Kiukweli nawapa Big up wapinzani

Hewa mkaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2012
743
500
Naanza kwa kusema, kama siyo kelele za wapinzani haya yote tungeyajuaje!!. Ni kutokana na wapinzani tukajua kwamba fedha za kodi zinaliwa hovyo. Ufisadi wa madini, maliasili na mikataba mingi mibovu, tumepata kujua kutokana na kelele za wapinzani.

Nakumbuka Kafulila na wengine imewacost ubungo ikiwa ni njia ya kuwaziba midomo ili mambo haya yafifie masikioni. Maskini Zito aliponea padogo kutokana na umakini wa wapiga kura wake.

Sasa tunaanza kuona matunda mara makinikia, mikataba mibovu kujadiliwa na wazembe kuwajibishwa kiaina. BIG UP.

Sasa ni lazima tupambane na hila zozote za kuwanyima nguvu wapinzani. Hila zozote za kuwapunguza idadi zitaturudisha kule tulikotoka.

Sisemi kwamba washike dola ila wawe wengi kusudi kelele yao iwe kubwa. Tumeanza kuona IPTL na mengi yanakuja.

Who knows siku moja tutasikia MEREMETA, ESCROW n.k Tukumbuke kuwa na rais mwenye uthubutu ni fursa ya pekee basi tumwongeze strength kwa kuwa na wabunge wa upinzani wengi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom