Kivuko cha MV kome III kuongeza nguvu Buchosa

Kivuko cha MV kome III kuongeza nguvu Buchosa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
KIVUKO CHA MV KOME III KUONGEZA NGUVU BUCHOSA

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) inatekeleza mradi wa ujenzi wa vivuko vipya 6.

Kivuko MV.KOME III no moja ya vivuko hivyo na kitakwenda kutoa huduma katika maeneo ya Nyakaliro Wilaya ya Buchosa na Kome Wilayani Sengerema.

Kivuko cha MV KOME III tayari ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 83% na kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 170, abiria 800 pamoja na magari 22.

Eneo hilo tayari lina kivuko MV. KOME II ambacho kinabeba tani 40, pamoja na abiria 120. Serikali imeona kwamba kivuko MV. KOME II hakitoshelezi mahitaji ya wakazi wa maeneo hayo ambao wanazidi kuongezeka siku hadi siku
 

Attachments

  • FB_IMG_1744876997915.jpg
    FB_IMG_1744876997915.jpg
    91.7 KB · Views: 15
Back
Top Bottom