuta) hawawezi kushindana na tanelec kwenye hilo eneo na ndio maana wanasema ,,made in Afrika for african market"!
Hili siyo jambo geni kwenye Biashara hata makampuni kama Toyota huwa wanatengeneza Toyota inayoitwa tropical version ambayo ni kwa ajili ya nchi za Kiafrika na iko tofauti na Toyota wanaoipeleka Ulaya au Ujapani!
Ahsante kwa kauli zako
Ungeweza kunielewesha mimi mjinga bila kauli zenye maudhi.Jukwaa hili lina watu wenye upeo tofauti, wa hali juu kama wako na vihiyo kamasisi.
Kwani hiyo logo imetengenezwa kwa ajili ya mfuta yatansformer au imetengenezwa kwa ajili ya transformer?
Je, Tanalec watatengeneza transformer za kuzuia mafuta pekeyake?
Nilidhini ni za kuuza duniani, kama soko kubwa lipo Afrikabado kuna nafasi ya kusema hilo. Siku soko la mafuta likifa ina maana naTanalec ndiyo basi!
Hao Toyota wanaotengeneza ‘Tropical version' nani kwakwambia ni Afrika tu.
Hivi unajua maana ya tropical countries?
Nakushauri ujifunze kujadiliana, utaelewa na kujifunza mambomengi. Ukikaa kwenye keyboard si kubonyeza tu button lazima ujue kwaniniunabonyeza
Watu wanalalamika Wageni wanachukua kazi zetu!!
Ahsante bwana ‘Intelligent'
Kwani tunaongelea nini? Nilidhani tunaongelea logo!^
Kampuni zote Duniani huwa zinakuwa kidogokodogo kulingana na mahitaji na tanelec haiko tofauti kwa sasa hivi wana uwezo wa kutengeneza transformer kwa ajili ya soko la Afrika kwanza hata siyo Afrika yote bali baadhi ya nchi zilizotuzunguka, wakiweza kujiimarisha kwa 100% ndio wataongeza uzalishaji na kufikia nchi nyingi zaidi barani Afrika wakitoka hapo ndio waanangalia nje ya Afrika kama Asia, Ulaya, Marekani na kwingineko!
Ndio maana unakuta kuna makampuni yana miaka 100 siyo kwamba yalianza tu na kuexport Dunia nzima HAPANA bali yalikuwa kidogo kidogo na kwa hatua kwanza kwa kuanzia na soko la nyumbani na baadaye kuanza ktk sasa tanelec kwenye mambo ya Transformer bado ni changa sana na huwezi kuiweka ligi moja na watengenezaji kama Siemens au GE hivyo ni lazima wawekeze nguvu pale wanapoweza kuwa na ushindani!
Kwahiyo nikisema 'MADE IN TANZANIA' nakosea kwani?
Shida ya hiki kiwanda ni moja tu
TANESCO
Tanesco wananunua transfomers ghali zaidi na mbuvu zaidi kutoka kwa importers wahindi
why wanafanya hivyo no one knows for sure
Kuna engineer mmoja nilimuuliza kwa nini wanafanya hivyo alinijibu, ni namna ya kufanya ufisadi!! Wanaagiza nje vifaa vya umeme vibovu kwa bei ya chini then wanasema ni bora zaidi na bei ni kuuubwa!! Kitu ambacho wakinunulia hapa bongo hawataweza kufanya hivyo
Siyo transformer tu, hata vile vikombe vya kwenye nyaya za umeme!! Nasikia kuna kiwanda kinaitwa KIDT (kama sijakosea kipo karibu na Mount Kilimanjaro International school) huko Moshi kinatoa vikombe vyenye ubora wa hali ya juu lakini vinaagizwa nje ya nchi ili wapate kupiga mpunga!! Halafu hivyo vinavyoagizwa ni hovyo hovyo kwa bei kuuubwa
Hii nchi tunaiua wenyewe, wazungu tunawasingizia tu
'Wanarudisha home' kwani zilitoka home?, zimetengenezwa Tz na mtalipa kodi tz, hata mkiuziana kwa robo bei.., MADE IN TANZANIA.Haukosei mkuu ila wanapopeleka hizo Transformer Kenya ni kama wanarudisha home, japo wanauziana ila ni moja pia ya njia ya kusafiririsha pesa kwani hujui watauziana bei gani
Tangu lini mkoa ukawa na rais ndugu..?Hongera kwa Zanzibar kuwa nje ye nchi. Nilidhani ni mkoa wa Tanzania/Tanganyika.