Kiwanda cha sukari cha Mtibwa ni mali ya Benjamin William Mkapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiwanda cha sukari cha Mtibwa ni mali ya Benjamin William Mkapa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Feb 12, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jumamosi wiki iliyopita nilikuwa bored kukaa nyumbani nikaona nitembee kwenye countryside, nikaishia kwenye shamba la miwa la Dizungu ambalo sina wasiwasi wowote kwamba ni shamba la Rais wa awamu ya nne aliyestahafu Benjamin William Mkapa.Shamba hili baada ya kuuliza wenyeji wangu, waliniambia kwamba Mkapa alilinunua kwa Mhindi moja ambaye jina nimelisahau.Nadhani hii ni moja ya biashara zake alizofanya akiwa Ikulu!Shamba hili nimeambiwa lina takriban hekta 900.Ni shamba linalotunzwa vizuri.Katia maongezi yetu na jirani zangu, nilitaka kujua mambo mengi.Hata hivyo jambo lililonigusa sana, ni pale mmoja wa wenyeji wangu ambaye ni mfanyakazi wa shamba la Dizungu ambalo ni shamba la Mkapa,alipolalamika kwamba wananchi wa Tanzania tunaibiwa sana.Nilipomuuliza kwa vipi,aliniambia kwamba shamba la Mtibwa ni mali ya Mkapa!Nilipomuambia anipe ushahidi wa kuthibitisha usemi wake,alisema ushahidi upo,nao ni kwamba mishahara yote inatoka Mtibwa,na hata Meneja wa shamba la Dizungu yupo Mtibwa.Alisema kila siku ya malipo,iwe katikati ya mwezi au mwishoni,bwana fedha anatoka Mtibwa kuja kuwalipa.Aliendelea kuniambia kwamba Shamba la Dizungu lina Headman tu, ambaye yuko chini ya Meneja wa Mtibwa.Ushahidi huu ulikuwa so convincing to me,hasa nikizingatia kwamba kumekuwa na minong'ono mingi kuhusu nani hasa analimiliki shamba la Mtibwa.My conclusion is,kama shamba la Mtibwa sio la Mkapa, basi upo uhusiano usiofaa kati yake na kampuni ya Mtibwa.Jee,huu ni ufisadi mwingine?
   
 2. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,545
  Likes Received: 1,296
  Trophy Points: 280
  Mkuu Tikera,

  ni ukweli usiopingika shamba unalolizungumzia ni la Mkapa. Mwaka 2004/2005 nilikua nafanya consultancy fulani katika kiwanda cha mtibwa, association ya wakulima wa nje wa miwa (Outgrowers association) pamoja na baadhi ya bank zinajishulisha na mikopo kwa wakulima hao.

  Vielelezo vingi kutoka kiwandani vilikua wazi vinasema na hata utawala wa kiwanda ulikiri hivyo.

  Kwangu mimi Mkapa kumiliki hilo shamba mimi sioni tatizo hata kidogo tatizo lipo kwenye kiwanda.

  Ni kweli kwamba mkapa pia ni mwanashare wa Mtibwa Sugar Company inasemekana ana about 75% share yeye na mkewe, mwanashare mwingine ni Manji (quality Group) ambayo pia ndio imewekwa kuendesha kiwanda. what is the problem

  1. Bei waliojiuzia kiwanda wakati wa ubinafsishaji ni sawa na kiwira

  2. Pamoja na hayo wafanyakazi wake wananyanyasika sana na haki stahiki kama pension zao ambazo walikua wanachangia zimekuwa hazifikishwi NSSF/PPF. walilalamika hadi kwa waziri mkuu Sumaye na hata Lowassa najibu yake yalikua yanakatisha tamaaa

  3. Kiwanda kina mkataba na wakulima wa nje (Mtibwa Outgrowers association - MOA) wa kuvuniwa miwa yao na kiwanda kisha kulipwa haki yao within 30days to maximum 45 days). Lakini cha kushangaza hawa mabwana walikuwa hawalipi even after 90days simply wanasema hawana fedha. Wakati sukari wameshaizalisha na kuiuuza, bado wanasema hawana fedha, kinachosikitisha ni kwamba wakulima hawa wamechukua mikopo kwenye mabenki (NBC, CRDB, NMB, n.k kwa wale wako interested mnaweza kupata justification ya hizi info zaidi kwenye hizi bank). Hivyo mkulima huyu wa MOA anabeba mzigo mzito wa riba pamoja na penalt za kutokurejesha mkopo wake kwa wakati. Yote haya ni kwa sababu Mkapa alikua anaweza kuzima jaribio lolote la wakulima hawa wanapotaka kuchukua hatua za kisheria, wapo waliofukuzwa kazi kiwandani, wapo waliokua na kazi zao kama walimu ghafla waliachushwa na kusingiziwa wamengia kwenye siasa n.k Huu ni udhalimu wa mamafya hawa.

  4. Kiwanda kimekuwa kikiwalipa wakulima kiwango kidogo(sucross content ndogo below 8 wakati makubaliano ya mtu mwenye miwa belowa 8% wasivuniwe normally ni 8plus na malipo ya miwa yanaendana na kiwango cha sukari kilichopo(kuna mchakato wao waliokubaliana nimeshahau formular). Hivyo kiwanda kinakuja kutoa ile industrial average of sugar content inakuwa below 8% ufisadi wanaufanya hadi wanajiumbua kwamba haiwezekani hata siku moja average sugar content ya wakulima wote iwe chini ya 8 only kukiwa kuna ufisadi. Lakini hata tonnage mizani zilikuwa zinawaibia wakulima na kila ukaguzi wa kushtukiza ukifanyika kulikuwa na hitilafu kwenye mizani hata kama umefanyika within 10days, wakulima kupitia chama chao MOA walilalamika kwa kiwanda, TBS na mamlaka mengine hakuna kilichofanyika kisa Mkapa et al at work. Je ni lini mkulima ataibuka?????? Mzigo wa mkopo wanamuongezea, huku wanamuibia kg zake za miwa na bado wanapunguza kiwango cha sukari ili wamlipe kiwango kidogo, je Tanzania tutaendelea????

  5. Kuna hela wakulima wanakatwa kwa ajili ya road maintanance kwenye maeneo ya mashamba yaoili iwe rahisi kuvuniwa magari yanayobeba miwa yasikwame an yaweze kwenda kwa kasi, kwa mwaka wanakusanya about 200 to 300 million kwa jili hiyo. Lakini inapotokea MOA imekamilisha mikakati yake ya kutaka kukarabati barabara kiwanda kinasema hawana hela. wakati hiyo hela sio ya kiwanda ni ya wakulima na kiwanda haipaswi kuitumia kwa namna yeyote ile na kama ikibidi kufanya hivyo lazima ipate idhini kutoka kwa MOA. Lakini kiburi cha hao jamaa ni kikubwa kupita kiasi.
  MOA wakafungua account maalum bank kwa ajili kila mwezi mauzo yote ya wakulima na hela za kukarabati ziwekwe kwenye hiyo account bado haikuwa suluhisho. KISA Mkapa na manji wanasema wameshika mpini.

  Mbona wakulima wa Kilombero sugar hawapati haya matatizo?????

  Kama kuna tatizo mahali kwa nini wasikae na kuzungumza badala ya kutishiana na kunyanyasana hata kama mtu mmoja ana nguvu???

  OMBI: Kama serikali inadhamini wakulima huu ndio wakati wa kutatua matatizo yao ieleweke Mtibwa tu annual turnover ni more than 5 Billion kutoka kwa outgrowers. wakisaidiwa hawa wakulima kutoka kwenye matatizo walio nayo mtafanikiwa vile vile kupunguza unamsikini through multiplier effects.

  Asante aliyeleta hoja na karibuni kwa michango kwa wenye data zaidi
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nadhani muda si mrefu tutasikia ile kinga yake inajadiliwa Bungeni hasa tunapozidi kukaribia 2010. Siamini kama Uchaguzi wa 2010 utapita hivi hivi bila Bunge kujadili kunga ya Mkapa ili kukiwezesha CCM kujiwekea mazingira ya ushindi.

  Ni suala la muda tu.
   
 4. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Taraatibu ndio mwendo, yatafichuka tu yote yaliyojificha! Naisubiri kwa hamu hiyo siku
   
 5. share

  share JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,294
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Mjasiliamali mkapa na mali za wadanganyika! Tutafika kweli!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo ambayo hata mtu uwe mahiri kiasi gani huwezi sweep under carpet. Kwa Mheshimiwa Mkapa kuna upepo wa kimbunga ambao unazidi kumkaribia pamoja na jitihada za kuukimbia mbali. Itakuwa vema akafikiria kujitakasa na kuueleza umma ukweli mana kukaa kimya sana, inaleta msukumo wa kuhisi kila alichonacho hakukipa kwa njia halali. Pengine yapo mengine ameyapata kwa kufuata taratibu zote, na ni yeye kutuelimisha hivyo kulikoni ilivyo sasa kutuachia wenyewe kusuka ama kunyoa. Au ndio kuthibitisha kuwa hakuzipata kihalali? Kwa kuwa yeye ni public figure, angetoa hizi dukuduku za watu kwa kusema yoote.
  Nilishawahi kusikia hili la Mtibwa...na tetesi pia zasema hata Kagera sugar inaendeshwa na Superdoll kwa niaba ya wanasiasa fulani waliojiuzia bei chee iliyokuwa mali ya umma.
  Kazi kwelikweli
   
 7. B

  Bi Tarabushi Member

  #7
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jumamosi wiki iliyopita nilikuwa bored kukaa nyumbani nikaona nitembee kwenye countryside, nikaishia kwenye shamba la miwa la Dizungu ambalo sina wasiwasi wowote kwamba ni shamba la Rais wa awamu ya nne aliyestahafu Benjamin William Mkapa.Shamba hili baada ya kuuliza wenyeji wangu, waliniambia kwamba Mkapa alilinunua kwa Mhindi moja ambaye jina nimelisahau.
  Correction, Benjamin Mkapa ni rais wa awamu ya tatu na si ya nne kama ulivyoainisha hapo juu mkuu..
   
 8. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Siku hizi ni Mwinjilisti Mkapa. Nadhani Mzee Mkapa kama ni kweli amejiuzia Mtibwa Sugar na kwa kuwa amekubali kuwa Mwinjilisti ni vema aturudishie Kiwanda chetu, akiri tu kuwa alijiuzia, ataje kiasi alichotoa ili kununu kiwanda na kisha Serikali ifikirie kumrudishia pesa zake na ianze upya machakato wa kubinafsisha Mtibwa Sugar.
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Please, do not kill me by heart attack!!! he nicknamed himself "Mr. Clean". It does not click on my nerves!!! Ila hapa sijajua katiba inasemaje kuhusu Rais wa nchi kujipatia utajiri au mali nyingi kupitia Ikulu!!! Pengine kuna kifungu kinamlinda. Vinginevyo naomba hivi, Iundwe tume kupitia ubinafsishaji wa Viwanda vyote au tuseme rasilimali za watanzania tupate kufahamu wamiliki halali. Hiyo report naamini itatoa mtu Roho au kupata permanent Comma.

  Mkapa na Anna mmetumaliza. Mnajidai hamuelewani kimaisha ya ndani but kiutajiri mnaelewana. kweli nyie ni wajanja ila si wa kuigwa.
   
 10. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ama kweli Mkapa kajiandalia bonge la bingo maishani mwake lakini analaanika kwa kutotenda haki katika unyakuaji wa mali za umma.JK upo harakisha suala la kinga ya Mkapa kwani wizi wake unazidi kufichuliwa,vitegauchumi alivyopora vinatosha kulipia 100% ya mikopo ya vyuo vikuu.
   
 11. w

  wajinga Senior Member

  #11
  Feb 12, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi nyie watanzania nani aliwaambia kwamba mkapa anakinga. Kinga ya namna gaani.Kinga ni wakati rais anatawala nchi tu baaasi. Akiondoka hana kinga. Kama unataka kumshitaki rais anaetawala ndio mbunge linaondoa kinga yake ili ashitakiwe. Mkapa sio rais na makosa aliyofanya ni ya jinai kuiibia republic.
   
 12. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2016
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Hivi Magufuli anaweza Kuutafuna huu mfupa??? Ndiyo maana kwenye kampeni alikomaa sana kututukana ni malofa na wapumbavu
   
 13. Osmokalu

  Osmokalu Member

  #13
  Apr 21, 2016
  Joined: Nov 13, 2015
  Messages: 78
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 25
  Mkapa ana roho mbaya sana ma mia ya familia Tanzania wanatabika kutoka na mali za wananchi alizo jibinafsishia.Mtibwa anahusika %100.Kiwanda cha karatasi Mgololo mpaka leo wafanyakazi wa iliokua SPM Hawajapata stahiki zao kutokana kupeana mali za wanchi yeye na jamaa zake.Anadhambi sana huyu mtu.Mambo mengi aliyodhulumu.Daahhaaa
   
 14. Tobinho

  Tobinho JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2016
  Joined: Nov 28, 2014
  Messages: 1,250
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  autafune ana meno?
   
 15. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2016
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,130
  Likes Received: 9,001
  Trophy Points: 280
  As long as Magufuli ni CCM haya hatoyaweza!! Ndio maana yupo busy sana kudraw attention ili kuziba watu macho na masikio wasione wala kujadili haya....

  ...........Lakini yana Mwisho......
   
 16. aminiusiamini

  aminiusiamini JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2016
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,416
  Likes Received: 1,298
  Trophy Points: 280
  Hakuna marefu yasiyo na ncha mkuu.
  Ila mimi nataka kuprove kwenye mathematica kuwa infinity number doesnt exist.
  Has to be an end to everything in this world. The day begins and it ends so do seasons and years .
  I mean everything has an end.
   
 17. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2016
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,130
  Likes Received: 9,001
  Trophy Points: 280
  Kabisa!! Kila jambo lina mwisho.... Ni suala la muda tu!!
   
 18. Prosper C Manasse

  Prosper C Manasse JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2016
  Joined: Dec 8, 2015
  Messages: 639
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 180
  Du. . . . . !!! Umeongea Vizuri Mpaka Nimetoa Machozi Mkuu Maana Mimi Naijua Mtibwa Kuliko Hata Viganja Vya Mikono Yangu.
  Hakuna Ambacho Muhimu Umekiacha.
  Kinachonisikitisha Ni Vitendo Ulivyoongea Hapo Yani Utafikiri Nini Sijui.

  Daily Wafanyakazi Wanagoma Kwa Kutolipwa Mishahara Kwa Wakati, Yani Mshahara Hulipwa Kwa Muda Wanaotaka Wao Ni Jambo La Kawaida Mpaka Wafanyakaz Wagome, Wazibe Njia Kwa Magogo Pamoja Na Kuwafungia Viongozi Maofisini. FFU Waitwe Kutoka Moro Town 100Kms Ndio Kidogo Panatulia.

  Miwa Kupandwa Mpaka Kuvunwa Inachukuwa Miezi9 Lakn Jambo La Kushangaza Unalipwa Pesa Baada Ya Miezi6 Au Zaidi, Sasa Jiulize Unapata Wapi Pesa Ya Kuhumia Shamba Wakat Miwa Ishavunwa Na Pesa Hawakupi, Matokeo Yake Mashamba Mengi Ya Miwa Yamekufa Na Watu Hawahitaji Tena Kulima Miwa.

  Miaka Ya 1998 Ambapo Ndipo Kiwanda Kiliingia Mikononi Mwa Watu Binafsi Ndio Wakat Ambapo Mambo Mengi Mabaya Yalianza Kutokea.

  Yani Inaniuma Sana Coz Wazee Wetu Miwa Ilikuwa Inawatoa, Hata Shule Tulizosoma Miwa Ndio Imetulipia Karo Lakn Leo Mtibwa Ni Njaa Sana.

  Waandishi Wa Habari Wakienda Hawaongei Kweli, Wanaitwa Lakn Wakiondoka Wanazibwa Midomo.

  Kuna Mzee Mmoja Pale Kabila Mzigua Alifariki Mwaka Jana, Watu Walipika Mapilau Na Kushangilia Hadharani Kitu Ambacho Hata Watu Wazima Wanasema Hawajawahi Kuona Tangu Wazaliwe.
  Huyo Mzee Alikuwa Akishirikiana Na Muwekezaji Kuwanyonya Wakulima Na Wafanyakaz.

  Mh.JPM Hili Ni Jipu Kubwa Sana, Kama Kweli Kilimo Ni Uti Wa Mgongo Basi Mmiliki Wa Kiwanda Cha Mtibwa Kashavunja Huo Uti.

  Sasa Angalia, Huu Uzi Ni Wa Mwaka 2009 Lakn Mpaka Sasa Matatizo Bado Ni Yale Yale , Labda Cjui Kama JPM Atafanya Mambo Maana Watu Wanahitaji Haki Zao.
  Yani Inauma Sana, Lakn Haina Shida, Sote Tutakufa Na Kuacha Mali Tulizojilimbikizia Na Kubeba Laana Za Watu.
   
 19. Osmokalu

  Osmokalu Member

  #19
  Apr 21, 2016
  Joined: Nov 13, 2015
  Messages: 78
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 25
  Mheshimiwa Magu anaijua vizuri Mtibwa na sijui kama ataiweza.JK kafika pale kachekacheka kaondoka madarakani ipo shidaaa.Baba Magu fanyia kazi MTIBWA na nasikia Nassoro kajenga kiwanda cha kutakatisha sukari Huko uarabuni kwa pesa za MTIBWA
   
 20. m

  mwembemdogo JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2016
  Joined: Feb 28, 2016
  Messages: 2,293
  Likes Received: 1,225
  Trophy Points: 280
  Masikini Tanzania mkapa tulimpa nchi atulindie kumbe anajiuzia Kwa bei ya kujipangia Mungu tuonee huruma
   
Loading...