Mkuu Tikera,
ni ukweli usiopingika shamba unalolizungumzia ni la Mkapa. Mwaka 2004/2005 nilikua nafanya consultancy fulani katika kiwanda cha mtibwa, association ya wakulima wa nje wa miwa (Outgrowers association) pamoja na baadhi ya bank zinajishulisha na mikopo kwa wakulima hao.
Vielelezo vingi kutoka kiwandani vilikua wazi vinasema na hata utawala wa kiwanda ulikiri hivyo.
Kwangu mimi Mkapa kumiliki hilo shamba mimi sioni tatizo hata kidogo tatizo lipo kwenye kiwanda.
Ni kweli kwamba mkapa pia ni mwanashare wa Mtibwa Sugar Company inasemekana ana about 75% share yeye na mkewe, mwanashare mwingine ni Manji (quality Group) ambayo pia ndio imewekwa kuendesha kiwanda. what is the problem
1. Bei waliojiuzia kiwanda wakati wa ubinafsishaji ni sawa na kiwira
2. Pamoja na hayo wafanyakazi wake wananyanyasika sana na haki stahiki kama pension zao ambazo walikua wanachangia zimekuwa hazifikishwi NSSF/PPF. walilalamika hadi kwa waziri mkuu Sumaye na hata Lowassa najibu yake yalikua yanakatisha tamaaa
3. Kiwanda kina mkataba na wakulima wa nje (Mtibwa Outgrowers association - MOA) wa kuvuniwa miwa yao na kiwanda kisha kulipwa haki yao within 30days to maximum 45 days). Lakini cha kushangaza hawa mabwana walikuwa hawalipi even after 90days simply wanasema hawana fedha. Wakati sukari wameshaizalisha na kuiuuza, bado wanasema hawana fedha, kinachosikitisha ni kwamba wakulima hawa wamechukua mikopo kwenye mabenki (NBC, CRDB, NMB, n.k kwa wale wako interested mnaweza kupata justification ya hizi info zaidi kwenye hizi bank). Hivyo mkulima huyu wa MOA anabeba mzigo mzito wa riba pamoja na penalt za kutokurejesha mkopo wake kwa wakati. Yote haya ni kwa sababu Mkapa alikua anaweza kuzima jaribio lolote la wakulima hawa wanapotaka kuchukua hatua za kisheria, wapo waliofukuzwa kazi kiwandani, wapo waliokua na kazi zao kama walimu ghafla waliachushwa na kusingiziwa wamengia kwenye siasa n.k Huu ni udhalimu wa mamafya hawa.
4. Kiwanda kimekuwa kikiwalipa wakulima kiwango kidogo(sucross content ndogo below 8 wakati makubaliano ya mtu mwenye miwa belowa 8% wasivuniwe normally ni 8plus na malipo ya miwa yanaendana na kiwango cha sukari kilichopo(kuna mchakato wao waliokubaliana nimeshahau formular). Hivyo kiwanda kinakuja kutoa ile industrial average of sugar content inakuwa below 8% ufisadi wanaufanya hadi wanajiumbua kwamba haiwezekani hata siku moja average sugar content ya wakulima wote iwe chini ya 8 only kukiwa kuna ufisadi. Lakini hata tonnage mizani zilikuwa zinawaibia wakulima na kila ukaguzi wa kushtukiza ukifanyika kulikuwa na hitilafu kwenye mizani hata kama umefanyika within 10days, wakulima kupitia chama chao MOA walilalamika kwa kiwanda, TBS na mamlaka mengine hakuna kilichofanyika kisa Mkapa et al at work. Je ni lini mkulima ataibuka?????? Mzigo wa mkopo wanamuongezea, huku wanamuibia kg zake za miwa na bado wanapunguza kiwango cha sukari ili wamlipe kiwango kidogo, je Tanzania tutaendelea????
5. Kuna hela wakulima wanakatwa kwa ajili ya road maintanance kwenye maeneo ya mashamba yaoili iwe rahisi kuvuniwa magari yanayobeba miwa yasikwame an yaweze kwenda kwa kasi, kwa mwaka wanakusanya about 200 to 300 million kwa jili hiyo. Lakini inapotokea MOA imekamilisha mikakati yake ya kutaka kukarabati barabara kiwanda kinasema hawana hela. wakati hiyo hela sio ya kiwanda ni ya wakulima na kiwanda haipaswi kuitumia kwa namna yeyote ile na kama ikibidi kufanya hivyo lazima ipate idhini kutoka kwa MOA. Lakini kiburi cha hao jamaa ni kikubwa kupita kiasi.
MOA wakafungua account maalum bank kwa ajili kila mwezi mauzo yote ya wakulima na hela za kukarabati ziwekwe kwenye hiyo account bado haikuwa suluhisho. KISA Mkapa na manji wanasema wameshika mpini.
Mbona wakulima wa Kilombero sugar hawapati haya matatizo?????
Kama kuna tatizo mahali kwa nini wasikae na kuzungumza badala ya kutishiana na kunyanyasana hata kama mtu mmoja ana nguvu???
OMBI: Kama serikali inadhamini wakulima huu ndio wakati wa kutatua matatizo yao ieleweke Mtibwa tu annual turnover ni more than 5 Billion kutoka kwa outgrowers. wakisaidiwa hawa wakulima kutoka kwenye matatizo walio nayo mtafanikiwa vile vile kupunguza unamsikini through multiplier effects.
Asante aliyeleta hoja na karibuni kwa michango kwa wenye data zaidi
Du. . . . . !!! Umeongea Vizuri Mpaka Nimetoa Machozi Mkuu Maana Mimi Naijua Mtibwa Kuliko Hata Viganja Vya Mikono Yangu.
Hakuna Ambacho Muhimu Umekiacha.
Kinachonisikitisha Ni Vitendo Ulivyoongea Hapo Yani Utafikiri Nini Sijui.
Daily Wafanyakazi Wanagoma Kwa Kutolipwa Mishahara Kwa Wakati, Yani Mshahara Hulipwa Kwa Muda Wanaotaka Wao Ni Jambo La Kawaida Mpaka Wafanyakaz Wagome, Wazibe Njia Kwa Magogo Pamoja Na Kuwafungia Viongozi Maofisini. FFU Waitwe Kutoka Moro Town 100Kms Ndio Kidogo Panatulia.
Miwa Kupandwa Mpaka Kuvunwa Inachukuwa Miezi9 Lakn Jambo La Kushangaza Unalipwa Pesa Baada Ya Miezi6 Au Zaidi, Sasa Jiulize Unapata Wapi Pesa Ya Kuhumia Shamba Wakat Miwa Ishavunwa Na Pesa Hawakupi, Matokeo Yake Mashamba Mengi Ya Miwa Yamekufa Na Watu Hawahitaji Tena Kulima Miwa.
Miaka Ya 1998 Ambapo Ndipo Kiwanda Kiliingia Mikononi Mwa Watu Binafsi Ndio Wakat Ambapo Mambo Mengi Mabaya Yalianza Kutokea.
Yani Inaniuma Sana Coz Wazee Wetu Miwa Ilikuwa Inawatoa, Hata Shule Tulizosoma Miwa Ndio Imetulipia Karo Lakn Leo Mtibwa Ni Njaa Sana.
Waandishi Wa Habari Wakienda Hawaongei Kweli, Wanaitwa Lakn Wakiondoka Wanazibwa Midomo.
Kuna Mzee Mmoja Pale Kabila Mzigua Alifariki Mwaka Jana, Watu Walipika Mapilau Na Kushangilia Hadharani Kitu Ambacho Hata Watu Wazima Wanasema Hawajawahi Kuona Tangu Wazaliwe.
Huyo Mzee Alikuwa Akishirikiana Na Muwekezaji Kuwanyonya Wakulima Na Wafanyakaz.
Mh.JPM Hili Ni Jipu Kubwa Sana, Kama Kweli Kilimo Ni Uti Wa Mgongo Basi Mmiliki Wa Kiwanda Cha Mtibwa Kashavunja Huo Uti.
Sasa Angalia, Huu Uzi Ni Wa Mwaka 2009 Lakn Mpaka Sasa Matatizo Bado Ni Yale Yale , Labda Cjui Kama JPM Atafanya Mambo Maana Watu Wanahitaji Haki Zao.
Yani Inauma Sana, Lakn Haina Shida, Sote Tutakufa Na Kuacha Mali Tulizojilimbikizia Na Kubeba Laana Za Watu.