Kiwanda cha kuchapisha vitabu Afroplus - Mwenge Chabomolewa usiku. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiwanda cha kuchapisha vitabu Afroplus - Mwenge Chabomolewa usiku.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tenende, Jan 11, 2012.

 1. t

  tenende JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  BOMOA BOMOA ILIYOENDESHWA na askari wa kiongozi wa kidini Josephat Mwingira USIKU wa kuamkia jumapili, umekiacha kiwanda katika uharibifu mkubwa wa mali. Kiwanda hiki kinapatikana karibu na SUMA JKT (sehemu ya Lugalo JWTZ) kikipakana ka kanisa la EFATHA. ENEO hili lina mgogoro wa muda mrefu na kesi iko mahakamani.
  Tinanga tinga, mabaunsa na walinzi wenye silaha walivamia kiwanda usiku saa 2, wakamkamata mlinzi, wakamnyang'anya simu, wakamfunga kisha wakaanza ubomoaji. Mitambo ya uchapishaji vitabu imeharibiwa vibaya, jengo, ofisi, samani za ofisi, nyaraka mbalimbali, vitabu na mali nyingine. Pia wizi ulitokea na vifaa mbalimbali zikiwemo kompyuta havionekani. Coverage ya habari hii kwenye vyombo vya habari haikupewa uzito. Lakini UKIMYA huu wa jamii pamoja na viongozi ni hatari sana kwa usalama wa watu hapo baadaye. UBABE PIA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NI HATARI SANA HASA UKITENDWA NA VIONGOZI WA DINI.
  Picha zinazoonyesha uharibifu huu nitazitoa muda wowote zitakapohitajika.:alien::hatari::hatari::hatari::hatari::hatari:
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Huyo nabii wa kuzimu sasa tamaa inamwelemea! ila yana mwisho
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Mazito! Hiyo bomoa bomoa imefanyika alfajiri ya leo?
   
 4. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 811
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Picha zinazoonyesha uharibifu huu nitazitoa muda wowote zitakapohitajika.

  Ndio zinahitajika sasa hebu tuwekee tuone huo udhalimu
   
 5. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mh jamani watumishi haya tutajua vizuri mbinguni,
   
 6. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Japo simwamini Mwingira katika utendaji wake, bado naamini taarifa hii inakandamiza upande mmoja. Toa ukweli wa pande zote.
   
 7. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Tenende mwaga picha... Huyu Mwingira amezoea ku~grab Mali za watu... Mfano Bagamoyo na hata hapo Kanisa lake lilipo alimpora Simon Eng.Group... Eti Nabii wakati yeye ni MAFIA...
   
 8. t

  tenende JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  P1090156.JPG P1090157.JPG P1090158.JPG P1090159.JPG P1090160.JPG P1090161.JPG P1090162.JPG P1090163.JPG P1090164.JPG P1090165.JPG P1090166.JPG P1090167.JPG P1090168.JPG P1090173.JPG P1090171.JPG P1090172.JPG P1090174.JPG P1090175.JPG P1090176.JPG P1090177.JPG P1090178.JPG P1090179.JPG P1090180.JPG P1090181.JPG P1090182.JPG P1090166.JPG
   
 9. t

  tenende JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haya si masalia ya majengo yaliyolipuliwa na mabomu nchini Iraq, Afghanistan, Pakistan au Nigeria. Hii ni kazi iliyofanyaka MWENGE katika mgogoro mbaya kabisa uliopo kati ya nabii Mwingira wa EFATHA na wamiliki wa kiwanda cha AFROPLUS.
  Hakuna jengo la EFATHA lilikumbwa na bomoa bomoa. Lakini kiwanda hiki kimebomolewa vibaya na mitambo yake yenye thamani ya mamilioni ya fedha ikiwa imeharibiwa vibaya na kuta zilizoangushwa usiku wa jumamosi (tarehe 7/1/2012) kuamkia jumapili (tarehe 8/1/2012). Hasara yote hiyo kabebeshwa mmiliki wa kiwanda hiki.
  Nabii huyuhuyu ana migogoro kama hii Kibaha na Bagamoyo. Na tena zipo taarifa kwamba nyuma yake kuna wakubwa, mmoja wao
  akiwa waziri mkuu mmoja wa zamani (siyo aliyejiuzuru).
  Kuna taarifa kwamba alinunua kinyemela maeneo ya viwanda kwa millioni 400. Anabomoa majengo ya viwanda hivi na kuiacha mitambo ikiharibika. Hata ukitembelea leo utajionea eneo likiwa na mitambo ya makampuni yaliyobomolewa.
  AFROPLUS ni wachapisha wa vitabu vya waandishi mbalimbali wazalendo. Sasa kazi imesimama kwa wiki nzima, kwenye picha hizo wafanyakazi wanaonekana wakifanya ukarabati wa majengo hayo. mingine ni mitambo iliyoharibika n.k.
   
 10. t

  tenende JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
 11. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pia waziri wa fedha wa awamu iliyopita nae ni jeuri na kibri kingine kinachompa mwingira afanye haya anayoyafanya! mwehu kweli huyu jamaa.
   
 12. t

  tenende JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wazo zuri, lakini vyovyote kwa hili siwezi kumwonea. Hasa ukijua kuwa haifai kuwasema vibaya viongozi wa dini. Naomba mwingine mwenye utetezi wake atuletee. Mimi nimeanzisha mjadala. ANGALIA PICHA. MMOJA AENDE KIWANDANI AJIONEE, KISHA AFIKE KANISANI KWAKE EFATHA AKUSANYE TAARIFA.
   
 13. t

  tenende JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wazo zuri, lakini vyovyote kwa hili siwezi kumwonea. Hasa ukijua kuwa haifai kuwasema vibaya viongozi wa dini. Naomba mwingine mwenye utetezi wake atuletee. Mimi nimeanzisha mjadala. ANGALIA PICHA. MMOJA AENDE KIWANDANI AJIONEE, KISHA AFIKE KANISANI KWAKE EFATHA AKUSANYE TAARIFA.
   
 14. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mpaka amefikia hatua ya kuja usiku na kufanya bomoa bomoa kuna msukumo na ujasiri fulani alionao. je mahakama ilishatoa amri ya mwisho...nini tamko la mahakama? je mmiliki wa kiwanda hiki ndiye mmliki wa eneo hilo? kuna amri yeyote iliwahi tamkwa na mahakama iliyokuwa inashughulikia mgogoro huu?..unawekana labda upande mmoja umekaidi agizo la mahakama...sasa sisi hatutaweza kujua ni mpaka mleta maada aweke mambo hadharani halafu itakuwa rahisi kuchangia.
   
Loading...