Wengi watadhani kuwa mpango wa kufufua kiwanda cha kutengeneza matairi kilichopo jijini Arusha umeanza hivi karibuni baada ya Mh Lowasa kuzungumzia juu ya kiwanda hicho. Kama mdau nimeona nikanushe taarifa hizo.
Jitihada za serikali za kufufua kiwanda hicho zilianza siku za nyuma, zaidi ya mwaka na nusu sasa umepita.
Nikiwa ofisini, nilipokea taarifa kuwa tunatakiwa kwenda kwenye ofisi za National development corporation kuchukua nyaraka za tenda kwa ajili ya kufanya marekebisho kwenye mfumo wa umeme wa kiwanda hicho. Ila kutokana na kampuni yetu kutokuwa na uwezo wa kutoa huduma katika maeneo yote na kwa kwa kuwa kampuni yangu ilikataa mapendekezo niliyotoa ya kuingia Joint venture na kampuni moja wapo, niliachana na tenda hiyo. Mwishowe kulingana na kumbukumbu nilizo nazo, kampuni ya Urban and rural engineering ya jijini Dar Es Salaam, ndiyo ilishinda zabuni hiyo na fedha hizo zaidi ya milioni mia sita za marekebisho katika mifumo ya umeme kugharimiwa na NDC. Marekebisho hayo yalijumuisha kufunga mota mpya kadhaa zenye uwezo mbali mbali, kubadishisha nyaya za umeme n.k.
Kwa muhtasari huo napenda kuwajuza uma wa watanzania wasipotoshwe kwenye kila jambo linalohusu maendeleo ya taifa hili kwa kufanya kila kitu kisiasa....