Kwa hyo Mungu ana ubaguzi?
Ikiwa mtu A ameenda macca kwa sababu ana fedha na amemudu kwenda anasamehewa dhambi Na vi pi mtu B ambae ameshindwa kwenda kwa sababu hana nauli dhambi zake hatasamehewa,,
In logic ? Lengo la kwenda macca n lipi?
Kuhiji Makkah ni kwa mwenye uwezo wa kwenda huko. Ama asiye na uwezo hana lawama. Hii ni katika Rehma na Fadhila za Allah kwetu. Kwenda kuhiji Makkah ukiwa na uwezo ni moja katika Nguzo 5 za Uislam.
Na kuna njia nyingi za kusamehewa madhambi, sio Hijja tu. Kama ulikuwa unadhani kuwa ni katika Hijjah tu ndio kuna kusamehewa madhambi, basi kuanzia Leo jua kuwa njia za kusamehewa madhambi sio ya Hijja peke yake.
Kuna kusamehewa madhambi katika Tawba ya kweli.
Kuna kusamehewa madhambi katika kuomba Istighfaar (kumuomba Allah Msamaha kwa kusema Astaghfirullah).
Kuna kusamehewa Madhambi katika 'Ibaadah nyengine pia;
Kuna kusamehewa Madhambi katika Swala, mpaka kwenye kutia udhu kuna kuanguka baadhi ya madhambi. Kuna kusamehewa madhambi katika Swala tano za Faradhi.
Kuna kusamehewa madhambi katika Swaumu/Funga, ziwe ni Funga za Waajib kama Funga ya Ramadhaan au Funga za Sunnah.
Kuna kusamehewa madhambi katika kufanya matendo mema, kwa mfano kutoa Swadaqah, na mlango wa Swadaqah katika Uislam ni mpana mno kiasi kwamba mpaka fakiri kwa kulingana na uwezo atakaokuwa nao bado anaweza kutoa Swadaqah kwa nafasi yake. Swadaqah katika Uislam hata kutoa shilingi hamsini ya kitanzania inaweza kuwa Swadaqah, hata kutoa kipande cha mkate inaweza kuwa Swadaqah, hata kutoa nguvu zako katika jambo lenye manufaa inaweza kuwa Swadaqah, chakula unachokiweka katika mdomo wa mkeo au watoto wako ni Swadaqah, hata mtu kustarehe na mkewe ni Swadaqah katika Uislam, hata mtu kuzungumza maneno mazuri ni Swadaqah, mpaka Muislam kukutana na Ndugu yake akatabasamu mbele ya uso wake ni Swadaqah katika Uislam. Kutoa na/au kusambaza Elimu Sahihi ya Dini ni Swadaqah. Kufanya jambo lenye kuwanufaisha watu ni katika Swadaqah, mpaka kuondoa udhia/kitu chenye kuudhi njiani (kama mwiba, uchafu, nk) ni Swadaqah. Kuna mlango mpana sana katika Swadaqah kwenye Uislam.
Ama Zakat, katika Uislam, ni Swadaqah maalum ambayo kiwango fulani cha mali kilichobainishwa na Shari'ah ambacho kinatolewa na Muislam aliyefikia uwezo fulani wa kimali uliobainishwa na Shari'ah, kiwango hiko ni haki aliyoifaradhisha/aliyoiwajibisha Allah kwa Muislam mwenye uwezo huo uliobainishwa kwenda kwa watu wanaostahiki kupewa (na wametajwa katika Shari'ah). Hiyo ni Zakat. Na asiyekuwa na uwezo wa kutoa Zakat, hana lawama.
Hivyo Zakat na Swadaqah kuna tofauti. Kiufupi Zakat ni aina ya Swaqadah ambayo imewajibishwa na iko katika kiwango maalum, inatolewa kwa watu maalum, na watu wenye uwezo maalum katika wakati maalum kama ilivyobainishwa katika Shari'ah.
Ila Swadaqah ambayo siyo Zakat, inatolewa kwa kiwango chochote bila kujali uwezo, kidogo au kikubwa, kwa yoyote yule awe ndugu, tajiri, masikini, fukara, Muislam au asiye Muislam, wakati wowote, ni jambo ambalo asiyelifanya hapati dhambi ila akilifanya anapata thawabu.
Kuna Swadaqah yenye kuendelea. Yaani kwa mfano Muislam akaenda kutoa, mfano, tofali moja tu kwenye kujenga Msikiti au tuseme akawa na uwezo akatoa labda nondo moja tu au mtu aliyejitolea hata hamsini ya kitanzania kama mchango wake au akaona mimi nitajitolea nguvu zangu kujenga kwa sababu ninaweza kujenga au ninaweza kubeba mizigo, basi ana sehemu yake katika thawabu ambazo ataendelea kuzipata muda wa kuwa Msikiti ule bado upo.
Na Swadaqah ni katika Sababu ya kufutiwa madhambi.
Kuna njia nyingi sana sana sana za kusamehewa Madhambi.
Kwa Muislam kuna kufutiwa Madhambi mpaka katika Mitihani na mabalaa yanayomsibu. Katika Uislam, Muislam hata akiumwa basi kuna sehemu katika Madhambi yake anafutiwa, akipata tatizo, sehemu katika madhambi yake anafutiwa, akiwa na huzuni, sehemu katika madhambi yake anafutiwa...
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislamu hatopatwa na tabu, wala maradhi, wala hamu wala huzuni wala udhia wala ghamu [sononeko] hata mwiba unaodunga isipokuwa Allaah Humfutia madhambi yake kwa sababu ya hayo)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Ninamshukuru Allah kwa Neema ya Uislam na Sunnah.