Kiukweli, nimeifurahia hukumu ya Lengai Ole Sabaya

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Nawasalimu waungwana wa JF,

Jana ilisomwa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake. Sasa inajulikana kuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Kila upande: wa mashtaka na ule wa utetezi una haki ya kukata rufaa ndani ya muda na taratibu zinazoainishwa na sheria.

Kiukweli, bila kujali kitakachotokea kwenye hatua ya rufaa, nimeifurahia hukumu ya akina Sabaya. Sifurahii mwenzangu Sabaya na yeyote yule kutumikia kifungo jela. Sifurahii mateso kwa mwenzangu yeyote yule. Jela si mahali pa kupafurahia.

Nilichokifurahia ni UJUMBE WA WAZI uliotumwa na Mahakama kupitia hukumu ile. Ujumbe wa kwamba kwenye jinai matendo ya mtu hutengwa na nafasi yake ya kiuongozi na kisiasa. Yaani,kiongozi anapotenda jinai hapaswi kujibanza kwenye nafasi yake ili kijinasua. Uongozi umetengwa mbali na matendo binafsi ya mtu aliyekuwa kiongozi. Ujumbe murua kabisa.

Hukumu ya Ole Sabaya inashabihiana na ile ya kwenye shauri la madai la Mchungaji Mtikila dhidi ya Mzee Augustino Mrema. Kwenye shauri tajwa, mahakama ilitenganisha matendo/maneno ya mtu binafsi na uwaziri wake(Mrema).

Hukumu ya Sabaya itufunze na kutukumbusha kutenda ya haki na halali pale tunapobarikiwa kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali. Hukumu hiyo itukumbushe pia kuwa uongozi hautaweza kuwa kichaka cha kujificha pale ambapo jinai au madai yatakapoletwa dhidi ya mhusika.

Jinai hufa na mhusika tu, haizeeki!
 
Tutofautiane kidogo; hii hukumu ya Sabaya usiitumie kama kigezo cha mahakama kuwa huru, binafsi naamini Sabaya amehukumiwa kwasababu yule aliyemtegemea amlinde alifariki, kama bado angekuwa hai, Sabaya hata mahakamani asingepelekwa.

- Pia, wako wale waliojitungia sheria za kuwalinda, wanafanya maovu makusudi wakijua hawataguswa na yeyote, hili linaonesha kama nchi bado tuna safari ndefu sana kufikia haki ya kweli licha ya hukumu ya Sabaya hapo jana.

Lakini pia kama ulivyosema, nafasi pekee ya Sabaya kwa sasa kujinasua na hukumu ya jana ni kwa kukata rufaa, japo naona nafasi yake kushinda rufaa hiyo ni ndogo sana.

Hapa nadhani Sabaya anaweza kutoka kifungoni sio chini ya 2030 kwa haraka haraka, pale ambapo Rais wa sasa atakapokuwa amemaliza muda wake, hii naifananisha na ile hukumu ya Babu Seya na mwanaye ambapo licha ya kuhangaika kwao kukata rufaa na kushindwa chini ya utawala wa Kikwete, walikuja kutolewa na Magufuli kwa mapenzi yake.
 
Nawasalimu waungwana wa JF,

Jana ilisomwa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake. Sasa inajulikana kuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Kila upande: wa mashtaka na ule wa utetezi una haki ya kukata rufaa ndani ya muda na taratibu zinazoainishwa na sheria.

Kiukweli, bila kujali kitakachotokea kwenye hatua ya rufaa, nimeifurahia hukumu ya akina Sabaya. Sifurahii mwenzangu Sabaya na yeyote yule kutumikia kifungo jela. Sifurahii mateso kwa mwenzangu yeyote yule. Jela si mahali pa kupafurahia.

Nilichokifurahia ni UJUMBE WA WAZI uliotumwa na Mahakama kupitia hukumu ile. Ujumbe wa kwamba kwenye jinai matendo ya mtu hutengwa na nafasi yake ya kiuongozi na kisiasa. Yaani,kiongozi anapotenda jinai hapaswi kujibanza kwenye nafasi yake ili kijinasua. Uongozi umetengwa mbali na matendo binafsi ya mtu aliyekuwa kiongozi. Ujumbe murua kabisa.

Hukumu ya Ole Sabaya inashabihiana na ile ya kwenye shauri la madai la Mchungaji Mtikila dhidi ya Mzee Augustino Mrema. Kwenye shauri tajwa, mahakama ilitenganisha matendo/maneno ya mtu binafsi na uwaziri wake(Mrema).

Hukumu ya Sabaya itufunze na kutukumbusha kutenda ya haki na halali pale tunapobarikiwa kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali. Hukumu hiyo itukumbushe pia kuwa uongozi hautaweza kuwa kichaka cha kujificha pale ambapo jinai au madai yatakapoletwa dhidi ya mhusika.

Jinai hufa na mhusika tu, haizeeki!

Hukumu ile ni kwa mujibu wa ushahidi, sheria na haki.

Hata Sabaya mwenyewe amesema -
Mungu yuko kazini!

Hukumu haijapindisha sheria wala kupora haki - shahidi hapa ni Sabaya mwenyewe Idugunde, Kamanda Asiyechoka na binamu zao.
 
Hii sheria iwe msumeno kwa viongozi wa ngazi zote kuanzia juu. Hapo ndio tutasema haki inatendeka, kuna viongozi wao hawaguswi kwa vile tu wamejiwekea kinga, Ila makosa wanayofanya wakiwa madarakani yanahitaji adhabu kama hizi.
 
Jamii yetu bado ina shida kuzaa mtu kama Sabaya..what if angejificha alivyo Hadi anakuja kuwa Waziri au Rais?Si tungeipata Taifa zima?Kama Mobutu au Samuel Doe?..

Alifikaje kuwa hadi DC?...

Tunao kina Sabaya wengine wangapi kwenye leadership?Ambao wanaona kama ustaarabu ni udhaifu?
 
vipi kuhusu Gaidi Mbowe ambaye kwa muda mrefu amekitumia chama kama kichaka cha kutekeleza uhalifu, ugaidi, ujambazi wa kuvuruga amani ya Nchi na hata mipango ya kuuwa viongozi?!
kwa muda wote huo alipo kuwa mwenyekiti wa chama, je, unajua katengeneza wahalifu wangapi?
Mbowe anaweza kuwa mtu hatari sana kwa Nchi huenda kuliko hata huyo sabaya.
Mbowe hakufaa kabisa hata kuwa mwenyekiti wa chama.
 
Hii kesi tofauti, huoni wenzako wote wameingia mitini?

Hushangai hawajaandika utopolo huo kama wako bado?

Kwani Idugunde Kamanda Asiyechoka Elitwege na binamu zao hadi sasa wangekuwa hawajatimba bado kwa uelewa wako?
 
😂😂😂😂Elitwege kumbe ni machinga goli lake lipo vingunguti anauza pombe Kali Kama anabisha ajitokeze hapa.

😁😁

IMG_20211016_132442_593.jpg
 
vipi kuhusu Gaidi Mbowe ambaye kwa muda mrefu amekitumia chama kama kichaka cha kutekeleza uhalifu, ugaidi, ujambazi wa kuvuruga amani ya Nchi na hata mipango ya kuuwa viongozi?!
kwa muda wote huo alipo kuwa mwenyekiti wa chama, je, unajua katengeneza wahalifu wangapi?
Mbowe anaweza kuwa mtu hatari sana kwa Nchi huenda kuliko hata huyo sabaya.
Mbowe hakufaa kabisa hata kuwa mwenyekiti wa chama.
Mwendakuzimu na Mbowe,nani hakustahili hata kuwa kiongozi wa familia (baba)!??
 
Jamii yetu bado ina shida kuzaa mtu kama Sabaya..what if angejificha alivyo Hadi anakuja kuwa Waziri au Rais?Si tungeipata Taifa zima?Kama Mobutu au Samuel Doe?..

Alifikaje kuwa hadi DC?...

Tunao kina Sabaya wengine wangapi kwenye leadership?Ambao wanaona kama ustaarabu ni udhaifu?
Mkuu the Boss huyu Sabaya humu humu tumemuumbua tangu alivyofoji kitambulisho cha Tiss na kuleta vurugu hotelini.
 
Back
Top Bottom