Kiwanda cha kutengeneza bacteria kilichojengwa Kibaha kwa ajili ya kutafuna viluwiluwi vya mbu

Asante

JF-Expert Member
Dec 18, 2009
2,086
1,081
Big-boost-for-war-against-malaria1.png

Rais Kikwete mwaka jana alifungua kiwanda cha kutengeneza bacteria kilichojengwa Kibaha kwa ajili ya kutafuna viluwiluwi vya mbu pale dawa hiyo inapowekwa kwenye madimbwi ya maji. Kiwanda hiki kiko chini ya NDC na ujenzi wake ulidhaminiwa na nchi ya Cuba na tuliambiwa uzalishaji ungeanza rasmi mwezi wa December 2015, lakini ukitembelea website ya NDC hakuna maelezo yoyote ya maana kuhusu kiwanda hiki, naomba yeyote anayejua ni wapi nitapata hizi dawa hapa Dar es Salaam au Kibaha anifahamishe tafadhali.
 
Kiwanda hiki mwanzo kilichelewa kuanza kwa shinikizo la watengenezaji wa dawa za kupulizia, NDC walifanya jitihada kubwa hadi kiwanda kikajengwa, tatizo jipya ni kuwa kiwanda kinazalisha na kuuza dawa zote nje ya nchi. National Development Corporation (NDC) wako kimya hawana majibu ni lini dawa hizi zitaanza kupatika madukani Tanzania?
 
Pooor investments ni sawa na Dangote hadi leo hatuoni Cement ya 8000
 
kuna vita kubwa sana juu ya hii teknolojia,wanufaika wa miradi ya magonjwa yanayosambazwa na mbu hawako tayari kuona kiwanda kinaendelea,kwani kinagusa maslahi yao direct.serikali lazima ipambane,na itambue kuwa hii ni teknolojia mpya africa,na ina biashara ya uhakika Africa na Asia.kudeal na bacteria au virus ni ngumu,pia ni hatari, NDC lazima ihakikishe wataalam wa kitanzania wanaofanya kazi kwenye huo mradi wanahudumiwa ipasavyo ili akili zao ziwaze kutulia na kufanya kazi kwa umakini. nitashangaa sana virusi vya ZIKA vitakapoingia nchini dawa iagizwe nje wakati tuna kiwanda pale kibaha.
 
National Development Corporation (NDC) kwa sasa hivi kuna tatizo ndani ya hili shirika.
 
Zika-virus-baby_816x544.jpg

Mtoto aliyezaliwa akiwa ameathirika na ugonjwa wa ZIKA unaoenezwa na mbu.
Zika-virus.jpg
 
kwa sasa tusipowatumia hao watu wa CUBA vizuri,nchi itakuja kujuta.hao jamaa nawajua,maswala ya sayansi ya afya wapo vizuri sana.
 
Mkwere yeye alikuwa anazindua tu wala haulizi hatua kilipofikia. Si ujajua hata mradi wa mabasi ya kasi ya ajabu DSM alishazindua, yako wapi sasa!!
 
Kiwanda ndio kwanza kinatafutiwa mkopo Wa bilioni 3 kinunue baadhi ya mashine zilizoungua wakati Wa majaribio na malighafi ya kuzalishia dawa.mashine ziliungua kutokana na hitilafu ya umeme.na serikali imekinyima pesa .Ila wameagizwa wakope na kwamba ikifika mwezi march 2016 wawe wameanza uzalishaji.huu ndio ukweli akijawahi zalisha chochote.
 
Yaani kiwanda hakijawekewa bima ya moto, hii ni mzaha sasa
 
Ajabu ataa Kikwete alikifungua kikiwa kimekufa tayari .hapo ndio utashangaa zaidi.nikama ilikuwa lazima akifungue kwakuwa ndio alikiomba tujengewee na wacuba
 
Kiwanda ndio kwanza kinatafutiwa mkopo Wa bilioni 3 kinunue baadhi ya mashine zilizoungua wakati Wa majaribio na malighafi ya kuzalishia dawa.mashine ziliungua kutokana na hitilafu ya umeme.na serikali imekinyima pesa .Ila wameagizwa wakope na kwamba ikifika mwezi march 2016 wawe wameanza uzalishaji.huu ndio ukweli akijawahi zalisha chochote.
Hujuma
 
Kabla rais mstaafu Dr. Kikwete hajaondoka madarakani alizindua kiwanda cha Tanzania Biotech Products kinachomilikiwa na NDC huko Kibaha. Kiwanda hiki Kinazalisha viuadudu vya kuua viluilui vya mbu wanaoeneza Malaria, Dengue, Rift valey Fever, Yellow fever. Tangu kiwanda hicho kizinduliwe Julai 2015 hadi leo hata haieleweki kama kinazalisha au lah, Mkurugenzi wa NDC anajinasibu kuwa kinazalisha, lakini ukweli hakuna kinachozalishwa. Na hata wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya 7/7 mwaka huu bado walijinasibu kuwa wanazalisha.

Sasa mi najiuliza mkurugenzi wa NDC na menejiment yake wanamhadaa nani? Kama wanazalisha wanauzia wapi? Na kama hawazalishi kwanini wanasema wanazalisha bidhaa? Kabla kiwanda hakijatengemaa mwaka jana NDC wakaja na issue ya kiwanda cha General Tyre, wakati ule wa kampeni mambo yalikuwa "Bam bam" tukaaminishwa General Tyre inafufuka, sasa huu unaenda mwaka si General Tyre si kiwanda cha Kibaha.

Ajabu na waziri wa viwanda nae yupo kimyaaa, Kibaha wala si mbali na Dar es Salaam lakini hata kusema atembelee kiwanda kujionea uzalishaji nae amenyamaza tu. Kweli tunahitaj Tanzania ya viwanda mbona kiwanda cha NDC kimeshaonesha kuwa tumeshindwa? Shida iko wapi? Nani ni kikwazo?
Ila kuna hizi tetesi za wafanyakazi wake kutolipwa mishahara kwa muda mrefu, miezi mitatu hadi minne nayo inatia kinyaa..."KAMA NI KWELI".

Nadhani NDC sasa wanapaswa kwenda na kasi ya rais aliyeaidi viwanda basi hivi vilivyopo vioneshe mfano, hakuna maana kuwa na majengo while uzalishaji hamna then kwenye mipango mnasema mna kiwanda, MNAZALISHA NINI?
NDC ikisimamia mipango yake mbona hata hatutahitaji wachina waje kujenga viwanda vya YEBOYEBO HAPA NCHINI.
 
Back
Top Bottom