KWELI Kivunja chungu 'praying mantis' hana madhara kwa binadamu

KWELI Kivunja chungu 'praying mantis' hana madhara kwa binadamu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Screenshot 2025-11-26 091242.png
 
Tunachokijua
National Geographic World inafafanua kuhusu 'Kivunja Chungu ambaye kwa kwa kiingereza anajulikana kwajina la la 'Praying Mantis' ambapo hawa ni wadudu wanaowinda, na jina lao limetokana na namna wanavyoshikilia miguu yao ya mbele ambayo hukunjwa na kuwekwa karibu kana kwamba wako katika hali ya kuomba ama kusali.

Mara nyingi hula wadudu kama nyuki, mende, panzi, nondo, vipepeo na vigelegele. Pia anaweza kula buibui na viumbe wengine wasio na uti wa mgongo. Hata hivyo, kama buibui atakuwa mkubwa kuliko yeye, kuna uwezekano mantesi mwenyewe akawa mhanga katika makabiliano hayo.

National Geographic inaeleza moja ya tabia maarufu ya mantisi ikiwa ni mwenendo wao wa kujamiana wenye ukatili ukijulikana kama sexual cannibalism. Madume, ambao ni wadogo kuliko majike, huweka maisha yao hatarini na mara nyingine huishia kuwa mlo. Takribani asilimia 30 ya wakati wote, jike humng’ata dume kichwani na kuendelea kukila hadi kiishe wakati mwingine kwa saa kadhaa mwili wa dume ukijaribu kuendelea kujamiana hata ukiwa unakaribia kufa.

Utafiti uliochapishwa mwaka 2016 uligundua kwamba majike wa mantisi wa Kichina wanapowala madume wao, hupata asidi muhimu za amino ambazo hutumika baadaye katika kutengeneza mayai wanayoweka. Pia inaonekana kwamba baada ya kumla dume, jike huweza kutaga mayai mara mbili zaidi ya kiasi ambacho kingetaga kwa kawaida.

Mantis hawana sumu wala hawaumi kwa kudunga. Pia hawabebi magonjwa ya kuambukiza. Na ingawa baadhi ya spishi, kama ile ya Afrika Mashariki ijulikanayo kama Leptocoloa phthisica, zinaweza kukua hadi karibu inchi 10 kwa urefu, midomo yao bado ni midogo sana.

Hii ina maana kwamba hata kama mantisi angeukuta kidole chako, taya zake hazina nguvu ya kusababisha jeraha kubwa.
​
Anaweza kumuuma binadamu, lakini hilo hutokea mara chache sana. Akijihisi kutishiwa na mtu, mantisi mara nyingi huchukua mkao wa kujilinda badala ya kujaribu kuuma.

Mantisi wadogo wenye urefu wa inchi tatu au chini ya hapo wakiuma binadamu, kuumwa huko huenda hakutohisiwa kabisa. Hata hivyo, kuumwa na mantisi mkubwa (ambaye anaweza kukua hadi karibu inchi nane) kunaweza kusababisha usumbufu kidogo, sawa na kuumwa na mbu.

​

​

​

Back
Top Bottom